Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-21
Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz
- aaah
- Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu, alijisemea Kazim. [1]
- aende
- Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
- aina
- Alisema kama muswada huo utapitishwa na bunge, wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kupitia mamlaka zao za vijiji watakazotakiwa kuziunda watakuwa na uwezo wa kutoa vibali vya wawindaji wa kigeni na wandani kulingana na aina ya wanyama wanaopatikana. [3]
- akawa
- Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [4]
- alifoka
- Sasa huo si ujinga, picha ndio nini? Picha ndio dawa, alifoka Kazim hali iliyomfanya waziri aendelee kufadhaika na kumueleza kuwa watakachokifanya ni kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari. [5]
- ama
- Kapteni Chiligati alisema hayo alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu na kusema vyuo vikuu vimejengwa bila kujali hali ya mtu na tofauti ya kabila, dini ama siasa. [6]
- amani
- Simwale alisema kuwa serikali ya Tanzania inajenga umoja, utulivu na amani na kwamba inalenga kuipa jamii maendeleo kwa kuboresha huduma muhimu badala ya kuanzisha vurugu kwa kualika 'mabaunza' kwenye kampeni. [7]
- ana
- Nilipokuwa darasani nafundisha niligundua kuwa Irene amepooza sana wakati siyo kawaida yake, nikaamua kumuita aniletee daftari lake nilisahihishe na hapo ndipo nilipogundua kuwa ana tatizo, alisema mwalimu Kaulule. [8]
- au
- Lengo ni kulinda na kutetea maslahi ya wanafunzi hivyo hatuna nia ya ugomvi na serikali au polisi tunajua watakufa wengi lakini haki itendeke tu, alisema. [9]
- baina
- Unapotoa nafasi ya kusikiliza na ukajaribu kuelewa unatoa upenyo wa maelewano baina yenu. [10]
- bali
- Taarifa za kampuni hatuziweki tu kwenye faili, bali zinaweza kupatikana pia kwenye daftari la registrar (msajili)," alifafanua Mahingila kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo). [11]
- bila
- Munishi Deogratius, mbunge wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Daruso) ambayo imetangazwa kuvunjwa na uongozi wa chuo, alisema maandamano hayo yana lengo la kupinga sera ya uchangiaji wa elimu ya juu, kuhitaji wanafunzi wote warudishwe vyuoni bila masharti yoyote. [12]
- binadamu
- Sasa, salaam ni salaam tu lakini bado ni mwanzo wa kumbagua binadamu mwenzio. [13]
- bwana
- Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na bwana mmoja aitwaye John Gottman unasema: namna vile watu wanavyogombana unaweza kujua ni kiasi gani watu wanapendana halikadhalika utaweza kujua ni maamuzi yatokanayo. [14]
- cha
- Mtu asipotoa kitambulisho cha kupigia kura, hauziwi mbolea. [15]
- chake
- Hata hivyo, katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM- Itikadi na Uenezi,- John Chiligati alikanusha habari hizo, akisema kwamba chama chake hakihusiki na wala hakina uhusiano na kampuni hiyo. [16]
- chongo
- Kweli ushabiki ni chongo. [17]
- chuoni
- Waliiambia Mwananchi kwa nyakati tofauti kuwa masharti yaliyowekwa ili kuweza kurejea chuoni, likiwemo la kumaliza kwanza kulipa ada, ni magumu. [18]
- dhana
- Epuka dhana na kusikiliza maneno ya watu. [19]
- dhidi
- KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoani Arusha, imependekeza zichukuliwe hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi waandamizi wa chama hicho wilaya ya Arusha kwa kumwalika Mwenyekiti Taifa, Rais Jakaya Kikwete, katika hafla ya kugawa pikipiki zilizo kuwa na utata. [20]
- duni
- Mama huyo ambaye ni mbunifu wa mitindo aliyedumu katika fani hiyo kwa muda mrefu zaidi, anasema elimu duni na kutoelewa umuhimu wa mitindo nchini ndiyo tatizo kubwa, kwani jamii ya kitanzania haina uelewa kabisa. [21]
- es
- Mwenyekiti wa TSNP, Mulokozi Elgius aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa maandamano hayo, ambayo yamepangwa kuanzia mkoani Dar es Salaam, yatashirikisha wadau wa elimu nchini wakiwemo wazazi wa wanafunzi hao pamoja na wanafunzi wa wote wa elimu ya juu na wale wa shule za sekondari. [22]
- eti
- Hata wale waliotishia kuwashitaki viongozi wa CHADEMA eti kwa kuwadhalilisha sasa wamebaki vichwa chini. [23]
- faida
- Kabla sijaeleza sababu ambazo naona zinasababisha kushuka kwa e-government nchini, labda nitaje faida za mpango huu. [24]
- fani
- Asia Idarous ambaye ni mkongwe katika fani ya ubunifu wa mitindo hapa nchini, anasema hiyo fani inayoweza kutumika kama shughuli ya kujikwamua kiuchumi, ikiwa muhusika atakuwa makini katika kufanya kazi zake. [25]
- hajui
- Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [26]
- hao
- Washitakiwa hao wa ni wafanyakazi watatu wa BoT, Imani Mwaposya, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha madeni ya biashara, Esther Komu (kaimu makamu mkurugenzi wa Idara ya Madeni) na Bosco Kimela (kaimu katibu wa BoT). [27]
- hapa
- Mimi ninadaiwa Sh50,000 yamatibabu na jina halijatoka na mimi sijui kama watanifukuza shule kwa ajili ya kiasi hicho cha pesa kwani mfukoni nimesaliwa na Sh20,000 ndiyo zinazoniwezesha kuishi mjini hapa, alisema mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa tatu ambaye akutaka jina lake liandikwe na ambaye anatokea Kigoma. [28]
- hapo
- Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali waliokuwepo mahakamani hapo tangu kesi hiyo ilipoanza asubuhi, walijikuta wakizuiwa kuripoti kesi hiyo kabla Noni kuanza kutoa ushahidi wakati hakimu mkuu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Addy Lyamuya alipotangaza amri hiyo. [29]
- hasa
- Mushenyera pia alililaumu Jeshi la Polisi kwa kuwatishia wananchi wa Mbeya Vijijini hasa pale inapobainika kuwa CCM haina wafuasi. [30]
- hata
- Sisi kama chama tunahakikisha kuwa uchaguzi huu ni wa haki na wananchi ni haki yao kuchagua kiongozi wanayemuhitaji katika kuleta maendeleo katika kata na vijiji na kwamba chama hata siku moja hakitadiriki kuanzisha vurugu za kisiasa. [31]
- hawa
- Nashangaa hawa watu walioandika hivi bila kuja kuniona. [32]
- hawajui
- Wanashndwa kuwathamini waandishi wa habari, hawajui kuwa vyombo vya habari ni mhimili wa nne wa dola?alisema Mrema. [33]
- hawana
- Hakimu Lyamuya alisema waandishi hawawezi kuripoti kesi hiyo kwa kuwa hawana kibali cha kuandika mahakamani. [34]
- hayo
- Akijibu tuhuma hizo, msimamizi wa uchaguzi mkoa wa Mbeya, Juliana Malange alisema kuwa ameyapata malalamiko hayo na anayafanyia kazi. [35]
- hili
- Akizungumza na gazeti hili katika hospitali ya Mwananyala ambako alipelekwa na walimu wake Dafrosa Bachuta na Bether Palangyo ili kupatiwa matibabu, mtoto Irene alisema kuwa mama yake amekuwa akimpiga kwa fimbo na rungu bila sababu hali ambayo imemfanya kumchukia zaidi mama huyo. [36]
- hivi
- Waandishi wa habari wamekuwa wakifuatilia mintaarafu ya kampuni hiyo kwenye ofisi za Brela bila ya mafanikio na hivi karibuni kuliibuka habari kuwa faili la kampuni hiyo limetoweka Brela, hali iliyozua wasiwasi kuwa huenda sakata la Kagoda litazimwa. [37]
- hizi
- Lakini pamoja na hayo, serikali imefanya jitihada kuhakikisha kwamba huduma hizi zinakuwa juu lakini baadhi ya watendaji wake wanazembea. [38]
- hizo
- Hadi juzi kadi hizo zilikuwa hazijarudishwa, na huenda wasipige kura, alisema Mziray. [39]
- hujui
- Kwa kuwa hujui aliyekuletea ana nia gani na mumeo. [40]
- huko
- Wananchi huko vijijini wanatafuta mahali pa kupeleka kero zao, lakini kwa kuwa Wapinzani hawataki kwenda vijijini, wananchi wanakosa vyama mbadala. [41]
- huku
- Kesi hiyo ilianza kuunguruma asubuhi huku Lyamuya akiwa anasaidiana na Hakimu Ignas Kitusi (Katibu wa Jaji Mkuu) na John Utamwa (Naibu Msajili wa Mahakama Kuu). [42]
- huna
- Ama unaota unahisi unakusaliti na huna uhakika, na huenda hujamuuliza. [43]
- huo
- WAKATI zoezi la kudahili wanafunzi likiwa linaendelea katika vyuo vya umma nchini, hali imebadilika baada ya mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) kutangaza maandamano nchi nzima yanayolenga kupinga udahili huo na yaliyopangwa kufanyika Jumamosi. [44]
- husika
- Uchaguzi kama uchaguzi unalenga katika kanuni sera na kuzingatia kanuni za chama husika za kuwahamasisha wananchi kuchagua kiongozi wanayemuhitaji sasa CUF kuleta mabaunsa mia moja wanamahanisha nini hao CUF kama ushindi kwa CCM upo na si kwamba ugonvi wa vijembe na kutumia nguvu utaleta maendeleo na ushindi kwa vyama pinzani,"alisema Simwali. [45]
- huu
- Uchaguzi wa Mbeya Vijijini unafanyika tarehe 25 mwezi huu baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Richard Nyaulawa kufariki dunia mwishoni mwa mwaka jana. [46]
- huwa
- Pia huwa nauza baadhi ya michoro yangu kwa wamiliki wa viwanda vya nguo hapa nchini na nje, hasa Dubai na China. [47]
- huyo
- Mama huyo ambaye ni maarufu kwa jina la Mama Rahimu alikuwa akimtendea vitendo hivyo vya kinyama Irene Kasanga (7), kwa madai kuwa ni kikojozi. [48]
- huyu
- Hivi sasa mama huyu ameolewa na ana watoto wanne, watatu wakike na wa kiume mmoja. [49]
- idadi
- Matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka jana yametoa picha halisi ya mwelekeo wa elimu nchini, kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kufeli ikilinganishwa na miaka iliyotangulia. [50]
- ikawa
- Na inawezekana ikawa hujui nini kamwambia mumeo kuhusu wewe. [51]
- ikiwa
- Mwenyekiti huyo aliyasema hayo juzi wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Kigogo jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya kampeni za oparesheni sangara ambayo imepangwa kufanyika nchi nzima. [52]
- ila
- Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mpaka sasa hakuna dawa zinazotibu ukimwi ila zilizopo ni za kupunguza makali ya ugonjwa huo ambao ni tishio la nguvu kazi duniani hasa kwa nchi zinazoendelea. [53]
- ile
- Kuna baadhi ya dawa alizopewa zilimpa mafanikio kidogo, akawa anaweza kutembea tofauti na ilivyokuwa siku ile usiku. [54]
- ili
- Alisema wamelitaarifu Jeshi la Polisi ili wapatiwe ulinzi na si kwamba wameomba kibali cha maandamano, hivyo akasema wana imani wanafunzi wote wataunga mkono maandamano hayo. [55]
- imeshuka
- UTAFITI uliofanywa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa (UN) kuhusiana na masuala ya e-government na ripoti yake kutolewa mwaka jana, Tanzania imeshuka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwaka 2005, ripoti hiyo ilipotolewa mara ya mwisho. [56]
- internet
- Kuna baadhi ya wasomaji wataanza kujiuliza e-government ni nini? Hizi ni huduma ambazo zinatolewa na serikali kwa wananchi wake kwa njia ya kompyuta ambayo imeunganishwa katika mtandao wa internet. [57]
- ipo
- Sasa ukikuta timu ambazo saikolojia yao ipo katika hali nzuri hutumia nafasi hiyo kujipanga na hatimaye kupata ushindi kirahisi"anasema Maximo. [58]
- juu
- Hatua hiyo ilitokana na Utamwa kuwasilisha hoja kwa upande wa mashitaka akitaka ufafanue juu ya shitaka la 5 ambalo upande wa mashitaka ulisema kuwa ni mbadala wa shitaka la 3 kwa washitakiwa wa pili, tatu na nne. [59]
- kabisa
- Ni matokeo inabidi tuyakubali kwani ni sehemu ya mchezo lakini mabeki ndio wamesababisha yote haya hawakuwa makini kabisa, walipoteana. [60]
- kadhaa
- Kwa mujibu wa taarifa kadhaa za uchunguzi zilizoripotiwa na vyombo vya habari, mawasiliano yaliyo kwenye nyaraka za usajili wa kampuni hiyo yanaonekana kuwa ni ya kampuni za wafanyabiashara maarufu. [61]
- kali
- KAMATI ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imepitisha mapendekezo ya muswada wa sheria ya wanyamapori itakayowapa wananchi mamlaka ya kutoa vibali vya uwindaji, adhabu kali kwa wawindaji haramu na kuundwa kwa mamlaka mpya itakayosimamia shughuli za uhifadhi wanyamapori. [62]
- kansa
- Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [63]
- kati
- Kwa mujibu wa Ndugai, muswada huo ulitakiwa kuwasilishwa bungeni mwaka jana kati ya mwezi Oktoba na Novemba, lakini walipendekeza ufanyiwe marekebisho kwanza na hivyo ulirudishwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali na hatimaye umefanyiwa marekebisho waliyopendekeza. [64]
- kiasi
- Katika shitaka la nne washitakiwa wote wanadaiwa kuwa Agosti 18 mwaka 2005 waliiba kutoka BoT Sh207,284,391.44. Katika shitaka la sita Mwakosya, Komu na Ndimbo wanadaiwa kuwa wakiwa waajiriwa wa BoT walifanya uzembe uliosababisha benki hiyo kupata hasara ya kiasi hicho cha fedha. [65]
- kibao
- Jamaa kauaaaa, kabakaaaaa, kafisadiiiiiii, kafanya kufuru kibao zinazopingana kabisa na msahafu wa dini yake, lakini badala ya kumkemea twamtetea. [66]
- kidogo
- Hadi awamu ya kwanza ya programu hiyo ilipomalizika mwaka jana, mafanikio yaliyopatikana na kidogo. [67]
- kijiji
- Jana nilikuwa kijiji cha Isupo na mjumbe wa serikali ya kijiji nikiongea na wananchi. [68]
- kikao
- Habari za uhakika toka ndani ya kikao cha awali cha kamati ya siasa ya mkoa zimeeleza kwamba, licha ya viongozi wote wa kamati ya siasa ya chama wilayani Arusha, kuomba radhi kwa maandishi kwa kitendo hicho, kamati ya mkoa imependekeza kuwa wachukuliwe hatua. [69]
- kila
- CAF ilisema kuwa timu mbili kutoka kila kundi ndizo zitakazocheza nusu fainali. [70]
- kile
- Sh5,000 tunayolipa ya kitambulisho niwizi mtupu kwani kitambulisho akijabadilika kitu ukilinganisha na kile cha awali zaidi ya rangi, lakini namba ni ileile, hadi picha alisema mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina moja la Bonge. [71]
- kipindi
- Musingi alisema kuwa anaamini kuwa dawa yake itafanya maajabu na kutangazwa kuwa dawa inayotibu ugonjwa wa ukimwi kwa sababu aliifanyia majaribio kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita na imeonyesha mafanikio. [72]
- kitakuwa
- Naye mkurugenzi wa msanii huyo, Hartmann Mbilinyi anasema Steve anatarajia kutengenezewa kipindi ambacho kitakuwa ni fungakazi kwa sanaa ya vichekesho ambayo inaonekana kupata umaarufu mkubwa hapa nchini. [73]
- kuambiwa
- Ugomvi mwingi wa wanawake wengi unatokana na maneno ya kuambiwa ama kudhania. [74]
- kubwa
- Alisema kuwa imekuwa ni kazi kubwa kutenganisha maeneo ya hifadhi na makazi ya watu katika maeneo hayo, jambo ambalo kwa kiasi fulani limesababisha kuwepo kwa migogoro ya wananchi na serikali. [75]
- kuchokwa
- Afadhali hata mpira maana hatimaye mashabiki wataanza kudai mabadiliko lakini katika siasa, watu watashabikia weeeeeeeeeeeee huku chama fulani kimeshapondwa badala ya kupendwa, kimechekwa na kuchokwa na hata kuchukiwa kutokana na kuchakaa kwake. [76]
- kudai
- Mbowe alirusha kombora hilo na kudai kuwa kama wahusika hao aliowataja wanaubavu basi wampeleke mahakamani na yeye yupo tayari kutoa ushahidi. [77]
- kufa
- Wakati wanaendelea kuangalia ile picha aliingia daktari aliyekuwa akimwangalia Kazim na kumwomba waziri afupishe mazungumzo, badala yake wamsake yule mvumbuzi wa dawa kwani isingepita saa 12 kabla ya Kazim kufa ikiwa hatapata ile dawa. [78]
- kufikia
- UTARATIBU mpya wa kuwarejesha wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwa wamesimamishwa kutokana na mgogoro uliosababishwa na sera ya uchangiaji elimu, haulisaidii taifa kufikia lengo lake la kukuza elimu na kupata wataalamu wa kutosha. [79]
- kuhusu
- Wakiona mwandishi anaandika ukweli kuhusu mambo yao wanamfukuza. [80]
- kujaribu
- Kujua na kujaribu kutumia njia sahihi ya kugombana kutasaidia kutatua migogoro yenu. [81]
- kukutana
- Hivyo walipanga muda wa kukutana. [82]
- kule
- KOCHA Marcio Maximo anasema sasa anaelekeza nguvu zake katika kuiandaa vema Timu ya Taifa, Taifa Stars ili iweze kukabiliana na mikiki mikiki ya Michuano ya Mataifa ya Afrika inayotarajia kupingwa kule Ivory Coast Februari. [83]
- kumbe
- Zaidi ya yote kumbe alikuwa amechukua mkopo benki baada ya biashara zake kumchanganyia, ili kuboresha zaidi, akiamini kuwa kwa namna alivyokuwa akipata fedha angeweza kulipa deni ndani ya muda mfupi. [84]
- kumuua
- Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [85]
- kuna
- Kama kuna mtu anahitaji kuziona anaweza kuzipata, hata kama anataka kupiga 'photokopi' (kudurufu) faili zima, hakuna siri yoyote katika usajili wa kampuni. [86]
- kuona
- Mtu yeote anaweza kuona kumbukumbu zote za mafaili kwa kulipia Sh1,500 tu na kwa waandishi wa habari, hii ni bure, hawatahitaji kulipa chochote," alibainisha Mahingila. [87]
- kushona
- Amefahamisha kuwa amekuwa akichora kila anachobuni na kisha kushona mavazi yanayowezatumika katika shughuli mbalimbali. [88]
- kusoma
- Inashangaza sana kwa uongozi wa chuo unaosimamiwa na wataalamu wa utawala na siasa na wapigania demokrasia nchini, kufanya maamuzi yanayowanyima wanafunzi wengi haki ya kusoma hata ambao hawakuhusika kuandaa mgomo au vurugu, ila tu kwa sababu ya umaskini wao. [89]
- kutibu
- KITUO cha Utafiti wa Magonjwa ya Zinaa na Ukimwi cha Chuo Kikuu cha London (UCL) nchini Uingereza kinafanyia utafiti dawa ya mganga wa jadi wa Kitanzania inayodaiwa kutibu ugonjwa wa ukimwi. [90]
- kuu
- Mziray pia alimtuhumu mjumbe wa kamati kuu ya CCM, John Malcela ameweka kambi kwenye vijiji vya Ilembo, na Isupo akikusanya kadi za wapiga kura. [91]
- kuua
- Ni suala la kawaida kuua albino na damu zao au viungo vyao tunavitumia kwenye shughuli hizo za uchimbaji madini na uvuvi, watu wengi wanafanya hivyo. [92]
- kuzidi
- Lakini mara nyingi kunyamaza ni kuzidi kuzidisha matatizo. [93]
- kwake
- Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jana katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kilumbe Ng'enda alisema kuwa Chadema wamegushi waraka huo na watakifikisha mahakamani. [94]
- kwangu
- Hii ya kwangu naiamini na ndiyo maana nimeamua kushirikiana na taasisi ya kimataifa ili ukweli ufahamike, alijigamba Musingi. [95]
- kweli
- Tumeupitia muswada ambao tilitaka ufanyiwe marekebisho na kwa kweli kwa sasa tumeridhika na tunasubiri kuuwasilisha katika kikao cha bunge kijacho, ili wabunge wachangie na kuamua ama kuupitisha ama kutoupitisha, alisema Ndugai. [96]
- la
- Juzi, ofisa wa kata ya Iyunga Mapinduzi alitangaza punguzo la bei ya mbolea kutoka Sh100,000, hadi Sh45,000. Hii ni rushwa, kwanini punguzo la bei lisubiri wakati wa uchaguzi?"lihoji Mushenyera. [97]
- labda
- Hata siku moja hakuna mtu anayeweza kukata tawi la mti alilokalia labda mwandawazimu alisema. [98]
- langu
- Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni, alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [99]
- lazima
- MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema lazima wafanye vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ambao tayari umeanza baada ya kutofanya vizuri katika mzunguko wa Kwanza. [100]
- leo
- Kwa mujibu wa daktari wa zamu Claudio Marandu, alisema kuwa bado uchunguzi unafanyika na taarifa juu ya uchunguzi huo zitatolewa leo kutokana na mashine ya X-Rays kuwa mbovu. [101]
- maana
- Alisema serikali imeshindwa kutafuta njia mbadala ambayo itasaidia kutatua tatizo hilo ndio maana inatumia nguvu za dola kuwatisha wanafunzi badala ya kuzingatia haki zao. [102]
- mabao
- MABAO mawili yaliyofungwa na Said Dilunga katika kipindi cha pili yameiwezesha Toto African kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Moro United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. [103]
- madai
- Wakati huo huo Patricia Kimelemeta na Ellen Manyangu wanaripoti kuwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeeleza kusikitishwa na kitendo cha serikali kuwafutia udahili wanafunzi 2,000 wa UDSM na kuwakamata wanafunzi wanne kwa madai ya kuandamana kupinga kufutiwa kwa udahili wenzao. [104]
- maelekezo
- Kocha wa Toto African, Mbwana Makata alisema kuwa wachezaji wake walitulia na kupata ushindi baada ya maelekezo. [105]
- mafuta
- Kivipi? Kama unavyojua kusema maneno yanayoudhi ni kama kumtupia kijinga cha moto mtu ambaye tayari ameshaoga mafuta ya taa. [106]
- mara
- Kabla ya amri hiyo, waandishi walikuwemo ndani ya chumba cha mahakama tangu asubuhi wakati kesi hiyo ilipoanza kuunguruma na kuahirishwa mara tatu hadi ilipoanza tena majira ya saa 8:00 mchana. [107]
- mbali
- Naye mwakilishi wa NCCR Mageuzi, Peterson Mushenyera alisema mbali ya kukusanya kadi hizo, viongozi wa CCM pia wanatumia mbolea ya ruzuku kama mtaji wa kujipatia kura. [108]
- mbinu
- Wapinzani mnapaswa mwende kwa wananchi na kubuni mbinu ambazo zitawavutia wananchi ili kujiunga. [109]
- mfumo
- LHRC imeitaka serikali kuangalia upya mfumo mzima wa uchangiaji elimu nchini na hasa kuipitia sera ya uchangiaji ili kupata mwongozo wa kutatua migogoro hiyo. [110]
- michuano
- Wachezaji hao walikuwa Kampala, Uganda wakiitumikia timu yao iliyokuwa ikishiriki michuano ya Chalenji. [111]
- mikakati
- Ukweli ni kwamba hawana mikakati wala ubunifu. [112]
- milioni
- Madega alisema kuwa mpaka kumalizika kwa ukarabati huo klabu hiyo inatarajia kutumia zaidi ya Sh 800 milioni. [113]
- minne
- Ripoti hiyo ya miaka minne iliyopita inaonyesha kuwa Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 127 mwaka 2005 hadi 147 mwaka jana. [114]
- misitu
- Maadhimisho ya siku hiyo yaliyoanza kuadhimishwa mwaka 2001 yamekuja huku kukiwa na taarifa kuwa sekta ya misitu imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upoteaji wa miti. [115]
- miti
- JANUARI Mosi mwaka huu ilikuwa ni siku ya taifa ya kupanda miti. [116]
- mitindo
- FANI ya mitindo imekuwa ikichukuliwa kama burudani, hasa pale wabunifu wanaponadi kazi zao, kitendo ambacho kimekuwa kikichangia kupotosha maana yake halisi. [117]
- mkubwa
- Hata hivyo, wakati kamati ya Siasa ya CCM mkoa ikiwa imependekeza kuswachukuliwa hatua baadhi ya viongozi wa wilaya, tayari kumeibuka mgawanyiko mkubwa ndani ya chama mkoani. [118]
- mno
- Anasema kuwa muda uliopo ni mfupi mno kabla ya kwenda Afrika Magharibi hivyo ni muhimu basi wachezaji waliomo katika kikosi chake wakaishi kulingana na maadali ya mchezaji soka ili kulinda viwango vyao lakini pia kwavile muda mwingi watakuwa katika klabu zao ni muhimu wakafata maelekezo ya walimu wao kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamemsaidia kwa kiasi kikubwa. [119]
- msaidizi
- Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [120]
- muda
- WAKALA wa serikali wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) jana ulifafanua utata wa faili la usajili wa kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, ukisema kuwa halikuwepo kwenye ofisi hizo kwa muda mrefu kutokana na maagizo ya rais. [121]
- mumeo
- Kubeba ulichoambiwa ukakitumia kama fimbo ya kumhukumu mumeo ni makosa makubwa. [122]
- mumewe
- Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [123]
- mweka
- Wiki iliyopita Makamu mwenyekiti wa Simba, Omary Gumbo aliwaambia waandishi wa habari kuwa klabu hiyo imekamilisha mchakato wa kumsaka katibu mkuu na mweka hazina wa kuajiriwa na na kudai kuwa tayari majina yao yameshakabidhiwa kwa TBL kwa ajili ya utekelezaji. [124]
- na
- Viongozi wa upinzani, Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa CUF, Peter Mziray (TPPP Maendeleo), Augustine Lyatonga Mrema (TLP) na Peter Mushenyera waliwaambia waandihi wa habari kuwa viongozi wa CCM wilayani Mbeya Vijijini wanadhibiti mbolea hiyo ya ruzuku na kuiuza kwa manufaa ya chama hicho tawala. [125]
- nami
- Hivyo ndiyo nami nikafikia hatua ya kujiuliza swali hili kuhusiana na nchi yetu kushuka. [126]
- nani
- Mbrazil huyo anasema kuwa soka ya dunia ya sasa imebadilika mpira hauchezwi kwa kuangalia rekodi za nyuma kwamba nani na nani wamefanya nini siku zilizopita kwani kila mmoja hutaka kufikia malengo aliyojiwekea. [127]
- nao
- Tumekuwa tukiwasiliana nao mara kwa mara, mara ya mwisho nilipoongea na Baraza aliniambia wanaisubiri KFF iwapatie tiketi ili waje," alisema Madega. [128]
- naye
- Mshambuliaji wa Polisi, Nicolaus Kapipe alikosa bao la wazi katika dakika ya 28 na Mokil Lambo naye akipaisha mpira akiwa karibu na lango. [129]
- nayo
- Katika taratibu za kawaida za kisheria, mtu anapokamatwa serikali ndio inayotoa ushahidi juu ya tuhuma anazokabiliwa nazo, lakini hivi sasa watuhumiwa wote watatakiwa kuiridhisha mahakama kuwa hawana hataia kwa makosa wanayokabiliwa nayo, alisema. [130]
- ndio
- Alisema migogoro iliyopo sasa inatokana na sera mbovu ya uchangiaji elimu ambayo ndio inayotoa mwongozo kuhusu ulipaji wa ada kwa wanafunzi. [131]
- ndiye
- Kingine kilichopitishwa katika mkutano huo, ni suala la kutoa tarifa za kadi kwa mchezo husika na kusema taarifa zitatumwa CAF na mwamuzi namba nne ndiye atakayehusika kukusanya taarifa za uwanjani. [132]
- ni
- Sasa hii kama siyo hujuma ni' ni'ni? Mbolea ina uhusiano gani na uchaguzi, alihoji Lipumba katika taarifa yake kwa waandishi wa habari. [133]
- nusu
- Katika hatua nyingine, CAF imeanzisha mfumo wa kucheza nusu Fainali kwa michuano ya Shirikisho kama ilivyo kwa mechi za Ligi ya Mabingwa. [134]
- nyingi
- Mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya klabu ya Simba, Hassan Othman Hassanoo alisema tayari wametuma barua kwa wadhamini wao kampuni ya Bia Tanzania, TBL, ili wawasaidie katika mchakato wa uendeshaji wa zoezi hilo ambalo alisema linagharimu fedha nyingi. [135]
- nyuma
- Washindi ambao walikuwa nyuma kwa bao 1-0, walianza kuhesabu bao katika dakika ya 76 baada ya kipa wa Moro United, Saleh Tendega kulitema shuti la Oscar Fanuel na Said Dilunga akauwahi na kuukwamisha mpira wavuni. [136]
- nyumbani
- Siku moja Kazim akiwa amejipumzisha nyumbani, alifuatwa na watu wale waliokuwa wakisimamia biashara zake za uvuvi wa samaki na uchimbaji wa madini. [137]
- nzuri
- Awali, Pius Kisambare aliifungia Moro United bao katika dakika ya nane baada ya kazi nzuri ya Amri kihemba. [138]
- pekee
- Hili si katika serikali pekee bali hata katika makampuni binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali. [139]
- poa
- Na kwa kuwa Makengeza Enterprises haitaki watu wapekue baadaye na kupata funza badala ya mafunzo, viatu maalum vitauzwa kwa bei poa hapohapo kwenye tamasha. [140]
- polisi
- Hapa tumeshatoa taarifa kwa Jeshi la polisi ili lituipe ulinzi. [141]
- ripoti
- Hata hivyo, taarifa na ripoti nyingine zitakazotumwa CAF zitafanywa na chama au shirikisho husika kwa mujibu wa taratibu," ilisema barua hiyo. [142]
- roho
- Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani, alisema Kazim huku akikata roho. [143]
- saa
- Kizaazaa hicho kilitokea jana saa 8:42 mchana wakati shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Peter Noni, ambaye ni mkuu wa mipango kazi wa BOT alipokuwa anataka kuanza kutoa ushahidi. [144]
- sanaa
- Anasema yeye binafsi amepania kuboresha sanaa yake na kuipenyeza katika soko la kimataifa. [145]
- sauti
- Jina laStive Nyerere limetokana na sanaa yake kwa kuwa alianza usanii kwa kuingiza sauti ya Baba wa Taifa ,Mwalimu Julius Nyerere. [146]
- sekta
- SERIKALI imesema kuwa inajivunia maendeleo ya michezo pamoja na miundombinu ya kisasa ya michezo na kutoa mafunzo mbalimbali kuhusu sekta hiyo kwa kipindi cha miaka mitata iliyopita. [147]
- sera
- Uchaguzi kama uchaguzi unalenga katika kanuni, sera na kuzingatia mipango ya chama katika kuwahamasisha wananchi kuchagua kiongozi wanayemuhitaji. [148]
- si
- Tanzania na si kutumia mabavu na kuvuruga uchaguzi. [149]
- sifa
- Kwa hiyo, kwa sifa ya Tanzania ilivyo, tangu eeeeenzi za mwalimu, tutasimama upande gani? Upande wa wanaonyanyaswa. [150]
- sisi
- Hata sisi tulishangaa kumuona pale kwani tunajua anakesi. [151]
- soka
- WAKATI viongozi wa Yanga wanalitupia lawama Shirikisho la Soka la Kenya, KFF kwa kuwachelewesha wachezaji wake, Mike Baraza na George Owino imeelezwa kuwa wachezaji hao wametimkia Misri kucheza soka ya kulipwa. [152]
- soko
- Idarous anapendekeza kuwa vianzishwe vyuo vya ubunifu wa mitindo katika ngazi mbalimbali ili kupata watu wenye ujuzi kamaili ambao wataweza kutengeneza bidhaa zitakazoweza kushindana katika soko la kimataifa. [153]
- tajiri
- Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [154]
- tiketi
- Katibu Mkuu wa Yanga, Lucas Kisasa alisema uongozi wa Yanga umekuwa ukifanya mawasiliano na wachezaji hao na kuelezwa kuwa bado KFF haijatoa tiketi ili wachezaji hao warejee nchini kuitumikia klabu yao. [155]
- toka
- Juhudi za kumpata Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Mark Karunguyeye, ili kuthibitisha tukio hilo ziligonga mwamba baada ya simu ya kutopatikana hewani, ingawa taarifa toka ndani ya jeshi hilo la polisi zilithibitisha kutokea kwa tukio hilo. [156]
- tulikuwa
- Nilifikiri sisi tulikuwa tunanyanyaswa lakini nilichoona huko ni zaidi. [157]
- tuna
- Sisi kama Chama cha serikali ya CCM tuna hakikisha kuwa uchaguzi huu ni wa haki na wananchi ni haki yao kuchagua kiongozi wanayemuhitaji katika kuleta Maendeleo katika kata na vijiji na kwamba chama hata siku moja hakitadiliki kuleta vurugu za kisiasa kwa kutumi vurugu bali kitatumia sera za demokrasi zinazokubalika kwa jamii na kukichagua kuwa ni chama kinachoweza kuleta maendeleo katika kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo la Mbeya vijijini,"alisema. [158]
- ubora
- Kwa mfumo wa sasa, ni rahisi mwalimu au walimu kutomaliza mitaala au kufundisha haraka na kumaliza mapema bila kujali ubora wa elimu na hakuna atakayehoji kwa sababu hawakaguliwi. [159]
- uko
- Mimi sikisemi chama chochote kile maana ushabiki huo uko kote kote, kwa chama cha zama zile hadi chama cha zama hizi. [160]
- uongozi
- Wengi wanalalamika kutorudishiwa kadi zao walizoambiwa wazipeleke kwa uongozi wa kijiji. [161]
- upo
- Kama ushindi kwa CCM upo. [162]
- upungufu
- Pamoja na kuwepo changamoto nyingi zinazosababisha tatizo hilo, upungufu wa wakaguzi wa elimu unachangia kwa kiasi kikubwa kiwango cha elimu kuendelea kushuka. [163]
- upya
- Baada ya kubadilishwa kwa hati ya mashitaka, Wakili wa Serikali Stanslaus aliwasomea upya mashitaka yanayowakabili. [164]
- usiku
- Mapendekezo ya kamati hiyo, ambayo yalijadiliwa juzi usiku na Kamati ya Maadili ya CCM mkoa yalipelekwa jana kwa njia ya Fax kwenye sekretarieti ya chama Taifa. [165]
- viatu
- Kutakuwepo na sanamu kubwa ya Kichaka na wote mtapewa nafasi ya kuitupia viatu kwa nguvu zote. [166]
- vibaya
- Ni dhahiri kuwa itajisikia vibaya hivyo kuboresha na kuongeza juhudi ili ripoti nyingine itakapotolewa iweze kufanya vizuri. [167]
- vijijini
- Mushenyera pia alililaumu jeshi la Polisi kwa kuwatishia wananchi wa Mbeya vijijini hasa pale inapobainika kuwa CCM haina wafuasi. [168]
- vikuu
- Vyuo vikuu vya ni mali ya umma haviusiki na masuala ya kisiasa na kama wanao huo waraka na majina ya wanafunzi waliofukuzwa kutokana na waraka huo watoe na wasiupotoshe umma,"alisema. [169]
- vile
- Naye kocha wa Moro United, Fred Minziro alisema kuwa wachezaji hawakucheza vile alivyowaelekeza. [170]
- vipi
- Mambo vipi mashosto. [171]
- vya
- Watu wanapokwenda kununua mbolea wanaambiwa watoe vitambulisho vya kupigia kura ambavyo husajiliwa na baadaye kurudishwa kabla ya kuuziwa mbolea hiyo. [172]
- vyake
- Kweli wale watu walimuua yule albino na kwenda na viungo vyake kwenye maeneo ya biashara. [173]
- vyote
- Hivi vyote vinapungua kwa kiasi kikubwa chini ya utaratibu huu. [174]
- wake
- Kampuni hiyo, ambayo umiliki wake umekuwa gumzo, inadaiwa kuchota Sh40 bilioni kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), lakini hadi sasa wamiliki wake hawajafikishwa mahakamani kama ilivyo kwa watu wengine 21 waliopandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kuiba jumla ya Sh133 bilioni kwenye akaunti hiyo. [175]
- wako
- Sasa Chadema wameanza Operesheni Sangara, wameshavuruga mikoa ya kanda ya Ziwa na sasa wako jijini Dar es Salaam. [176]
- wala
- Mukandala alikanusha habari kwamba chuo kinaongozwa kisiasa, akisema kuwa huo ni uzushi mtupu na kwamba chuo hakina dini wala chama. [177]
- wangu
- Nimeridhishwa na kiwango cha wachezaji wangu licha ya kwamba hatukufanikiwa kutwaa ubingwa kule Uganda hii inanipa imani ya kwamba ikiwa tutajiandaa vya kutosha basi tuna nafasi ya kufanya vizuri kule Ivory Coast," anasema. [178]
- wao
- CCM wanatumia waandishi wao wa habari wanaoandika matakwa yao. [179]
- wawe
- Na sasa si suala la Waislamu tu, wawe Waislamu wenzetu au Waislamu waleee. [180]
- wenye
- Alisema katika kipindi hicho serikali imewezesha kuanzishwa kwa kituo cha michezo, (Sports Complex) ambayo ni uwanja wa kisasa wenye viwango vya olimpiki. [181]
- wenyewe
- Kwa muda mrefu kumekuwa na hoja ya kuviunganisha vyama hivyo ili kuwa na nguvu ya pamoja ya kukishinda chama tawala CCM. Lakini hoja hii imeshindikana hasa kwa kuwa wapinzani wenyewe hawafanani kimalengo. [182]
- wetu
- Hakuna ukweli wa hilo, sisi tunachokijua ni kwamba hawa ni wachezaji wetu wanashughulikia tiketi zao na tunao kwenye timu yetu, sasa kama watatoroka uwezekano wao wa kucheza soka ni mdogo kama yaliyowakuta akina Kabanda (Laurent) na Mwaipopo (Credo), alisema Kisasa. [183]
- wewe
- Lakini pia ikumbukwe kuwa alichangia pikipiki hizo mwaka 2007 na kama ulikuwepo siku ya tukio, nadhani hata wewe uliona hali ilivyokuwa, alisema kiongozi huyo. [184]
- wiki
- Stars iliyokuwa ikiitwa Kilimanjaro Stars katika michuano ya Kombe la Chalenji, iliwasili Dar es salaam wiki iliyopita ikiwa imeshika nafasi ya tatu. [185]
- yenu
- Inachokupasa ufahamu kuwa kuziba kauli katika suala ambalo limekuudhi hupelekea madhara makubwa mbeleni katika mahusiano yenu na huenda ikaathirika afya yako. [186]
- yetu
- Hivi sasa dawa yetu itakuwa inapakiwa katika makasha maalumu na kuwa katika umbile kama la vidonge maarufu kama rangi mbili hatua itakayoifanya kuwa rahisi kuisafirisha lakini pia kutumika kirahisi tofauti na ilivyokuwa awali. [187]
- yeye
- Mbowe alisema kuwa yeye anauhakika suala la kuwashughulikia mafisadi hapa nchini bado halijatekelezwa ipasavyo kwani anauhakika walengwa bado hawajashughulikiwa. [188]
- yote
- Wakati watuhumiwa wa kesi za EPA wanafikishwa mahakamani mwezi Novemba mwaka jana, Lyamuya alikuwa nje ya nchi kwa matibabu na aliporejea kazini alidaiwa kuhitisha majalada yote ya EPA, lakini alipoulizwa na waandishi wa habari alikana. [189]
- yuko
- Huyu yuko kwenye upande wa madini. [190]
- yule
- Na ni vyema ukaongea naye ili upate ukweli kwa kusema wasiwasi wako, au kile ulichoambiwa kwa kumkutanisha na yule aliyesema itasaidia kuondoa migogoro yenu. [191]
- yupo
- Wakati huohuo Benton Nolo anaripoti kuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amesema yupo tayari kupelekwa mahakamani kutoa ushahidi wa mafisadi. [192]
- za
- Naye Peter Mziray wa PPT Maendeleo alisema kuwa baadhi ya vijiji wamerubuniwa kusalimisha kadi zao za kupigia kura kwa wenyeviti wa vijiji. [193]
- zako
- Zipo hizi hisia wakati mwingine za kumchukia bila kujua sababu, lakini sababu ni kwamba dhana zako ndizo zinakupeleka huko. [194]
- zangu
- Sikiliza Kazim, usinitukane tafadhari, mimi ni mtu mwenye heshima zangu, nakusaidia tu, usiniletee shida, kama vipi rudi kule India tuone kama utapona, kosa langu ni nini? alijibu waziri kwa sauti ya hasira. [195]
- zenye
- Hivyo UN ikaona kuna haja ya kufanya utafiti ili kujua nchi zilizopiga hatua katika matumizi ya kompyuta na internet katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wake na zenye ubora. [196]
- zetu
- Kazi ya ukarabati imekalika kwa kiasi kikubwa niseme ni asilimia 90 mpaka sasa nafikiri ifikapo Machi tutaanza kulitumia rasmi kwa shughuli zetu za klabu"alisema Madega. [197]
- zipo
- Lakini jana, msajili wa makampuni, Esteriano Mahingila aliwaambia waandishi wa habari akisema: "Nataka niwaambie kuwa nyaraka za Kagoda zipo. [198]
- ziwe
- Mganga huyo, Elias Musingi aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa UCL tayari imemtumia vifaa mbalimbali vya kutengeneza dawa aliyoipa jina Legus, ili ziwe katika mfumo wa viwango vinavyokubalika kimataifa. [199]
- zote
- Kuhusu taarifa za kupotea kwa faili la usajili wa Kagoda, Mahingila alisema kuwa kuwa mpangilio wa kuhifadhi kumbukumbu za kampuni katika ofisi ya Brela hufanywa kwa njia ambayo hata kama faili likipotea, taarifa zote zinaweza kupatikana kwenye daftari la msajili bila wasiwasi wowote. [200]