Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-29
Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz
- aaah
- Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu, alijisemea Kazim. [1]
- aende
- Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
- afe
- Si bora afe tujue moja. [3]
- aina
- Hata hivyo Kamanda huyo alisema kuwa ndani ya gari hilo ambalolimepasuliwa vioo na namba zake za usajili ni T 324 ADK aina ya Isuzu Journey kulikuwa na wachezaji wa Mtibwa na mshabiki wa mtibwa aitwae Adolf Shaban ambaye alikuwa ameumizwa maeneo ya kichwani. [4]
- ajira
- Tangu 2005 hadi 2008, watu 1,271,923 walipata ajira serikalini na kutoka sekta mbalimbali," alisema na kusisitiza kwamba hayo ni mafanikio makubwa. [5]
- akawa
- Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [6]
- alifika
- Muda mfupi baadaye waziri alifika hapo hospitalini, kwani si mbali sana kutoka kwenye ofisi yake. [7]
- ama
- Sasa lipi jema? ukae utulie ama. [8]
- ambalo
- Kamati ya bunge ya ardhi,Maliasili, Utalii na Mazingira, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Job Ndugai ilipotembelea kijiji hicho ilitangaza mashamba namba 1,2.3 kutolewa katika upanuzi wa ziwa Manyara ambalo linaelekea kukauka. [9]
- ambapo
- Uchaguzi huo ulifanyika Januari 25, mwaka huu ambapo watu waliopiga kura hizo ni 44,855 kati ya 127780 waliojiandikisha. [10]
- ana
- KOCHA wa timu ya Etoil d'Or Mirontsy ya Comoro, Nassurdine Maanrouf amesema ana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi wakati kikosi chake kitakapoivaa Yanga katika mapambano wa kuwania Kombe la Klabu Bingwa Afrika utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. [11]
- anaweza
- Wizara hiyo iliagiza kubandikwe mabango sehemu zote za hospitali kuwa 'Damu hutolewa bure' na yaonyeshe namba za simu ambazo mgonjwa anaweza kupiga na kuarifu uongozi wa hospitali. [12]
- angalia
- Nasikia unamjua, ni huyu hapa angalia vizuri picha, kama unajua anapatikana wapi, nitaagiza hata magari mengine yamsake maeneo hayo, nitaomba hata jamaa yangu mmoja usalama wa taifa mstaafu mwenye uwezo mkubwa katika masuala ya kupeleleza atusaidie kumpata, alisema waziri. [13]
- au
- Dk Slaa aliielezea kauli hiyo kuwa inawezekana alijisahau au hana washauri wazuri au hakua na nia thabiti ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa unaoendelea kwa muda mrefu Zanzibar. [14]
- azidi
- Naomba Mungu azidi kuwajaalia nguvu, maisha marefu na mafanikio kwa mwaka huu mpya. [15]
- bado
- Katika hatua nyingine, wabunge hao wa upinzani walidai kuwa pamoja na umoja uliokuwa umeundwa na vyama vyao kusambaratika, wao bado wataendelea kuwa na mshikamano. [16]
- bali
- Inasema sehemu ya taarifa hiyo kuwa matokeo ya umimi wa baadhi ya mashirika ya kimataifa ndio hayo ya kuyumba kwa masoko ya fedha duniani, tukio ambalo kwa sasa linaathiri sio tu mabenki, bali hata watu wasiokuwa na hatia. [17]
- bara
- RIPOTI ya hivi karibuni ya Benki ya Dunia, imezungumza mengi kuhusu uchumi wa dunia huku ikiitupia macho pia Afrika na kusema kunahitajika jitihada zaidi kurekebisha uchumi wake ambao bado hauvutii, kwa maana kuwa bado wakazi wengi wa bara hilo ni maskini mno. [18]
- baya
- Unapompekuwa bila shaka unatafuta makosa! tuseme ukweli; hilo si jambo baya kufanya kama tayari hisia zako na ishara fulani zimeashiria kuwa huyu mtu lazima anakuwa anakutenda au kama huonyeshwi unapendwa. [19]
- bila
- Liyumba anakabiliwa na mashitaka matatu ya kutumia vibaya madaraka yake, kuidhinisha malipo ya ujenzi wa majengo pacha bila idhini ya bodi ya wakurugenzi wa BoT na kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh 221, 197, 229, 200.95 bilioni. [20]
- binafsi
- Alisema kuwa umefika wakati kwa wamiliki wa magari kutoangalia maslahi yao binafsi, badala yake wazingatie maslahi ya watu wanaowahudumia. [21]
- chakula
- TIMU ya soka ya Khalij Sert ya Libya itakayopambana na Prisons Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, imetaka isiandaliwe chakula na wenyeji wao kwani watakuja wakiwa wamejikamilisha. [22]
- dua
- Kama ilivyo kawaida kwa ndugu jamaa na marafiki wa waliopoteza maisha yao pamoja na uongozi wa CUF kila ifikapo Januari 26 na 27 hukusanyika katika maeneo mbalimbali kuwakumbuka na kuwaombea dua marehemu hao. [23]
- es
- Maranda na Farijala wanadaiwa kuwa kati ya Aprili mosi na Septemba 2 mwaka 2005 mkoa wa Dar es Salaam, waliiba kutoka BoT Sh1,864,949,294.45 baada ya kudanganya kwamba, kampuni ya Kiloloma & Brothers imepewa deni na kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai India. [24]
- ghafla
- Wakishapewa mikopo wale waliosomeshwa shule za wenyenchi kuanzia chekechea, hao ndio walazimishwe kuthibitisha kwamba baba zao wamekuwa maskini ghafla baada ya kulipa miaka yote ile. [25]
- haina
- Kwanza waziri mwenyewe ni albino, kama ataniambia mambo yasiyoeleweka, nitatuma watu tumuue viungo vyake tuvipeleke kwenye biashara, ambayo hadi sasa bado haina mafanikio licha ya kuua yule albino ambaye alikuwa msaidizi wangu wa karibu, alijisemea. [26]
- haja
- Akizungumzia utendaji wa kituo chake katika kuhamasisha uwekezaji alipokutana na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Ole Naiko, anasema kuwa katika zama hizi ambazo ni za ushindani mkubwa wa kibiashara wawekezaji wengine wanapaswa kujitokeza hivyo kuna haja ya kuangalia upya mkataba wa Ticts ili kuimarisha shughuli za bandari. [27]
- hakuna
- Hadi jana hakuna wakili yeyote aliyefika mahakamani hapo kushughulikia dhamana ya washitakiwa hao. [28]
- halafu
- Tunasafirisha zaidi zao hilo katika nchi za Uingereza, kwa mawakala wetu, tunachokifanya ni kuwapa bidhaa zote halafu wao ndiyo wanaziuza katika nchi nyingine," anasema Ali Abeid. [29]
- hao
- Hata hivyo wakili anayewatetea washitakiwa hao, Majura Magafu aliiomba mahakama impe muda ili akazipitie nyaraka zilizotolewa mahakamani hapo jana, kwa kuwa hakuwahi kupewa na upande wa mashitaka. [30]
- hapa
- Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Msemaji wa Kambi ya Upinzani na Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed alisema kuwa wanamtaka Pinda kutoa maelezo ya kuliridhisha bunge juu ya wapi alipopata madaraka ya kwenda kinyume na katiba kwa kuwaagiza wananchi wajichukulie sheria mkononi kuwaua wale wanaowatuhumu kuhusika na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). [31]
- hata
- Sikiliza mwandishi, usifanye kuwa hili wewe hulijui siyo kweli hakuna mtu ambaye hajui ni kwanini watu hawakujitokeza kupiga kura, kwani hata wananchama wenyewe wa CCM siyo wote ambao walikuwa wanamkubali mgombea wao," alisema Andrew Mwakitalu. [32]
- hatari
- Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk Wilbrod Slaa alisema hawakutarajia matamshi ya hatari namna hiyo yangeweza kutamkwa na kiongozi mkubwa serikalini. [33]
- hati
- Pia washitakiwa hao wanatakiwa kutoa nusu ya pesa zilizoibwa kama dhamana ambayo ni zaidi ya Sh50 bilioni au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha pesa. [34]
- hawa
- Kwa kawaida tukiwakamata hawa watu wanaojiunganishia maji kinyamela huwa tunawapelekea Ankara ya miezi 24, na kwahoteli kama hii tunaikadiria inatakiwa ilipe milioni nne kila mwezi" alisema Mndolwa Pia alisema mbali na hoteli hiyo kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha, wataifikisha mahakamani kwa kosa la kuiujumu Dawasco. [35]
- hii
- Alisema hivi sasa wananchi wa vijijini wameamka, kwani wanajua kuchambua mazuri na mabaya na kwamba, safari hii walitaka kumchagua mtu anayefaa na siyo chama kama ilivyokuwa huko nyuma. [36]
- hili
- Alisema kuwa kambi ya upinzani ilikuwa na wasiwasi juu ya ukweli wa habari hiyo iliyotolewa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, lakini jana walipata uthibitisho kutoka ofisi yake kuwa ni ya ukweli. [37]
- hivi
- Waziri Mkuu kuhamasisha wananchi kuchukua sheria mkononi, ni kitendo cha kulaaniwa," alisema Hamadi wakati akifafanua juu ya kauli hiyo aliyoitoa Pinda alipokuwa kwenye ziara Kanda ya Ziwa, hivi karibuni. [38]
- hizi
- Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Rais wa shirikisho la ngumi za kulipwa nchini PST, Emmanuel Mlundwa alisema tayari mabondia wa pande zote mbili wameshathibitisha kushiriki katika mchezo huo. [39]
- hizo
- Fedha hizo ziliingia kutoka BoT kwa njia ya mtandao wa kompyuta na tulipata nakala ya barua iliyotumwa kutoka BoT kwenda kwa washitakiwa ikiwataarifu kwamba, wameingiziwa kiasi hicho cha fedha," alisema Manongi. [40]
- hoteli
- Akizungumza wakati wa zoezi hilo jana, Mkurugenzi Mkuu wa Biashara wa Dawasco, Raymond Mndolwa alisema wanaidai hoteli hiyo zaidi ya Sh96 milioni. [41]
- huenda
- Kuharibu kwa uchumi wa dunia, sio tu kwamba kutapunguza watalii ambao wengi wanatoka nje ya Afrika, pia hata misaada kutoka nchi za nje hasa za Ulaya inayotegemewa kwa ajili ya kuendesha bajeti za ndani kwa serikali nyingi za Afrika huenda ikapungua katika mwaka huu kutoka na uchumi wa nchi hizo kuyumba. [42]
- huko
- Huu ni mchezo wa muda mrefu sana unaofanywa na CCM, na kama hali itaendelea kuwa ya hiyo huko tunakokwenda kutakuwa na matizo makubwa sana," alisema Bashange. [43]
- huku
- Alisema ili kuwe na biashara huria ya kweli ni vyema kuwepo na usawa kati ya mtumiaji na mtoa huduma, kuliko hivi sasa ambapo wamiliki wanajiangalia wenyewe huku watu wanaowahudumia wakiumia. [44]
- huru
- Dk Lunogelo, ambaye ni mchuni na mtaalam wa kilimo anasisitiza kuwa katika wakati huu ambao ulimwengu unapigania biashara huru, ni vema serikali ikaachana na mpango huo wa kuwazuia wakulima kuuza wanakotaka. [45]
- huu
- Pia kambi hiyo ya upinzani iliahidi kuwa itaupinga kwa kauli moja muswada wa wanayamapori, unaotarajia kuwasilishwa kwenye mkutano huu wa 14 wa bunge unaoendelea hapa, kwa maelezo kuwa umezingatia zaidi maslahi ya wageni na kupuuza watanzania. [46]
- huyu
- Kwanza ya yote kuna vitu shostito vya kuangalia; huyu mtu anakuheshimu kiasi gani anakupenda kiasi gani na anakujali kiasi gani. [47]
- idadi
- Yapo mengi yanayozungumzwa kuhusu sababu ya idadi ndogo ya wapigakura kujitokeza kupiga kura, Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kilikuwa na mgombea katika uchaguzi huo kimekaririwa kikieleza kwamba, sababu ya wananchi kushindwa kujitokeza ni kutokana na kukosa elimu ya uraia. [48]
- ikiwa
- Hali hii imesababisha matatizo makubwa ikiwa ni pamoja na wachangia damu bila malipo kushindwa kuendelea kuchangia damu na kufanya mpango kutofikia malengo,"alisema. [49]
- ikiwamo
- Alisema wameshapita maeneo mbalimbali ikiwamo Kilimanjaro na katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambapo wamepata ushirikiano mkubwa, na kwamba watahakikisha wanalikabili tatizo hilo ipasavyo. [50]
- ila
- Mambo yote yalikwenda sawa ila tu kiongozi huyo alisema kuwa timu hiyo itakuwa ikijitegemea kwa chakula ambapo itakuja na wapishi wake watakaokuwa wakiandaa chakula cha timu hiyo mpaka siku ya kuondoka," alisema. [51]
- ile
- Inatabiriwa kuwa shughuli za biashara ulimwenguni katika mwaka huu zitaporomoka kwa wastani wa asilimia mbili, hali ambayo inaikaribia ile iliyowahi kutokea miaka 25 iliyopita. [52]
- iliyopo
- Sheria ya uchaguzi iliyopo inayompya mgombea kutangazwa kuwa mshindi kwa idadi yoyote ya kura atakayopata bado ina kasoro. [53]
- ina
- Alisema wapinzani wanamshauri rais kuwa kauli hiyo ni ya hatari kwa umoja wa kitaifa, kwa sababu ina mbegu ya ubaguzi na inatonesha vidonda vya machungu waliyo nayo wakazi wa Pemba ya kuuliwa kwa wenzao zaidi ya 20 katika utawala wa serikali ya awamu ya tatu. [54]
- ingawa
- Hata hivyo, kwa upande wa migogoro, Profesa Kapuya alisema wizara yake ilipokea migogoro 9,624, na kuitatua 8,345 kati ya hiyo sawa na asilimia 86.7. Hayo ni mafanikio ya kutangaza ingawa hakuitaja. [55]
- japo
- Sio kweli kuwa kumpekuwa ni kumdhibiti na si kweli kuwa wanaume hawapekuliwi, kwa kuwa japo wengine wanadai hawajali lakini najua japo kwa siri au kwa kujua au kutokujua wanapekua. [56]
- jukumu
- Kampuni iliyopewa jukumu la kuyapakua ya Ticts, ndiyo inayotupiwa mzigo wote wa lawama ikidaiwa kwamba imeshindwa kutimiza majukumu yake barabara. [57]
- jumla
- Mapambano hayo yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa na kuwakutanisha jumla ya mabondia nane kutoka visiwani Zanzibar na Dar es salam lengo likiwa ni kuweka rekodi za mabondia hao wa mchezo wa ngumi na mateke nchini. [58]
- juu
- Alisema barua yake aliyoiandika BoT kuhusu mashaka yake juu ya fedha hizo ilijibiwa na Reli Septemba 28, 2005 akielezwa kuwa asiwe na mashaka na fedha hizo kwa kuwa ni malipo halali ambayo yanatokana na majukumu ya kitaifa ya madeni ya nje. [59]
- juzi
- Washitakiwa hao walifikishwa juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh221 bilioni. [60]
- kadhaa
- Hapa nchini tumeshuhudia wake za marais wakiingia katika kashfa kadhaa ama kujihusisha katika biashara wakiwa ikulu au kutumia nafasi ya waume zao kufanya mambo ambayo ni kiyume. [61]
- kamili
- Kamanda huyo alisema kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo iliwapate mashaidi kamili wa tukio hilo. [62]
- kansa
- Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [63]
- karibu
- Lakini wakati akisema hayo, serikali katika kipindi hicho hicho cha miaka mitatu iliyopita iliajiri watu karibu 90 tu. [64]
- kata
- Hata hivyo baadhi ya wananchi wa kata ya Utengule, wilaya ya Mbeya Vijijini walisema hawakwenda kupiga kura kwa sababu hawakumuona mtu ambaye anafaa kuwaongoza. [65]
- kati
- Shahidi huyo alisema kati ya Septemba 2, 2005 na Novemba 8, 2006 washitakiwa walichukua Sh1,150,249,294.45 kutoka katika akaunti hiyo. [66]
- kibao
- Unafikiri wale waliokatika shule za ukata wanaweza kushindana na wale wanaotoa mamilioni kwa ajili ya shule ya wanafunzi wachache na walimu kibao, na kufanya tuisheni juu mpaka wanaweza kufaulu bila hata kuelewa kitu. [67]
- kikao
- KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wlaya ya Kishapu, Elly Mlaki, ameangua kilio ndani ya kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, baada ya kushindwa kujibu swali la mmoja wa madiwani. [68]
- kina
- Hata hivyo mkurugenzi huyo, hakutoa maelezo ya kina kuhusu swali hilo, jambo lililomsukuma Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,kuingilia kati na kutaka ufafanuzi wa kina juu ya swali hilo. [69]
- kisiasa
- Alibainisha kuwa kauli hiyo ni kinyume na ahadi aliyoitoa wakati akihutubia bunge kwa mara ya kwanza kuwa atahakikisha anamaliza mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar. [70]
- kiwango
- Fedha zilizotolewa zinalenga kusaidia Mpango wa Serikali wa Maendeleo ya Elimu (ESDP) katika kuboresha elimu ya msingi na sekondari pamoja na kuongeza nafasi ya elimu kwa masikini na kiwango cha ufundishaji kwa walimu. [71]
- kuanzia
- Mkurugenzi Mtendaji wa Dawaco, Alex Kaaya alisema juzi kwamba, kuanzia Februari mosi, mwaka huu madeni yote ya Dawasco yatakusanywa na kampuni za udalali za Majembe, City Delivery Services na Collection Africa zote za jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kuimarisha utendaji katika ukusanyaji wa madeni. [72]
- kudai
- Silla alisema wameshangazwa na kamati ya bunge iliyowatembelea hivi karibuni baada ya kudai jambo hilo limekwisha tolewa uamuzi bungeni na hivyo limefungwa. [73]
- kuelewa
- Anasema, Wapemba hawajafikia hatua ya kujifunga mabomu na ndiyo maana wanatumia njia za amani na kidiplomasia katika kudai haki zao na kwamba ikishindikana watatumia njia nyengine ili viongozi waweze kuelewa kuwa wapo makini katika jambo hilo. [74]
- kufa
- Mwambieni Rais Kikwete kuwa mauaji sio suluhu la migogoro ya kisiasa na kwamba siku zote anayetetea haki haogopi kufa, bali anayedhulumu ndie anayeogopa kufa, kwa hiyo tutaendelea kudai haki yetu na kamwe hatotufumba midomo kwa maneno wala risasi," anasistiza Duni. [75]
- kufikia
- Alisema ili nauli ishushwe ni lazima mafuta yashuke hadi kufikia Sh1,100, wafanyabiasha washushe bei za vipuli na mataili, kodi zisizo na msingi ziondolewe na kuwekwa uongozi madhubuti katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo. [76]
- kuja
- Hii ni mara yangu ya kwanza kuja Afrika Mashariki lakini hiyo yote hainipi tabu kwavile katika soka unakakiwa kuwa tayari kucheza mahali popote"alisema Maanrouf. [77]
- kukosa
- ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Joachimu Liyumba na Meneja Mradi wa benki hiyo, Deograthias Kweka wameendelea kusota rumande kwa kukosa dhamana. [78]
- kukuza
- Thamani ya fedha ya nchi yoyote ni muhimu sana katika kukuza uchumi na kuleta maisha bora kwa wananchi wake. [79]
- kule
- Ndio ndugu, mimi naitwa Kazim ni mwenye mgodi wa madini ya almasi kule Mwadui, tatizo ni kwamba hali kwa sasa imekuwa mbaya mno, nimechanganyikiwa hapa hata sijui la kufanya, alisema akiomba ushauri. [80]
- kumpa
- Wananchi walio wengi ambao ni wapiga kura wa Chadema walivunjika Moyo baada ya kuona kuwa mtu ambaye walikusudia kumpa kura zao ameenguliwa. [81]
- kumuua
- Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [82]
- kupita
- Hivi sasa tumeanza kuutekeleza mpango huu, tumeanza kupita katika maeneo ya hospitali mbalimbali kuhakikisha hakuna watu wanaofanya biashara hiyo ya damu,"alisema. [83]
- kupitia
- Wakizungumza katika mkutano huo ambao ulishirikisha wananchi 547, wananchi hao walieleza kutokubaliana na maamuzi ya bunge kupitia Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ambayo iliwatembelea hivi karibuni. [84]
- kusaka
- Umepekuwa umekutana na kitu umekiamini sivyo kwa kiherehere chako cha kusaka mambo. [85]
- kuu
- Surunga alisema wanashangazwa na Bunge kutoa maamuzi ya kutoa maeneo yao kwa upanuzi wa hifadhi wakati bado kuna kesi ya msingi mahakama kuu ya ardhi. [86]
- kuua
- Ni suala la kawaida kuua albino na damu zao au viungo vyao tunavitumia kwenye shughuli hizo za uchimbaji madini na uvuvi, watu wengi wanafanya hivyo. [87]
- kuuza
- Hivi karibuni serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mpango wa Taifa wa Damu Salama ilipiga marufuku hospitali au mfanyakazi kuuza damu kwa wagonjwa au ndugu zao. [88]
- kuuzwa
- Ndugai alisema serikali inaendelea na mazungumzo ya kununua shamba jingine lilikuwa linamilikiwa naPrince Benard na kuuzwa kwa mkulima wa Kiasi Ghanji, ili litolewe kwa wananchi wa kijiji cha Moya Mayoka kwa uhifadhi. [89]
- kuwaza
- Kutokana na hali hii serikali za nchi nyingi duniani zitakuwa zikitumia muda mwingi kufikiria na kupanga mipango ya kuboresha hali ya mambo ndani ya nchi zao, badala ya kuwaza kusaidia nchi nyingine. [90]
- la
- Kiongozi wa jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Cypriana William alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa. [91]
- lake
- Serikali ya Ufaransa, kupitia Shirika lake la Misaada ya Maendeleo (AFD), wiki iliyopita ilitoa awamu ya pili ya msaada wake kuchangia bajeti ya elimu kiasi cha Paundi 890,898.82 sawa na Sh1.425 biloni, fedha za Tanzania," ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya balozi Labriolle. [92]
- langu
- Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni, alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [93]
- lao
- KIPA wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kado, Salum Ussi na Uhuru Suleiman wamejeruhiwa baada ya basi lao kushambuliwa kwa mawe na mashabiki wa Yanga baada ya mchezo wa juzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. [94]
- lengo
- Alisema kikosi chake hakitakuwa na mabadiliko makubwa katika maandalizi hayo kwani atatumia mbinu zilezile kwa lengo la kuwaweka kikosi chake katika morali ya kupata ushindi zaidi. [95]
- limekuwa
- TATIZO la msomgomano wa makontena katika Bandari ya Dar es Salaam, limekuwa likipigiwa kelele na wadau mbalimbali. [96]
- lipi
- Wapige kura kwa lipi wakati hawakuridhishwa na sera za vyama vengine?" alihoji Tumbo. [97]
- lori
- Hatua ya Mkurugenzi huyo kuangua kilio, Ilikuja baada ya Diwani wa Magalata, Albert Kapongo, kumuliza swali lililohusu jinsi ofisi yake ilivyotumia Sh 120 milioni, kununulia lori la Idara ya Elimu. [98]
- mabao
- WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Prisons ya Mbeya imeendelea kuwa nyanya baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Simba, mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. [99]
- mabara
- Akizungumza na Mwananchi mjini hapa jana, mratibu wa pambano hilo la kuwania ubingwa wa mabara, unaotambuliwa na shirikisho la masumbwi duniani UBO, Zumo Makame alisema wamepanga kiingilio kuwa Sh3,000 ili kuwawezesha watu wengi kushuhudia mpambano huo. [100]
- madai
- Wakati vyama hivyo vikitoa madai hayo, Chama Cha Mapinduzu (CCM) kimefurahishwa na ushindi huo kikisema ni wa kishindo. [101]
- madini
- Wakati sekta ya kilimo ikionekana kushindwa kuimarisha uchumi wa Mtanzania kutokana na kuwekewa vigingi kuuza nje mazao, licha ya kutopewa misaada mikubwa ya kukiimarisha, sekta nyingine ya madini nayo imekuwa ni kilio kila kukicha. [102]
- mafuta
- Sumatra iliitisha mkutano huo baada ya kupokea mapendekezo kutoka Baraza la Watumiaji wa Bidhaa zinazosimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra-CCC) kutaka nauli hiyo ipungue kwa asilimia 25 kutokana na bei ya mafuta kupungua. [103]
- makini
- Kwa ujumla, tunashangaa hatua iliyochukuliwa na Dawasco kwani tunaamini walikuwa na uwezo wa kufanya kazi hiyo kama wangekuwa makini. [104]
- mapema
- Ilifafanua kwamba awamu ya kwanza ya msaada huo wa Sh 1.458 bilioni ulikabidhiwa kwa serikali ya Tanzania mapema Novemba mwaka uliopita. [105]
- mazoezi
- Cheka alisema ana uhakika wa asilimia 100 ya kushinda mpambano huo kutokana na aina ya mazoezi anayoyapata na kutambua udhaifu wa Matumla. [106]
- mbali
- Wakiongea na mwandishi wa gazeti hili katika maeneo mbali mbali ya kata hiyo, walisema hawakuona sababu ya kwenda kupiga kura wakati mtu waliyekuwa wanaamini anafaa aliondolewa kwenye kinyang`anyiro hicho. [107]
- mbaya
- Sio hivyo tu, hata uvuvi nao unakabiliwa na usimamizi mbaya. [108]
- mbinu
- Hata hivyo, alikataa kuweka wazi mikakati ambayo kambi hiyo ya upinzani itaitumia kufanikisha mpango huo kwa maelezo kwamba, ni sawa na askari wanaoenda vitani kuweka hadharani mbinu zao za kivita. [109]
- mdogo
- Kauli ya Kabwe iliungwa mkono na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, Erasto Tumbo aliyesema kuenguliwa kwa mgombea wa chama hicho na uwezo mdogo wa ushawishi kwa wagombea waliobaki, ndivyo vilivyosababisha wapigakura wengi waususie uchaguzi huo na kwamba, Tume yaTaifa ya Uchaguzi imechangia kwa kiasi kikubwa. [110]
- mfupi
- Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, Maanrouf alisema kuwa uimara wa kikosi chake chenye wachezaji vijana ndiyo siri ya kuibuka na ushindi huo. [111]
- mimi
- Ni kweli ninafanya kazi, lakini si yangu, utajiri wangu umepungua, nilikuwa nataka kununuaq ndege binafsi ya kutembelea, kwa hali ya kipato changu cha sasa, sina uwezo wa kufanya hivyo, mbaya zaidi tayari nilishatamba kwa watu kwamba nitanunua ndege, nisipomnunua wataniona mimi ni maskini alijisemea. [112]
- miti
- Kupungua kwa uzalishaji wa zao hilo kumezifanya nchi za Indonesia na Madagascar kushindwa kutengeneza vitu kama sigara aina ya kretek inayotengenezwa, manukato, viungo vya kupikia pamoja na dawa za miti shamba. [113]
- mke
- Katika mtazamo wa kiume wenyewe wanasema inawezekana kumpenda mke wangu lakini nikamtamani Heriet lakini hili halina maana kuwa ni Heriet nataka kuwa naye, bali mke wangu. [114]
- mno
- Bila shaka wengi wanatambua kwamba sekta isiyo rasmi ina nafasi kubwa mno katika ajira. [115]
- msaidizi
- Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [116]
- mshindi
- UCHAGUZI mdogo jimbo la Mbeya Vijijini umemalizika huku mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Luckson Mwanjali akitangzwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),kuwa mshindi. [117]
- mumewe
- Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [118]
- mzuri
- Henry ni mchezaji mzuri," alisema Maximo. [119]
- na
- Juma Reli, alimweleza asiwe na mashaka na fedha za EPA zilizoingizwa katika akaunti ya washitakiwa kwa kuwa ni malipo halali. [120]
- namba
- Anselem ambaye ni mwenyekiti wa kwanza wa kijiji hicho, kilichoanzishwa mwaka 1972, alisema mashamba namba 1,2 na 3 ambayo yametolewa kwa Mamlaka la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ni mali ya kijiji hicho kwa mujibu wa sheria ya ardhi. [121]
- nao
- Baada ya kuona mawe yanazidi, wachezaji wa Mtibwa waliteremka kwenye basi lao kwa ajili ya kupambana nao lakini walishindwa na kurudi kwenye gari ndipo polisi walitokea na kuanza kupiga mabomu ya machozi kwa ajili ya kuwatawanya watu. [122]
- naomba
- Ndugu mkurugenzi naomba kupata ufafanuzi wa matumizi ya Sh120 milioni zilizotumika kununulia lori la Idara ya Elimu,"alisema. [123]
- nauli
- MJADALA wa kupunguza nauli za mabasi ya abiria kwa asilimia 25 ulioitishwa jana na Mamlaka ya Udhibiti ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, (Sumatra) haukuzaa matunda kutokana Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (Taboa), kupinga pendekezo hilo. [124]
- nchini
- SERIKALI ya Ufaransa imeipatia Tanzania msaada wa Paundi 890,898.82 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini. [125]
- ndani
- Shahidi huyo pia alisema tangu akaunti ya washitakiwa iingiziwe fedha kutoka BoT haijawahi kuingiziwa nyingine kutoka sehemu yoyote ndani na nje ya nchi. [126]
- ndicho
- Mwenyekiti alisema kijiji hicho kilichosajiliwa kwa namba 12813 AR/RV/1670 ndicho kisheria wamiliki halali ya mashamba hayo kutokana na hati hizo hivyo kama Bunge lilikuwa linataka yatolewe kwa hifadhi ya Ziwa manyara wangewashirikisha. [127]
- ndiye
- Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke Emmanuel Kandilahabi alikiri viongozi wa Mtibwa kufika wakiwa na mtuhumiwa Daud Mkunde ambaye ni shabiki wa Yanga wanaodhani kuwa ndiye aliyeharibu gari lao. [128]
- ndoto
- Nchi ambayo imeshindwa kulinda thamani ya fedha yake ni ndoto kuleta maisha bora na hakuna sababu ya kujidanganya kwamba nchi hiyo inapiga hatua katika kukuza uchumi. [129]
- ndugu
- SERIKALI kupitia Mpango wa Kitaifa wa Huduma za Damu Salama (NBTS), imeanza kutekeleza zoezi la usimamizi, kuhakikisha hakuna wafanyakazi au wahusika wengine wanaouza damu kwa wagonjwa au ndugu za wagonjwa. [130]
- ngumi
- BONDIA wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka amesema hana wasiwasi na Rashid matumla na kuwataka mashabiki kuja kuona akitoa kipigo. [131]
- ngumu
- KOCHA Mkuu wa Yanga Dusan Kondic amesema kuwa mechi ya Jumamosi kati yao na timu ya Etoile d'Or Mirontsy ya Commoro katika michuano ya klabu bingwa Afrika ni ngumu kwani mpaka sasa hawafahamu aina ya mchezo wa wapinzani wao. [132]
- nini
- Jamani, serikali kwa kipindi cha miaka mitatu imewaajiri wateule wake 90 tu?, imekuwaje? Kuna nini? Hayo ni baadhi ya maswali ya watu waliosikia taarifa za ajira ya serikali. [133]
- nzuri
- Alisema kuwa watawakikisha katika mechi hiyo timu yake inashinda mabao mengi ilikuweza kujiweka katika nafasi nzuri hasa katika mechi ya marudiano ambayo itachezwa kwao. [134]
- pale
- Mratibu wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padre Vic Missiaen anasema mgogoro huu wa kiuchumi una madhara makubwa kimaadili hasa pale watu wachache ndani ya jamii kuonekana kutowachukulia hatua wanaovuruga harakati za kuwa na uchumi imara. [135]
- pambano
- Mbali na kuwa na pambano hilo pia siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi kati ya Deo Njiku na Hemed Chilambo wakati Hamis Ajali atazipiga na Abdalah Gobeto. [136]
- pekee
- Je, ni busara kutangaza ajira za wafanyakazi wa baa pekee kwenye vyombo vya habari, wakati watalaamu wameachwa mitaani? Bila shaka wizara, imefanya mengi mazuri lakini suala la ajira hata kama ni la kisiasa lingesubiri kutangazwa muda mwingine. [137]
- pia
- Shahidi huyo alisema kuwa pia aliandika barua kwa washitakiwa, Septemba 19, 2005 akitaka wamueleza kuhusu fedha hizo zina madhumuni gani, mwenye nazo ni nani na watakuwa wanazichukua kwa utaratibu gani. [138]
- picha
- Ikabidi kwa kumtia moyo, ikabidi aende kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia utafiti huo na kufanikiwa kupata picha yake. [139]
- pili
- Alisema washitakiwa walimjibu, Septemba 26, 2005 katika barua iliyoandikwa na mshitakiwa wa pili, Rajabu Maranda kwamba, fedha hizo zimetokana na kulipwa kwa deni waliloomba kwa niaba ya kampuni ya BC Cars Exports Ltd ya Mumbai India. [140]
- pole
- Anawapa pole wafiwa wote waliomtarajia lakini anawaambia kwamba upande wa Bi Elimu mwenyewe, kweli Mwenyezi Mungu amemrehemu maana maumivu yake yalikuwa makali sana na alikuwa anadhoofika siku hadi siku licha ya madaktari wa uongo na kweli waliokuwa wanadai kumtibu. [141]
- saa
- Masharti mengine ya dhamana ni kuwasilisha hati zao za kusafiria, kutosafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kuwa na kibali cha mahakama na kuripoti ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kila Ijumaa saa 2:00 asubuhi. [142]
- sana
- Suala hilo tulilitolea taarifa tangu mwanzo kwa tume ya uchaguzi na walitangaziwa kuwa waache mchezo huo, lakini kwa kweli limeathiri sana uchaguzi na kuwanyima wananchi wengi haki ya kupiga. [143]
- sauti
- Kufuatia kubanwa kwa maswali hayo, mkurugenzi huyo aliaanza taratibu kutoa kwikwi na baadaye kuangua kilio hadharani kwa sauti kubwa na kuwafanya madiwani kushikwa na butwaa. [144]
- sawa
- Alisema pia kati ya Oktoba 18 na 24, 2005 washitakiwa walituma pesa nje ya nchi Paundi 350,000 sawa na Tsh 714,700,000 kwenda kampuni ya BC Cars Exports Ltd ya Mumbai India. [145]
- sherehe
- Mfano wa hali hii ni uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa Kenya mwaka jana ambako tukio la uvurugaji matokeo ya uchaguzi lilifanyika waziwazi na kulazimika Rais Mwai Kibaki kutangazwa mshindi huku sherehe za kumwapisha zikianza. [146]
- shida
- Umempata? alidakia Kazim, aliyekuwa akizungumza kwa shida. [147]
- shule
- Agizo hilo lilitolewa jana na mkuu huyo wa wilaya , wakati alipokuwa akizungumza na baadhi ya watendaji wa kata hiyo na walimu wakuu wa shule za sekondari za Manispaa hiyo. [148]
- si
- Hata hivyo, Mwambungu aliwataka watendaji hao kuhakikisha wanakusanya fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa kutoka kwa wananchi na kutumika katika malengo yaliyokusudia na si matumizi mengine. [149]
- sio
- Tukumbuke kuwa Yanga imeshawahi kucheza na Wacomoro katika michuano ya kombe la shirikisho Afrika lakini sio hawa tunaocheza nao keshokutwa ndiyo maana nasema mechi ni ngumu sana, aliongeza. [150]
- soko
- Awali akiwasilisha mapendekezo ya kutaka nauli ya ishuke kwa asilimia 25 Mwenyekiti wa (Sumatra- CCC), Giliiard Ngewe aliwakumbusha wadau wa sekta ya usafirishaji mwaka jana walipoomba nauli ipandeshwe walitumia kigezo cha kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na ndani. [151]
- suala
- Katika mkutano wa wakazi hao uliofanyika kijijini hapo juzi chini ya Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Arbina Ammi na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, John Ombay, wakazi hao pia wamekubaliana kulifikisha suala hilo mahakamani endapo hawatapa ufumbuzi wa rais. [152]
- tabia
- Pia kuna uzembe katika kuandaa ankara za madai pamoja na kufuatilia kutokana na kujijengea tabia ya kukaa ofisini kusubiri wateja hata baada ya kupita miezi mitatu. [153]
- tajiri
- Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [154]
- tamaa
- Alisema kuwa kitendo cha mtendaji huyo kisipochukuliwa hatua kitawakatisha tamaa wananchi, na hivyo kutojitokeza tena kuchangia michango ya mingine ya maendeleo katika Manispaa hiyo. [155]
- tani
- Mwaka jana, Kenya iliiomba Tanzania iiuzie tani 160,000 za mahindi, Tanzania ilikataa kutokana na Hifadhi ya Chakula ya Taifa kuwa na uwezo wa kuhifadhi wastani wa tani 150,000 tu. [156]
- tena
- Hali hiyo ilipoendelea mkuu wa mkoa alimwomba mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuahirisha kikao hicho kwa vile haikuwa rahisi tena kuendelea nacho wakati kuna kilio cha mkurugenzi. [157]
- tu
- Mgombea wa CCM Mchungaji Luckson Mwanjali alishinda kwa kupata kura 32867 sawa na asilimia 73, CUF kura 10,578 (asilimia 23) na Chama Cha Sauti ya Umma (SAU) kiliambulia kura 496 tu ya kura zote zilizopigwa. [158]
- tulikuwa
- Jana (juzi) tulikuwa na kikao na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) pamoja na Salhin Sad moja kati ya viongozi wa timu hiyo kutoka Libya aliyetuwa nchini kwa ajili mandalizi ya timu hiyo. [159]
- ukata
- Sasa Mkombozi akifanikiwa kuruka vikwazo vyote hivi, anapelekwa kwenye shule za ukata, shule za kukatisha tamaa moja kwa moja wakati akina Aimbora wanazidi kupeta ndani ya shule za wenyenchi. [160]
- ukawa
- Huenda ukawa umekutana na kitu ambacho kinabaki kuwa hisia zako tu tofauti na mapokezi ya kitu chenyewe. [161]
- ukoo
- Ya nini kumpa matumaini wakati yeye na ukoo wake wote wameshatolewa nje katika dunia ya leo. [162]
- ule
- Padre Missiaen anasema mshikamano wa maana zaidi ni ule unaoweka kipaumbele kuzingatiwa kwa maadili ya uongozi, kuwafanya viongozi wakiwemo wa kidini kutekeleza wajibu wao kwa jamii kwa kujali haki na amani kama msingi wa ujenzi wa uchumi endelevu. [163]
- una
- Lakini wakasisitiza kuwa wataendelea kuwashauri viongozi wao wasawazishe tofauti zao na kuendelea kuwa na ushirikiano, hasa ikizingatiwa kuwa muswada wa vyama vya siasa ambao upo katika hatua za mwisho kabla haujawasilishwa bungeni, una kipengele kinachowezesha vyama kuunda ushirika unaweza kukusanya nguvu za pamoja ili kushinda kwenye chaguzi mbalimbali. [164]
- upya
- Ikiwa fedha ya nchi yoyote inapungua thamani kila kukicha na pasipo kuwa na uwiano wa ongezeko la mishahara, basi uchumi wake umeshindwa na unapaswa kujipanga upya na hata kuleta mjadala wa taifa wa kutafuta mbinu za kuufufua. [165]
- usiku
- Siku moja usiku akiwa nyumbani alitafakari sana hali ngumu ya maisha ambayo angeanza kuishi. [166]
- usoni
- Akizungumza na Mwananchi kutoka Hospitali ya Aga Khan, Kado alisema kuwa vioo vya dirisha vimemkata usoni na vingine machoni hali inayomfanya ashindwe kutazama vizuri. [167]
- utakuwa
- Mpambano mwingine utakuwa kati ya James John atakayepambana na Jackson Jovin huku Shaban Madilu akipambana na Alex Dewa. [168]
- vema
- Kuhusu maandalizi ya Prison, Chambuso alisema kuwa kwa kushirikiana na TFF mambo yaendelea vizuri na wana matumaini ya kufanya vema katika pmbano hilo licha ya kukabiliwa na majeruhi wengi. [169]
- vichwa
- Waishiwa walitingisha vichwa vyao kwa uchungu sana. [170]
- vile
- John Mwang'ombe alieleza kuwa sababu iliyomfanya ashindwe kupiga kura kwa vile hakuona mtu wa kumpigia. [171]
- vipi
- Je, upungufu wa wauguzi katika Hospitali za Mikoa ya Lindi, Mwanza, Mara, Kigoma na Amana utamalizwa vipi? Alihoji daktari mmoja wa hospitali ya Amana ambaye hakutaka kutajwa jina lake. [172]
- visiwa
- Maanrouf ambaye aliwasili na kikosi cha wachezaji 22 alisema kuwa zaidi anatarajia kuwatumia wachezaji wake waliowahi kucheza nje ya visiwa hivyo ikiwemo Madagascar ili kuimaliza Yanga kwakuwa watakuwa na uzoefu wa kutosha. [173]
- vocha
- Lakini pia naamini kwamba Waziri alipata takwimu nyingine nyingi za waajiriwa kutoka kwenye kampuni za simu baada ya kuwaorodhesha watu mbalimbali wanaouza vocha na 'line' katika mitaa mbalimbali nchini. [174]
- vya
- Wapinzani hao hawakuishia hapo, pia wamemgeukia Rais Jakaya Kikwete wakimlaumu kuwa naye anafanya vitendo vya kuvunja umoja wa kitaifa pamoja na kwenda kinyume na mambo ambayo aliliahidi taifa wakati anaingia madarakani. [175]
- vyake
- Kweli wale watu walimuua yule albino na kwenda na viungo vyake kwenye maeneo ya biashara. [176]
- vyumba
- Mwambungu alisema fedha anazodaiwa kutoweka nazo ofisa mtendaji huyo ni za michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya sekondari ya kata ya Mlimani. [177]
- wadau
- Mwenyekiti wa Taboa, Mohamed Abdullah alisema hakuna sababu kwa wadau hao kuomba nauli ishuke kabla ya kufanyika utafiti wa kutosha juu ya gharama zinazotumika kuendeshea vyombo vya usafiri. [178]
- wala
- Naye Maria Ngogo alipohojiwa ni kwanini hakujitokeza kupiga kura wakati kulikuwa na mgombea ambaye ni mwanamke na angeweza kumuunga mkono kwa kumpigia kura alisema kuwa anachoangalia ni mtu anayefaa kuwaletea maendeleo siyo rangi ya mtu, sura wala jinsi. [179]
- wanafanya
- Na kwa nini wanafanya vizuri. [180]
- wangu
- Sina cha kuzungumza badala ya kufurahishwa na matokeo ya uchaguzi hivyo na kuwashukuru wananchi wa Mbeya Vijijini kwa kumchagua mgombea wangu,"alisema Makamba. [181]
- wao
- Katika barua hiyo, Maranda pia alieleza kuwa wao wana biashara mpya ya ukusanyaji madeni na kwamba, wana kibali maalum cha kutumia sehemu ya fedha ambazo zimelipwa BoT na wanalipwa kamisheni katika fedha hizo," alisema Manongi. [182]
- wapo
- Alisema wapo wachezaji wengi wenye vipaji na wanaoweza kwenda kuchezea timu za kimataifa na endapo watapata nafasi hiyo ni bora wakaitumia ipasavyo kwa maendeleo yao binafsi na ya Taifa kwa ujumla. [183]
- waume
- Badala ya kumsaidia Rais kuwatumikia wananchi, wanadhani nafasi ambayo wanayo waume zao ya kuiongoza nchi ni kwa ajili ya kujinufaisha wao na ndugu zao. [184]
- wawili
- Masharti ya dhamana kwa washitakiwa hao ni wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali na barua zao za utambulisho zitoke kwa waajiri wao. [185]
- wazee
- Katika mkutano huo wazee hao waliunda kamati ya wazee kwenda jijini Dar es Salaam kuonana na rais kumuomba asiridhie upanuzi wa hifadhi hiyo. [186]
- wetu
- Makala haya ya Mwandishi wetu DISMAS LYASSA inataja sababu za hali hiyo na nini cha kufanya ili kuwa na maendeleo. [187]
- wote
- SIKU moja baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza matokeo yanayoonyesha asilimia 65 ya wapigakura wote kutojitokeza, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejigamba kuwa asilimia hiyo ni watu waliotaka kukipigia kura chama hicho. [188]
- wowote
- Henry ambaye aliondoka juzi kwenda Norway katika majaribio, ataungana na mshambuliaji wa Simba, Emeh Izechukwu ambaye anatarajiwa kuondoka wakati wowote. [189]
- yake
- Akihojiwa na wakili wa serikali, Boniface Stanslaus, Manongi alisema aliamua kuandika barua katika Kurugenzi ya Usimamizi wa Mabenki BoT kuelezea mashaka yake kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kuingizwa haraka katika akaunti ya washitakiwa. [190]
- yako
- KIPIMO kimoja muhimu katika kujua ubora na mwelekeo wa uchumi wa nchi yako ni thamani ya fedha. [191]
- yalikuwa
- Aidha Lipumba anasema, anasikitika kuona mambo ambayo yalikuwa yanadaiwa na waandamanaji hao na kupoteza maisha yao hadi leo hayajatimizwa na serikali ya Tanzania. [192]
- yao
- Alisema baada ya kupata majibu hayo alimwandikia barua mkuu wake wa kazi kumjulisha kwamba, washitakiwa wanaweza kuendelea na shughuli za akaunti yao. [193]
- yetu
- Tumeshtushwa na hili kwani ni kinyume kabisa na misingi ya katiba yetu. [194]
- yeye
- Katika dakika ya 23, Oswald Morris alikosa bao akiwa yeye na kipa, Deo Minish 'Dida' kabla ya Jabir Aziz kumjaribu kipa wa Prisons Nelson Kimath aliyelitema shuti lakini Emeh Izuchukwu alizubaa na mabeki wakaokoa. [195]
- yuko
- Bwana Jamhuri Mwananchi anafurahi kutangaza kwamba Bi Elimu Mkombozi hajafa bali yuko mahututi. [196]
- yule
- Kumbe yule jamaa wa pembeni alikuwa ametumwa. [197]
- zangu
- Sikiliza Kazim, usinitukane tafadhari, mimi ni mtu mwenye heshima zangu, nakusaidia tu, usiniletee shida, kama vipi rudi kule India tuone kama utapona, kosa langu ni nini? alijibu waziri kwa sauti ya hasira. [198]
- ziwa
- WANANCHI wa kijiji cha Moya Mayoka kilichoko wilayani Babati, wamepanga kumuona Rais Jakaya Kikwete, kupinga uamuzi bunge wa kuchukua mashamba yao ili kupanua hifadhi ya ziwa Manyara. [199]
- zote
- Wakizungumzia juu ya kauli iliyodaiwa kutolewa na Rais Kikwete wakati akiwa kwenye ziara kisiwani Pemba, kwamba siku zote wanachagua chama kisichokuwa na serikali na hivyo itawachukua miaka mingi, hadi wao kuwa na serikali; walisema inavunja umoja wa kitaifa. [200]