Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-30

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


alifariki
Hata hivyo, mmoja alifariki juma moja baadaye. [1]
ama
Aliendelea kuelezea jinsi maalbino wanavyouawa kikatili, akisema wengi walikufa kwa kushindwa kupata huduma mapema ya kuzuia damu baada ya ama kukatwa mikono ama miguu na majitu hayo katili yenye imani potofu kwamba, viungo hivyo vinaweza kumpatia mtu utajiri. [2]
amani
Hata katika hotuba ya Rais siku alipoapishwa rasmi kuwa Rais aliweka bayana kuwa Marekani ni rafiki wa mataifa yote, kila mwanaume, mwanamke na mtoto ambaye anapenda amani na heshima" alisema balozi huyo. [3]
ana
Kwa vile kauli hiyo haijaleta madhara mpaka sasa Waziri Mkuu ana uchochoro wa kupita ili kujisafisha. [4]
anaweza
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Imani Madega amesema kipa wa timu hiyo, Mserbia Obren Curkovich kwa sasa anaweza kushiriki Kombe la Shirikisho baada ya leseni yake kukamilika. [5]
anga
Kazi nyingine iliyofanywa na kikundi kazi hicho, ni kubaini kwa ufasaha matatizo yanayoikabili kampuni hiyo, na kuchunguza vyanzo vyake kwa ajili ya kutoa ushauri wa kuboresha huduma za usafiri wa anga. [6]
angeandika
Mwandishi angeandika, madhumuni ni kuwa na mamlaka yenye uwezo wa kutekeleza majukumu yaliyoainishwa kwenye sera. [7]
au
Pinda alisema mtu anaposikia au kusoma taarifa za mauaji ya albino, hawezi kupata hisia juu ya mateso wanayoyapata, sawa na anayewasikiliza watu walionusurika kufa au walioshuhudia vitendo hivyo vikitendeka. [8]
azidi
Naomba Mungu azidi kuwajaalia nguvu, maisha marefu na mafanikio kwa mwaka huu mpya. [9]
bado
Kimsingi, Tanzania bado haijasaini wala kuridhia mkataba huu. [10]
bandia
ASILIMIA 40 ya bidhaa zinazoingizwa nchini ni bandia. [11]
baraza
Mfalme alisema kuwa maafisa watendaji hao wamesimamishwa kazi kufuatia agizo la baraza la madiwani wa halmsahuri hiyo lililoketi Januari 27 kutokana na tuhuma ya kusababisha mifuko 55 ya saruji kuganda, mifuko 45 kutumika kiholela na kususa kusimamia mradi huo. [12]
bize
Wengi wao ukiwaambia suala hilo hujifanya ‘bize’ na kuonyesha manjonjo kwenye usukani. [13]
bodi
Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo, Nicolaus Mbwanji, alisema jana kuwa utaratibu huo utaanza kutumika katika mwaka mpya wa fedha wa 2009/2010 kwa kuanzia na wanafunzi wa fani za sayansi. [14]
bomba
MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam, (Dawasco), imewakatia maji wananchi zaidi ya 500 wa maeneo ya Boko baada ya kubainika wamejenga nyumba juu ya bomba la mamlaka hiyo na kujiunganishia maji kiholela. [15]
bosi
Pinda alisema anapata taabu kujibu swali hilo, kwa sababu hawezi kuyatolea maelezo mambo yaliyozungumzwa na bosi wake na wala hajui kama ni kweli rais alisema kama vyombo vya habari vilivyoripoti. [16]
cha
Alisema alielezwa kuwa, wauaji wanachokifanya ni kumshambulia albino na kumkata kiungo wanachokitaka kwa kutojali hali wanayomuacha nayo kama ni mateso, kufa au kupona hivyo alipatwa na uchungu kiasi cha kujikuta anatamka kuwa, watu wanaokutwa wakitenda hayo nao wanapaswa kuadhibiwa papo hapo. [17]
chako
Angalia pia kiherehere chako kisijekuharibia. [18]
dhumuni
Alisema dhumuni ni kuwa na mamlaka yenye uwezo wa kutekeleza majukumu yaliyoainishwa kwenye sera. [19]
es
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam, Sheikh Ramadhan Sanze alisema Pinda alifanya kosa la kiufundi kwa kuwa yeye ni mtendaji mkuu wa serikali, hivyo hakupaswa kusema jambo linalopingana na msimamo wa serikali, sheria na katiba ya nchi. [20]
eti
Sipendi nichague wachezaji eti kwa kuwa leo ninao wengi kutoka Mwanza na Mbeya basi niwapunguze na kuangalia wengine kutoka mikoa mingine. [21]
feki
Mhesa anaeleza baadhi ya bidhaa bandia na athari zake kwa jamii:"Magari yamekuwa yakipata ajali kila mara na kusababisha vifo kwa sababu ya matairi na breki feki zinazotumiwa na magari hayo. [22]
fikra
Ni wazi kuwa kusoma machapisho kunasaidia katika maendeleo ya nchi, hilo litawezekana tu kama wananchi wenyewe watabadili fikra zao. [23]
fukwe
Alisema viongozi hao wameshindwa kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kituo cha utalii licha ya kuwa na fukwe nyingi na kwamba, hiyo ni kwa sababu wameshindwa kuziendeleza fukwe hizo na kuzifanya zipendeze. [24]
gani
Kwa mfano wenzetu kule Nairobi, Kenya wanayo, lakini sisi hapa sijui tumepitiwa na ugonjwa gani. [25]
goma
Mfano mzuri ni hili neno goma. [26]
haja
Inawezekana kabisa kwamba zilionekana kuwa hazikidhi haja iliyozifanya zikaundwa. [27]
halifai
Ni vema ikaeleweka kuwa neno dhumuni siyo sahihi kwani halifai kutimiwa kama lilivyotumika hapo juu. [28]
halisi
Katika bidhaa halisi, tarehe hizo zinaandikwa kwa kutumia mashine maalum au kompyuta. [29]
hana
Kwa upande wake Mloka amesimamishwa kazi kutokana na kuwadanganya wajumbe waliokwenda kukagua mradi huo ambapo mtendaji huyo alidai hana taarifa za kuwepo kwa mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kasanga. [30]
hao
Wanafunzi hao pia waliitaka serikali itoe mikopo kwa asilimia 100 kwa wanafunzi wote na vitivo vyote, badala ya kutenga makundi ambayo hata hivyo, hayazingatiwi kutokana na baadhi ya watoto wa wenye uwezo kulipiwa zote na wale wa masikini wakiwekwa kwenye makundi ya kuchangia. [31]
hasa
Mauaji ya albino yamekuwa yakitikisa nchi na hasa katika eneo la Kanda ya Ziwa, licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi, mashirika ya kutetea haki za binadamu, vyama vya walemavu na watu binafsi. [32]
hata
Alisema serikali imeliagiza jeshi la polisi kutumia maarifa yake, hata kama itabidi kutumia gharama kubwa, ili kuwatia mbaroni watu wote wanaojihusisha na mauaji hayo. [33]
hati
MAWAKILI wanaomtetea aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Joachimu Liyumba, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh221 bilioni wamesema wanaendelea kushughulikia hati kwa ajili ya dhamana ya mteja wao. [34]
hawa
Kwa faida ya Watanzania tusikubali hawa wanaogomesha maendeleo. [35]
hayo
Waziri Mkuu alisema hayo baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed, kumtaka atoe ufafanuzi kuhusu kauli aliyoitoa hivi karibuni akiwa katika ziara Kanda ya Ziwa, kuwaruhusu wananchi kuwaua watu watakaokutwa wakimchinja albino. [36]
hicho
Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma, Salim Biman alisema jana kuwa mkutano huo, utafanyika katika viwanja vya Kibandamaiti ambapo mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa chama hicho , Profesa Ibrahim Lipumba. [37]
hii
Nchi hii haina dini na kwa hiyo haingozwi na sheria za dini bali inaongozwa na sheria za nchi, kwa hiyo Pinda alipaswa kuangalia sheria ya nchi kwanza kabla ya kutoa agizo lake," alisema Sheikh Sanze. [38]
hili
Tunaling'oa bomba lote hili, tutalihamishia sehemu nyingine. [39]
hizi
Siku hizi watu wakioa wasipopiga picha pale baharini wanajiona kama hawajakamilika, lakini baadaye nikasikia kuwa halmashauri imepiga marufuku kupiga picha hapo. [40]
huenda
Ninachokiona ni kwamba huenda kuna ulegelege fulani katika kutekeleza ahadi hiyo. [41]
huko
Washindi hao watano ambao wataambatana na timu hiyo watagharamiwa kila kitu kwa siku zote watakazokaa huko ikiwemo na usafiri wa kwenda na kurudi. [42]
huo
Alisema, athari ya kauli kama hizo zinaweza kusababisha migogoro kati ya dini na dini nyingine, kabila moja na jingine au dhehebu moja na jingine kama wananchi watautumia wito huo. [43]
huu
Kwa sasa utoaji mikopo hautafuata 'division' (daraja), bali utakuwa ukizingatia udahili wa wanafunzi katika vyuo na kwa utaratibu huu, chuo kitapewa idadi ya wanafunzi watakaokopeshwa kulingana na programu zake na idadi itapangwa kulingana na vipaumbele vya taifa, kama itakavyoelekezwa na serikali, ikiwemo elimu na sayansi," alieleza. [44]
huwa
Kwamba katika sheria nyingi zitumikazo sasa ni chache miongoni mwazo ambazo zitakuwa ni mpya au ngeni katika jamii hiyo, zaidi ya hapo sheria nyingi huwa ni marekebisho na masahihisho ya sheria za zamani ambazo ama zimepitwa na wakati, au zimeonekana kuwa zilikuwa zikitumika kwa makosa kwa maana ya kwamba hazikuwa zimekusudiwa kwa watu au jamii hiyo. [45]
huyo
Steven Ekovich amesema dunia isitegemee maajabu kutoka kwa Rais huyo mpya kwa kuwa hawezi kuwa na Sera zake binafsi. [46]
huyu
Kikubwa ambacho tulikua hatujakamilisha kwa golikipa huyu ni vivuli vya hati yake ya uhamisho ambapo CAF walikua wakihitaji lakini tayari tumefanya mazungumza na chama cha soka nchini Serbia na tumeshamalizana na tatizo hilo," alisema Madega. [47]
idadi
Alifafanua kuwa wakati akiwa kwenye ziara hiyo iliyokuwa maalumu kwa ajili ya kukemea na kupanga mikakati ya kukabaliana na vitendo hivyo, idadi ya maalbino waliouawa walikuwa 30 na baada ya kukemea vitendo hivyo, ghafla akapewa ripoti ya kuuawa wengine wawili, jambo ambalo lilizidi kumuudhi na kumchanganya. [48]
ijayo
SHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF, limetangaza mikakati yake muhimu ambayo limedhamiria kuifanyia katika kipindi cha miaka minne ijayo. [49]
ikawa
Inawezekana ikawa walizochuma au walizojichumia. [50]
ikiwa
Alisema katika kufanikisha mpango huo mpya, bodi yake inatarajiwa kudahili wanafunzi 60,000 watakaokopeshwa ikiwa ni zaidi ya mwaka jana walipodahili 55,685 na kwamba, mwaka huu wanatarajia kutumia kiasi cha Sh175 bilioni. [51]
imara
Inahitaji kuwa imara ili iweze kutoa wachezaji wa uhakika. [52]
ina
Naibu waziri serikali , inachukua hatua mbalimbali za kudhibiti ukiukwaji wa haki za binadamu na ina nia ya dhati ya kuridhia na kutekeleza yale yalioainishwa katika mikataba inayopinga hali hiyo. [53]
ipo
Pinda alisema kuwa serikali ipo tayari kupokea maoni kutoka kwa watu mbalimbali, yanayoweza kusaidia kupata mbinu ya kukomesha kabisa mauaji hayo, ili kuiokoa jamii hiyo ya albino. [54]
iwe
Tunashauri kwamba, kilio cha wanafunzi ni kupewa mikopo kwa asilimia 100 na hata katika madai yao, hawakujigawa katika makundi, hivyo ili kuondoa tatizo hilo, kama serikali imeamua kutoa mikopo kwa asilimia 100 iwe kwa wanafunzi wote na wote waanze pamoja. [55]
jukumu
Lakini pia Kamanda Kombe, katika kutekeleza agizo la Waziri Masha, nilidhani kwamba angeunda timu ambayo ingekuwa na jukumu la ukaguzi na uhakiki wa magari yote kwa kuanzia na yale makubwa yaendayo mikoani ili kubainisha mabovu na kuchukua hatua stahili ikiwemo kuyafutia kabisa leseni. [56]
juzi
Rais Kikwete alitoa agizo hilo juzi jioni katika Ukumbi wa Karimjee wakati wa chakula cha jioni, kilichoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kumpongeza kwa mafanikio ya serikali yake katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. [57]
kadhaa
Mlima ya Oldonyo Lengai ulioko chini ya mamlaka ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro (NCCA) ulilipuka mara kadhaa mwaka jana na mwaka juzi. [58]
kali
Ajali hizi zimetokea huku kukiwa na agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha ambaye aliwaagiza polisi wa usalama barabarani kutoruhusu magari mabovu kutembea na kutangaza kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva wote watakaosababisha ajali hizo. [59]
kama
Mara akaanza kububujikwa na machozi na baada ya sekunde kama 15, alichukua kitambaa chake akajifuta. [60]
kata
Akielezea mabadiliko hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, George Nyatega alisema wanafunzi watakaopata mikopo watapaswa kupitishwa na bodi za elimu za kijiji, kata, tarafa na wakuu wa wilaya, ili kuwatambua zaidi na kuepuka udanganyifu kwa waombaji. [61]
kibali
Kwa mujibu wa Biman, Jeshi la Polisi Zanzibar limeridhia na kutoa kibali cha kufanyika Mkutano huo akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano muhimu. [62]
kikazi
Migogoro hii ya kikazi ilikuwa ikichukua miaka mitatu hadi mitano lakini sasa utatuzi wa migogoro ya kikazi itachukua siku 21 hadi 30 tu kutokana na kutumika kwa sheria hizi zilizoandikwa kwa Kiswahili. [63]
kila
Alisema bodi imejiandaa kufungua ofisi zake katika kila kanda na kwamba, wataanzia Dodoma na Zanzibar, lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu na vyuo. [64]
kile
Kama mnaona kile nilichofanya ni makosa naomba mnivumilie. [65]
kina
Kikosi cha Maximo kina wachezaji watatu kutoka Zanzibar ambao ni Nadir Haroub 'Cannavaro', Farouk Ramadhani, Abdi Kassim 'Babi' pamoja na kocha msaidizi Ally Bushir ambaye Maximo amefanya naye kazi kwa zaidi ya miaka miwili sasa. [66]
kiume
Ilimchukua dakika tano kwa watoto hao, sita wa kiume na wawili wa kike kuzaliwa alianza saa 4:43 hadi saa 4:48 asubuhi kukamilisha kazi hiyo ngumu iliyoshuhudiwa pia na kundi kubwa la wauguzi na wataalamu wengine. [67]
kiunganishi
Ya ni kiunganishi muhimu wakati wa kutoa maelezo. [68]
kiwanda
Mfanyabiashara huyo ambaye hakumtaja jina anajenga kiwanda katika Ubungo. [69]
km
Jumanne Tluway alishinda mbio hizo za km 42 mwaka jana kwa kutumia saa 02:15:37 akifuatiwa na Andrea Sulvin (02:16:22). [70]
kocha
Kombo alisema hayo katika baraza la wawakilishi la Zanzibar na kusisitiza watampeleka Maximo visiwani humo kwa gharama zao ingawa alikuwa amesahau kwamba kocha huyo amefanya ziara visiwani humo mara mbili kwa ajili ya kusaka vipaji, huku Tanzania Bara akiwa amefanya katika baadhi tu ya mikoa. [71]
kuanza
Jana bodi hiyo ilitangaza rasmi marekebisho ya taratibu za mikopo kwa kukubali kuanza kuwakopesha wanafunzi wa sayansi kwa asilimia 100 kuanzia mwaka wa fedha wa 2009/2010, pamoja na kuongeza fedha za kiwango cha fedha za vitabu kutoka Sh120,000 hadi Sh200,000 kwa mwaka kwa wote. [72]
kuchezesha
Kulikuwa na habari za kusakiziana za kuchezesha mechi hiyo. [73]
kuelewa
Kwa msomaji wa kawaida wa mitaani ambaye siyo msomi hataweza kuelewa neno 'bize'. Kwa neno manjonjo tunaweza kupata maneno kama kwa kujidai au kwa majivuno. [74]
kufika
Ni dhahiri kwamba, agizo hilo la rais linakwenda na wakati kwa vile ongezeko kubwa la magari ambayo badala ya kupunguza tatizo la usafiri, yamekuwa kero kwa wananchi kutokana na msongamano unaosababisha watu wachelewe kufika wanakokwenda. [75]
kufuta
Wakati hayo yakitokea bungeni, baadhi ya viongozi wa dini nchini, wamemtaka Waziri Pinda kukiri kosa, kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa mamlaka za kisheria, Bunge na Wananchi. [76]
kuingia
Hata hivyo maofisa hao wa Dawsco walipotaka kuingia katika baadhi ya nyumba ili kufanya ukaguzi iwapo kuna maji yanayosambazwa na mamlaka hiyo wafakazi hao walizuiwa na walinzi kuingia ndani. [77]
kuja
Ukweli ni kwamba kila mtu ambaye ni shabiki wa Yanga na mpenzi wa soka yoyote atapenda kuangalia mechi aweze kuja kushudia mchezo huu bila ya kuwepo kwa kikwazo cha viingilio vikubwa, alisema mwenyekiti huyo. [78]
kujadili
UONGOZI wa klabu ya Simba umesema kuwa utaanza kujadili suala la kutafuta Katibu na Mhazini wa kuajiliwa mara baada ya mechi yao na JKT Ruvu. [79]
kukataa
Katika lugha ya mitaani neno sakizia linaweza kuwa na maana ya kusingizia au kukataa jambo kiujanja. [80]
kukerwa
Rais pia alieleza kukerwa na uamuzi wa viongozi wa jiji kuwaruhusu wafanyabiashara wa magari makubwa ya mizigo kuegesha katika eneo la Jangwani. [81]
kukosa
Liyumba na Meneja Mradi wa benki hiyo, Deograthias Kweka ambao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumanne wiki hii, bado wameendelea kusota rumande kwa kukosa dhamana. [82]
kula
Lakini pia mfumo wetu wa kusimamia matumizi sahihi ya barabara nao unapaswa kuangaliwa upya kwani ndiyo unaotoa mwanya kwa baadhi ya askari waliopewa jukumu hilo kula rushwa hivyo kuzidi kujenga mazingira hatari ya kutokea kwa ajali. [83]
kumpa
Akademiki Mwenyenchi ambaye inasemekana alikuwa anaona hakuna haja ya kumpa Bi Elimu hata punje ya mchele na badala yake achukue chakula chote yeye mwenyewe. [84]
kuna
Kuhusu tatizo la mipango miji, Rais Kikwete alisema ingawa viongozi hao wameshindwa kulifanya Jiji la Dar es Salaam liweze kupendeza na hata kuwa kitovu cha utalii na kwamba, ingawa kuna wataalamu, lakini wanashindwa kuutumia ujuzi wao. [85]
kununua
Alisema tatizo la usafiri jijini linasababishwa na kutokuwa na usafiri bora wa umma, jambo ambalo linawafanya watu walazimike kununua magari binafsi. [86]
kuona
Sipendi taifa Stars iingie katika masuala ya siasa, pia sifurahii kuona viongozi wanazungumza mambo bila kuyafanyia utafiti kitu ambacho kinaweza kufanya uchinganishi na chuki ndani ya timu yetu. [87]
kusaka
KOCHA wa Taifa Stars, Marcio Maximo amejibu tuhuma za Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mahmoud Thabit Kombo wa Zanzibar kwamba amekuwa akibagua visiwa hivyo katika suala la kufanya ziara ya kusaka vipaji kwa kuwa zaidi upande wa Tanzania Bara. [88]
kushinda
Kaduguda alisema mapunziko hayo ya timu ya Taifa watayatumia vizuri ilikuakikisha kuwa timu yao inaitetea nafasi waliokuwanayo sasa kwa kushinda mechi zote tisa zilizobaki ilikumaliza ligi. [89]
kushudia
Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega alisema wameamua kuweka viingilio vya chini kuwapa nafasi mashabiki wake wengi kushudia mchezo huu. [90]
kusikia
Hata siku moja sijawahi kusikia watu wanaulaumu kwamba Taifa Stars ina wachezaji wengi kutoka Mwanza na Mbeya. [91]
kutafakari
Haya ni mawazo yangu tu katika kutafakari njia ambazo agizo la Waziri Masha lingetekelezwa. [92]
kuwa
Hamadi alisema katiba ya nchi inamlinda mtu kupewa nafasi ya kujitetea, hivyo akamtaka waziri afafanue maana ya kauli yake, kwa kuwa ni kinyume na taratibu ambazo nchi imejiwekea katika kuhakikisha haki inapatikana. [93]
kwake
Akizungumza jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Maximo ameiambia Mwananchi kwamba wasitegemee suala la upendeleo maalum kutoka kwa kikosi chake kupitia suala la Ubara na Uzanzibar kwa kuwa Stars si timu ya kisiasa. [94]
kwenda
Alisema baada ya kwenda kukagua katika shule hiyo, wajumbe hao walikuta mifuko 115 ya saruji hali iliyowalazimu kupendekeza kwa halmashauri hiyo kusimamishwa kwa mtendaji huyo. [95]
la
Alielezea pia kuhuzunishwa zaidi na tamko la Bunge la Jumuiya ya Ulaya (EU) la kulaani mauaji hayo, kana kwamba wao wanaguswa sana na suala hilo kuliko Serikali ya Tanzania. [96]
leseni
Desemba 8, mwaka jana Mamlaka ya anga nchini (TCAA) iliipokonya ATCL leseni ya kurusha ndege zake ndani na nje ya nchi kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo suala la usalama. [97]
lina
Tunaelewa kwamba, rais hakumaanisha kuwa jiji lina fedha za kutosha kufanikisha mkakati huo, bali ubunifu wa hali ya juu unaoweza kutoa changamoto ya kupatikana kutoka kwa wahisani au wafadhili na hata mkopo kutoka taasisi za fedha za ndani na nje ya nchi. [98]
lipo
Hivyo huwa ni jukumu la upande wa utetezi kupekuwa na kutafiti kama sheria au kosa ambalo mtu wao anakabiliwa nalo lipo chini ya sheria husika. [99]
lugha
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya anasema kuwa tatizo kubwa lililokuwepo awali lilitokana na sheria za kazi kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza hivyo kusababisha wafanyakazi wengi kuingia katika migogoro isiyokuwa ya lazima kutokana na kushindwa kuzitafsiri sheria hizo. [100]
magazeti
KWA mara nyingine naendelea kuwapa wasomaji maelezo na ufafanuzi kuhusu makosa yanayojitokeza katika magazeti na namna ya kuyasahihisha. [101]
maisha
Licha ya kitita cha zawadi hiyo ya fedha wanafunzi watakaoshiriki pia watapata fursa ya kujenga mtandao wa mawasiliano ambayo yatadumu katika kipindi chote cha maisha yao. [102]
makala
Waandishi na wahariri wa makala wameshindwa kuliona kosa hili na kulisahihisha. [103]
malengo
Adre' alisema malengo ya Marekani siku zote ni kuimarisha uhusiano na nchi zote, hivyo haitasita kutoa msaada wa kimaendeleo pale itakapoonekana inahitajika kufanya hivyo. [104]
maofisa
Alivishukuru vyuo mbalimbali nchini kwa kutoa maofisa wake katika kukusanya matatizo ya wanafunzi, kuhusiana na mikopo na kuyashughulikia kwa utaratibu uliopangwa na bodi hiyo. [105]
mapacha
Madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo wameweka historia mpya kwa kusaidia kuzaliwa kwa watoto hao mapacha ikiwa ni mara ya pili kutokea katika historia ya Marekani. [106]
mara
Pinda alisema alipokuwa katika ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, alipata taarifa za kusikitisha kuhusu mauji ya albino na mara kesho yake habari zikatoka kwenye vyombo vya habari kwamba, albino mwinge kauawa. [107]
mauzo
Alipokuwa njiani kupeleka benki fedha za mauzo za kampuni hiyo amefariki dunia. [108]
mawazo
Alisema Watanzania wana mawazo tofauti ya ama kufuta au kuendelea na adhabu ya kifo na kwamba serikali kwa upande wake, inalifanyia kazi kazi kwa kutumia Tume ya Kurekebisha Sheria. [109]
mbele
Alisema mechi hiyo itakuwa ngumu sana kwani wanacheza dhidi ya timu ambayo hawaijui, lakini watahakikisha wanatoka na ushindi mkubwa kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele mechi ya marudiano. [110]
mbio
WANARIADHA mbalimbali maarufu wa ndani na nje ni miongoni mwa waalikwa watakaoshirik mbio za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Machi Mosi, Moshi moani Kilimanjaro. [111]
mdogo
Biman alisema katika mkutano huo, Profesa Lipumba atajibu hoja mbalimbali za Rais Jakaya Kikwete, zikiwemo za, CUF kufuta ndoto ya kuiongoza Zanzibar, wanaobeza maendeleo ya CCM ni walevi tende na kuzungumzia uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Mbeya vijijini. [112]
mfumo
Sera mpya ya uchangiaji elimu ya juu, ambayo iliweka mfumo wa kutoa mikopo kufuatana na makundi, imesababisha wanafunzi kugoma kwa madai kuwa unalenga kuwanyima haki watoto wa masikini kupata elimu ya juu na hatimaye vyuo kufungwa. [113]
midomo
Unajua midomo kazi yake ni kusema. [114]
miji
Rais pia alisisitiza ujenzi wa miji mipya ya pembezoni mwa jiji na kuweka huduma zote muhimu kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa watu katikati ya jiji. [115]
mikopo
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imefanya mabadiliko ya utaratibu wa utoaji mikopo kwamba, sasa watatoa asilimia 100 kwa wanafunzi wa vitivo mbalimbali kulingana na vipaumbele vya serikali. [116]
mimi
Hata mimi nilikuwa nikienda kucheza pale, na pale palikuwa pana angaliwa sana wala hakuna maji yaliyokuwa yanajaa, lakini sasa mmeliachia na watu wamelitumia kwa matumizi yao. [117]
mke
Utawala wa Obama ambao Waziri wake wa mambo ya nje ni mke wa zamani wa taifa hilo tajiri duniani, Hillary Clinton umesema utahakikisha unaimarisha uhusiano wake na Tanzania. [118]
mkoani
Katika hatua nyingine Rais Jakaya Kikwete amepokea ripoti ya awali ya milipuko ya mara kwa mara ya jivu la volcano kutoka kwenye mlima Oldonyo Lengai mkoani Arusha kutoka kwa wataalamu wa masuala ya Volkano wa Marekani. [119]
mmoja
KUNDI la madaktari 46, katika hospitali ya Kaiser Pemanente Bellflower Los Angels, Marekani, walifanikiwa kumsaidia mama mmoja kujifungua watoto wanane. [120]
mradi
HALMASHAURI ya Wilaya ya Morogoro imewasimamisha kazi maafisa watendaji watatu wa kata na vijiji wa wilaya hiyo kutokana na uzembe uliosababisha mradi wa TASAF wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa ya shule ya sekondari ya kata ya Kasanga kukwama huku Halmashauri hiyo ikipata hasara ya zaidi ya Sh 1.6 milioni. [121]
msingi
Cha msingi ni kukiri kosa, kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa mamlaka za kisheria, Bunge na Wananchi" alishauri Sheikh Sanze. [122]
muda
Wapinzani pia walimtaka Pinda atoe maelezo yanayodaiwa kuwa yalitolewa na Rais Jakaya Kikwete kisiwani Pemba kwamba, aliwashangaa wakazi wa eneo hilo kuwachagua watu ambao hawawezi kuunda serikali na ambao watachukua muda mrefu kupata nafasi hiyo. [123]
mwa
Alisema katika kumbukumbu za serikali, hadi mwishoni mwa mwaka jana vikongwe 2,866 walikuwa wameuawa kwa imani potofu kuwa ni wachawi. [124]
na
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameangua kilio bungeni kuonyesha uchungu alio nao dhidi ya vitendo vya mauaji ya kikatili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), hivyo kuyeyusha hoja ya wabunge wa upinzani waliokuwa wamepania kumbana, ili ajiuzulu kwa madai kwamba, alitoa amri ya kuua wauaji ambayo ni kinyume na katiba ya nchi. [125]
nalo
Suala la kwamba kuna wachezaji wengi kutoka bara nalo pia si kitu cha kuzungumza namna hiyo kwa kuwa tuna wachezaji kutoka Zanzibar. [126]
nasema
Sawa tumefungwa mechi tatu mfululizo, inaogopesha lakini mimi nasema tuna uwezo mkubwa wa kushinda Jumapili hivyo hakuna kutabiri hapo. [127]
naye
Aidha katika siku za karibuni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwa katika ziara mikoa ya kanda ya Ziwa alinukuliwa akisema "Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye amueni cha kumfanya kwani sasa viongozi wote tumechoka. [128]
ndani
Kwanza, ni lazima ieleweke wazi kuwa Marekani inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi, ni wazi kuwa fedha nyingi zitatumika kurekebisha hali hiyo, ndani ya Marekani"alifafanua. [129]
ndio
Madega pia, aliongeza kuwa wadhamini wao watakuwa na kazi ya kutoa misaada hiyo kwa Yanga kila mwaka kwani wao ndio mabingwa pekee Tanzania. [130]
ndiye
Pamoja na hayo, Mhesa anasema mtumiaji wa bidhaa hizo ndiye mwenye dawa ya kumaliza tatizo la kuwepo kwa bidhaa bandia na athari zake kwa jamii. [131]
ngazi
Kuhusu uboreshwaji wa Katiba alisema kuwa zitatayarisha kanuni zinazotamkwa ndani ya Katiba na nyingine nyingi zinazostahili kuwepo, kuundwa kwa baraza la usuluhishi wa mambo ya soka na kuendeleza marekibisho ya katiba hadi ngazi ya wilaya. [132]
nini
Kwa nini nasema hivyo? Adhabu zinazotolewa kwa kukiuka Sheria ya Usalama Barabarani sio kali tena. [133]
nyie
Ujumbe wetu kwa wapinzani wetu ni rahisi kabisa, kuwa nyie endeleeni kuwachagua mnaowataka, lakini endeleeni kutukabidhi sisi serikali na dhamana ya kuleta maendeleo. [134]
nyuma
Rais pia alishangazwa na uamuzi wa jiji kuwazuia wananchi kupiga picha za harusi ufukweni, nyuma ya Ikulu na kubadilisha matumizi ya ardhi iliyoachwa wazi. [135]
pa
Mnawabana kiasi kwamba, hawana hata pa kupumulia, hivi ni vitu vidogo tu wapeni uhuru," alisema Rais Kikwete. [136]
peke
Pamoja na kupongeza kwa juhudi zilizofanywa na bodi katika kulipatia ufumbuzi tatizo hilo lililosababisha wanafunzi kufanya fujo na vyuo kufungwa, kuwakopesha wanafunzi wa sayansi peke yake kunaweza kuleta matatizo vyuoni, kwa kuwafanya wengine waonekane au wajione bora kuliko wenzao, jambo linaloweza kuibua mgogoro mwingine. [137]
pekee
Hawa pia watapewa badala ya wale wa serikali pekee. [138]
pengine
Kama wamevamia basi watafutieni mahali pengine ili vijana wapate mahali pa kuchezea," aliagiza. [139]
pia
Waziri Pinda aliwaomba radhi watu walioudhika kutokana na matamshi na pia akimuomba Mungu amsamehe iwapo amewakosea. [140]
pili
Alisema lengo la mabadiliko hayo ni kuondoa pengo kutoka kundi moja hadi lingine na kuleta uwiano mzuri katika makundi ya uchangiaji na kuwa sasa mikopo haitatolewa kwa kufuata madaraja ya viwango vya kufaulu vinavyotumika sasa (daraja la kwanza na la pili). [141]
polisi
Hata hivyo, alisema kuwa katika ziara hiyo, ambayo iliwahusisha pia baadhi ya mawaziri, wabunge, viongozi wa polisi, viongozi wa dini na kisiasa, waliahidi kushirikiana kuhakikisha kuwa wanakabiliana na kulimaliza tatizo. [142]
raia
Makosa kama haya yalikwishafanyika katika mfumo mzima wa sheria zetu nchini, hali iliyosababisha raia wengi wasiojua sheria kuumizwa. [143]
saa
Biman alisema Profesa Lipumba atazungumzia kauli hizo kwenye mkutano huo ambao utafanyika kuanzia saa 8:00 mchana ambapo pia atazungumzia chaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini uliofanyika hivi karibuni na mgombea wa CCM kuibuka kidedea. [144]
salaam
Mechi hiyo ambayo itachezwa Jumamosi Saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam utakuwa na viingilio vya aina nne. [145]
sana
Naomba Mungu anisamehe kama nimewakosea," aliomba Waziri Mkuu na kuongeza kuwa serikali imechukizwa sana na mauaji hayo ya kikatili. [146]
sanifu
Lengo ni kuyafanya magazeti yetu yawe ni chanzo cha Kiswahili sanifu ndani na nje ya nchi yetu. [147]
sera
Akizungumza kutoka Paris nchini Ufaransa, Profesa huyo alisema Rais Barack Obama, kama ilivyo kwa watangulizi wake, ataongoza kwa kufuata sera na maslahi ya taifa la Marekani. [148]
sh
Marekebisho mengine ambayo bodi imefanya ni kuongeza kiwango cha mikopo kwa vitabu na viandikwa (stationary) kutoka sh. [149]
si
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Valentino Mokiwa alisema kauli ya Pinda ya kutaka aliyeua albino auawe si sahihi kwa sababu mtu akimuua aliyeua ni muuaji na ana kosa kisheria. [150]
siyo
Huu siyo utendaji kazi makini, ukaguzi na uhakiki wa magari hasa ya abiria unapaswa kuwa wa kudumu kwani maisha ya watu yanakuwa hatarini kila kukicha. [151]
tabia
Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Utamaduni, Rose Sayore anasema kuwa bado kuna changamoto kubwa katika kufanikisha Watanzania wengi wanapata haki zao, kutokana na tabia ya kutopenda kusoma kwa umakini machapisho mbalimbali. [152]
tamati
Yapo maneno mengine tunayalazimisha kuyanyambua na kuweka kiambishi tamati. [153]
tarehe
Kwa mujibu wa taarifa za FCC, bidhaa bandia hutambuliwa kwa kutumia tarehe ya kuanza kutumika kwa bidhaa na mwisho wake. [154]
tatu
Walipofikiswha mahakamani hapo jana, wakili anayemtetea Liyumba, Alexander Kyaruzi aliiambia mahakama kuwa, wanazo hati tatu za nyumba zenye thamani ya Sh600 milioni kwa ajili ya mteja wao. [155]
tena
I can't tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena). [156]
tishio
Kama ilivyo kwa fani nyingine, elimu ya udereva inastahili kupewa nafasi ili kuwapata madereva makini watakaofuata sheria ili kupunguza ajali hizo ambazo kwa sasa zinakuwa tishio kwa maisha ya watu. [157]
tofauti
Hii ni changamoto kwa kuwa Rais huyo anafanya kazi na watu wenye mitazamo tofauti,"alisema," Prof. [158]
tu
Alifafanua kuwa, Waziri Pinda ametengeneza mazingira ya uchafuzi na uchochezi, kutokana na kauli yake hiyo kwani baadhi ya watu wanaweza kuitumia vibaya kwa kumuua mtu kwa sababu ya chuki tu baina yao. [159]
ugani
Halmashauri ya Wilaya Kasulu inakabiliwa na uhaba wa wataalamu ugani hali inayosababisha kushindwa kufikia malengo ya kilimo. [160]
ujanja
Madereva wengi hawana mafunzo sahihi ya kuendesha magari hasa ya abiria na hivyo kuifanya kazi hiyo kwa ujanja ujanja jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya wananchi na mali zao. [161]
ukame
Same ni wilaya zilizokumbwa na hali ya ukame kwa muda mrefu hasa ukanda wa tambarare. [162]
ukoo
Ya nini kumpa matumaini wakati yeye na ukoo wake wote wameshatolewa nje katika dunia ya leo. [163]
ukweli
Hata hivyo, Mhesa anakubaliana na ukweli kwamba zaidi ya asilimia 80 ya walaji nchini hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na haki zao. [164]
ule
Nadhani polisi kupitia kikosi chake cha usalama barabarani tena kwa kumtaja kiongozi wake, James Kombe ingefanya ukaguzi kama ule wa Dar es Salaam katika stendi zote kubwa na ndogo nchini. [165]
ulinzi
Isitoshe alisema aliwataka viongozi wa vijiji kurejesha ulinzi wa jadi, maarufu kama sungusungu ili kukabiliana na wauaji. [166]
umekutana
Umepekuwa umekutana na kitu umekiamini sivyo kwa kiherehere chako cha kusaka mambo. [167]
umma
Hata hivyo hivi sasa vyuo vikuu vya umma vilivyokuwa vimefungwa, vinaendelea kudahili upya, ingawa hatua hiyo imekuwa ikipingwa na wanafunzi. [168]
uongozi
Akizungumza na waandishi wa habari jana Rais wa TFF Leodegar Tenga alisema kuwa ili kufanikisha mikakati hiyo ni lazima kila kiongozi kwa kushirikiana na wadau wa soka kujitolea kwa dhati katika nafasi yake kusaidia ujenzi na misingi ya uongozi wa mpira nchini. [169]
ushauri
WAJUMBE wa kikundi kazi kilichoundwa kwa ajili ya kuchunguza na kutoa ushauri kwa Serikali juu ya kuinusuru Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), kimekabidhi taarifa yake jana kwa Waziri wa Miundombinu Dk Shukuru Kawambwa. [170]
uzazi
Daktari anayehusika na masuala ya uzazi hospitalini hapo, Harold Henry ambaye pia alishiriki katika shughuli hiyo alisema afya ya watoto wote pamoja na ya mama yao zao zinaendelea vizuri. [171]
vema
Kama nimekosea nakubali kukosolewa kwa lengo la kujenga, lakini kama ni vingine basi ni vema tukatumia busara zaidi na kutofautisha soka na mambo ya siasa," alisema Maximo akionyesha kujiamini. [172]
vifo
Mara nyingi hatua kama hizi za ukaguzi zimekuwa zikilipuka kila kunapotokea ajali mbaya na kusababisha vifo. [173]
vigezo
Jijini Dar es Salaam, Benjamain Sawe na Zawadi Msalla wanaripoti kuwa, Mkurugenzi wa Usambazaji wa Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu, Lubambula Machunda amewashauri wanafunzi kufuata utaratibu uliowekwa na bodi ya mikopo nchini, ikiwa ni pamoja na kufuta vigezo sahihi vilivyopangwa katika kufuatilia madai na matatizo mbalimbali yanayoshughulikiwa na bodi hiyo. [174]
viingilio
KLABU ya Yanga imetangaza viingilio vya mchezo wao Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Etoile d'Or Mirontsy ya Comoro utakaocheza Jumamosi kati ya Sh. [175]
vijana
Alisema eneo hilo ni maalumu kwa ajili ya vijana kufanyia michezo mbalimbali, lakini sasa limegeuzwa la kuegesha magari hayo. [176]
vilivyo
Tumeanza kutumia mfumo huo kuhakikisha tunadhibiti vilivyo bidhaa zote zinazoingia nchini na kuziteketeza zile bandia," anasema Mhesa. [177]
vingine
Kuhusu uchaguzi huo, mgombea wa CUF aliishia kupata nafasi ya pili huku chama hicho na vingine vya upinzani walitoa madai mbalimbali kuulalamikia uchaguzi huo, ambao idadi ya watu waliopiga kura ilikuwa chini ya asilimia 45 ya watu waliojiandikisha kupiga kura. [178]
vinne
Meneja Huduma za Jamii wa Zain, Tanzania, Tunu Kavishe alisema awali Tanzania ilikuwa iwakilishwe na Vyuo Vikuu vinne; Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi za Tiba Muhimbili, MUHCS, Hubert Kairuki, St Agustine na Chuo Kikuu cha Mzumbe. [179]
vita
Alisema vita dhidi ya mauaji ya albino imekuwa ikitumika kisiasa zaidi kuliko kitaalamu na kuongeza kuwa, mamlaka husika ziliangalie tatizo hilo kitaalamu badala ya kuliacha likitumika kisiasa. [180]
vyuo
Katika marekebisho hayo bodi hiyo imeongeza makundi yatakayopata mikopo kutoka sita hadi 11, pamoja na kutoa mikopo ya kujiendeleza kwa wahadhiri wa vyuo binafsi sawa na wale wa serikali. [181]
wadau
Prisons inashuka uwanjani keshokutwa kuvaana na Khalij Sert ya Libya katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika huku wadau wengi wakiipa nafasi ndogo ya kushinda kutokana na kufanya vibaya kwenye ligi. [182]
wakuu
Akizungumza jana jijini Mwanza alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kutembelea vyuo 17 na kuzungumza na wanafunzi, viongozi wa serikali zao na wakuu wa vyuo hivyo. [183]
walio
Hata hivyo, pamoja na juhudi kubwa za serikali katika kuhakikisha kuwa Watanzania walio wengi wananufaika kutokana na kubadilishwa huko kwa matumizi ya lugha kuwa katika Kiswahili, bado kuna changamoto kubwa kwa Watanzania katika kusoma na kupitia mabadiliko kama hayo. [184]
walipatwa
Wataalamu wa masuala ya watoto mapacha nchini humo walipatwa na kigugumizi kuelezea nini kilichotokea. [185]
wapo
Hakukuwa na malalamiko yoyote katika kufanikisha kujifungua kwa watoto hawa," anasema Dk Henry na kuongeza kuwa watoto hao walizaliwa wiki nane kabla ya muda wapo katika mashine maalumu. [186]
waweze
Alisema ameyaona makosa yaloyojitokeza na atayafanyia kazi kabla ya mchezo huo wa Jumapili na amewataka watanzania kuwaombea ili waweze kushinda. [187]
wenzao
Meneja Udhamini wa TBL, George Kavishe alisema wataakikisha wanatoa jezi kwa kila mechi watakayocheza Yanga katika mashindano hayo ilikuwapa uhuru wachezaji iwapo kama watakuwa wanataka kubalishana na wachezaji wenzao. [188]
wiki
IKIWA imepita wiki moja, tangu Rais wa Marekani, Barack Obama apishwe , msomi wa Marekani, Prof. [189]
wowote
Madaktari hao waliokuwa wamejiandaa vyema kwa kufanya maandalizi kabambe kabla ili kuondoa utata wowote ambao ungeweza kutokea wakati wa kujifungua huko. [190]
yapo
Anasisitiza kuwa kuna mabadiliko mengi yanayotokea kila siku, hivyo wafanyakazi, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, wanatakiwa kufuatilia kwa umakini na si kuishia kuilalamikia serikali tu kwa kila jambo hata kama mambo mengine yapo ndani ya uwezo wao. [191]
yawe
Lengo langu ni kupunguza na ikiwezekana kuyaondoa kabisa makosa yasiyokuwa ya lazima ili magazeti tunayochapisha yawe ni mfano wa kuigwa katika nchi za jirani na pia nchi nyingine zinazochapisha maandishi kwa Kiswahili. [192]
yetu
Hii ni kwa sababu baadhi ya vipengele vya mkataba huo, vinapingana na vya sheria za nchi yetu," alisema Balozi Seif. [193]
yeyote
Na hii kimsingi ndiyo kazi ya kwanza ambayo mwanasheria yeyote anapoletewa kesi ya jinai huifanya kuhakikisha kwamba ni kweli hilo kosa analokabiliwa nalo mteja wake lipo kwa mujibu wa sheria. [194]
yote
RAIS Jakaya Kikwete amewaagiza viongozi wa Jiji la Dar es Salaam kuweka utaratibu wa kujenga barabara za kupita juu kwenye makutano yote ya barabara za jijini, ili kupunguza msongamano wa magari. [195]
yule
Yoyote yule asitegemee kuwa na upendeleo fulani kutoka katika kikosi changu, Zanzibar waache lawama na moja kwa moja waboreshe ligi yao kwanza. [196]
za
Hali hiyo ilitokea jana bungeni, wakati Pinda akielezea yaliyomfanya atoe kauli hiyo tata kikatiba na misingi ya haki za binadamu. [197]
zake
Alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, bodi hiyo ilikuwa ikitoa mikopo kwa makundi na asilimia zake katika mabano A(100), B(80), C(60), D(40), E(20) na F(0), lakini sasa imeongeza idadi ya makundi hayo hadi kufikia 11, ambayo ni na viwango vyake vya asilimia za mkopo katika mabano A(100), B(90), C(80), D(70), E(60), F(50), G(40), H(30), I(20), J(10) na K(0). [198]
zile
Mathalan, watu wanaobomolewa nyumba zao, wengi wao hujikuta wakikwama kutokana na kutokuzielewa vyema sheria zilizopo, hasa zile za ujenzi wa nyumba katika maeneo ya barabara. [199]
zipo
Kutokana na hali hiyo, ni wazi kwamba bado bidhaa hizo zipo madukani na madhara yake yataendelea kuiangamiza jamii. [200]