Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-01
Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz
- achukue
- Haisemi nani achukue hatua, wala kwa vipi. [1]
- aina
- FUVU la kichwa cha binadamu limekutwa nyumbani kwa mfanya biashara maarufu wa Maili moja mjini Kibaha, Ally Msuya maarufu kwa jina la Puku likiwa limehifadhiwa kwenye ndoo ndogo aina ya Sadolini iliyokuwa na mafuta ya kupikia yanayojulikana kwa jina la samli. [2]
- ajira
- Profesa Lipumba anasema, serikali iliahidi ajira milioni mbili kwa Watanzania lakini hadi sasa mwaka wa tatu unaondoka huo inaona aibu hata kuzungumzia kipengele hicho. [3]
- ama
- Katibu wa matajiri hao wa mafuta nchini, Bisarara alisema akiba yao inatosha na kwamba hakuna haja ya wananchi ama serikali kuwa na wasiwasi kwamba bidhaa hiyo inaweza kupungua. [4]
- ambaye
- Kaimu kamanda wa polisi, Kilongo tukio hilo lilitokea Desemba 30, 2008 na kumtaja aliyeuawa kuwa ni Mwandu Mayala, 40, mkazi wa kijiji cha Ihalo ambaye anadaiwa kuiba mpunga huo mali ya Zakaria Shija. [5]
- amekuwa
- Kocha huyo aliyeshiriki upangaji wa ratiba hiyo jijini Abidjan, Ivory Coast Alhamisi iliyopita alisema kuwa siku zote amekuwa akiwakumbusha wachezaji wake kucheza kwa kujituma bila ya kuangalia aina ya timu, kitu ambacho anasema wamemwelewa na kuondoa hofu waliyokuwa nayo awali. [6]
- ampe
- CCM kuwa ni kwa nini asichague moja, yaani "ya Kaisari ampe Kaisari, na ya Mungu ampe Mungu" na akimtuhumu kuwa na urafiki wa karibu na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na wenzake. [7]
- ana
- Akijitetea kabla ya hukumu hiyo, Kulyama alidai apunguziwe adhabu kwa sababu ana familia inayomtegemea na wazazi na kwamba tayari ameshapoteza kazi, lakini utetezi wake ulitupiliwa mbali na hakimu huyo. [8]
- asije
- Alisema kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakitangaza kuwa Mwinyi asije kufanya uzinduzi wa kampeni na asipofanya hivyo atachafuliwa. [9]
- au
- Ni ukweli ulio wazi kuwa katika mwaka huu tunaoumaliza sasa baadhi yetu tumekuwa tunafanya vitendo au kutoa kauli ambazo zilikuwa zinalielekeza taifa kubaya," alisema Kikwete. [10]
- bado
- Baada ya kuangalia kumbukumbu za mahakama Hakimu Kabate alimweleza Rama kuwa upelelezi bado haujakamilika na kumtaka aulize swali lingine. [11]
- baina
- Yanga ilifungiwa miaka mitatu pamoja na kutozwa faini baada ya kususa mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa baina yake na Simba, Agosti mwaka jana. [12]
- bali
- Kimsingi siungi mkono si tu kwa sababu Mkapa ni wa kusini bali alivyoliongoza taifa," alisema Athumani akimzungumzia Mkapa ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Lupaso wilayani Masasi. [13]
- bao
- Zambia iliyoingia katika michuano hiyo kama mwalikwa baada ya Eritrea kujitoa, ilianza kupata bao katika dakika ya 25 lililofungwa na Given Singuluma. [14]
- barua
- Katibu wa Ujumbe wa watu walikwenda kuwasilisha barua ya madai hayo kwenye Ofisi za Mwakilishi Mkazai Umoja wa Mataifa, Hamad Ali Mussa alisema wanataka kisiwa hicho kiwe na mamlaka yake kama vilivyo visiwa vinavyounda utawala wa Comoro. [15]
- basi
- Hivyo kama Mzee Mwinyi naye alitenda kosa wakati wa utawala wake, basi atachukuliwa hatua. [16]
- bei
- Basi mheshimiwa hakimu naomba hela nikanunue soda maana kila siku nasikia soda zimepanda bei lakini mimi sijawahi kunywa,"alisema Rama. [17]
- bila
- Nilifurahi kumsikia Rais Kikwete akisema hatamshitaki Mkapa, bila shaka aliona mbali. [18]
- binafsi
- Tena tulikuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza manufaa binafsi ya kisiasa. [19]
- bora
- Lakini, hali ingekuwa bora zaidi kama uchumi wa dunia usingepata misukosuko. [20]
- cha
- Tumeunda kikosi-kazi kinachojumuisha Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa cha kuendesha mapambano haya," alisema Kikwete. [21]
- chake
- Alisema mauaji hayo ni ya mateso na hayana sababu ya kwa kuwa chanzo chake ni cha kipuuzi na kwamba wanaoamini kuwa wakipata viungo vya albino watatajirika, waganga na wauaji serikali itawabana. [22]
- chuo
- Mwezi mmoja baadaye uongozi wa chuo uliwarejesha wanafunzi wote isipokuwa wanafunzi 56 walioesemekana kuwa vinara wa kuwashinikiza wenzao kugoma. [23]
- dana
- Kwa mujibu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo wanafunzi hao walitaka kukabidhiwa rasmi hosteli za chuo hicho zilizopo mtaa wa Chole jijini Dar es Salaam ambazo kwa muda mrefu uongozi wa chuo umekuwa ukiwapiga dana dana na kushindwa kuwakabidhi kama yalivyokuwa makubaliano ya awali. [24]
- dhahabu
- Mramba, waziri mkongwe aliyepata kushika wizara nyeti kwenye serikali za awamu zote nne, na Yona, aliyeshika wizara kwenye serikali za awamu mbili, walipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kutumia vibaya ofisi kwa kuiruhusu kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers) ya Uingereza kuingia mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria. [25]
- dhati
- Na hapa ndipo kunapokuja umuhimu wa kuwa na ushirikiano katika taasisi za siasa, hasa vyama vya upinzani kama kweli vinania ya dhati ya kukiondoa CCM madarakani. [26]
- dola
- Wakati bei ya mafuta ikipanda nchini, hali ni tofauti katika soko la dunia ambako nishati hiyo imeshuka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita baada ya kupanda kwa kasi hadi kufikia dola 140 za Kimarekani kwa pipa mwezi Julai. [27]
- elimu
- Mkurugenzi wa vijana wa Chadema, John Mnyika ndiye aliyekuwa wa kwanza kuusisimua umati huo, baada ya kuwataka wananchi hao kumuuliza mgombea wa ubunge wa CCM, Mchungaji Luckson Mwanjali, kiwango chake cha elimu na kuwa ana uwezo gani wa kuwasaidia. [28]
- Binafsi kwa wale wote walionikumbuka kwa mwaka mzima iwe ni kwa email, barua, kwa kupigia simu, kunitumia meseji ama hata hao walio nibip nikapata hisia kuwa walikuwa wananifikiria na wananikumbuka kwa namna moja ama nyingine imenionyesha wanajali kiasi kama hicho, naomba niseme ahsanteni sana. [29]
- endapo
- Mwenyekiti wa CCM mkoani Mbeya, Nawabu Mulla alitoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari kuwa wabunge wa CCM wagawanyika na kuwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi atakashifiwa endapo atahudhuria uzinduzi huo. [30]
- eneo
- Wakiwa wenye utulivu mkubwa, wakiongozwa na nyimbo za kuhamasishana huku wakilindwa na ulinzi mkali wa polisi katika mkutano huo uliofanyika katika kata ya Utengule Usongwe, wakazi wa eneo hilo walionekana kila wakati wakimshangilia mgombea huyo. [31]
- es
- Wakati fulani wanafunzi wa sekondari waliandamana hadi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, wakirusha maneno makali dhidi ya serikali, wakidiriki kuiita kuwa ni ya kisanii. [32]
- furaha
- Tuna furaha kuona wenzetu Zambia wamekubali mwaliko wetu licha ya kualikwa dakika za mwisho baada ya Eritrea kujitoa," alieleza Musonye. [33]
- fursa
- Mmiliki wa kampuni inayoagiza mafuta ya GBP, Salim Baabde alisema kuwa walifunga ofisi katika kipindi cha sikukuu ili kuwapa wafanyakazi wao fursa ya kusheherekea Krismasi na familia zao. [34]
- fuvu
- Kwa mujibu wa mashuhuda na majirani walisema kuwa fuvu hilo ambalo lilikuwa limehifadhiwa kwenye kisadolini kidogo lilikuwa limehifadhiwa ndani ya mafuta aina ya Samli ili lisiweze kutoa harufu kali ya uozo ndani ya nyumba hiyo kwa kipindi chote ambacho ililengwa kikae humo. [35]
- gani
- Baadhi ya vurugu hizo zilihusishwa na vyama vya kisiasa, ingawa havikuwekwa bayana kama ambavyo Rais Kikwete hakuweka bayana vitendo hivyo vya uchochezi vilifanywa na watu gani. [36]
- gari
- Mtapendekezaje kwamba sisi tupewe tuzo ya tako kwa kuthamini gari kuliko kompyuta. [37]
- gumzo
- Michuano hiyo inafunguliwa rasmi mjini hapa, mahali ambako gumzo katika mitaa na mabasi ya abiria ni kuhusu mashindano hayo ambayo timu ya Tanzania, Kilimanjaro Stars imekuwa gumzo. [38]
- hadhi
- Lakini, hali ya uwanja wa michezo wa Bugembe mjini hapa ambako ufunguzi ulifanyika ilizua malalamiko kutoka kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo kuwa haufai na hauna hadhi inayolingana na michezo yenyewe. [39]
- hakuna
- Mwenyekiti huyo pia alisema kuwa Halmashauri ya Kuu ya CCM mkoani Mbeya inakanusha chama hicho kimegawanyika, akisema kuwa, hakuna wabunge waliogawanyika ndani ya chama hicho. [40]
- hali
- Akizungumzia hali ya uchumi alisema "kwa jumla hali ya uchumi wa nchi yetu kwa mwaka 2008 ilikuwa ya kiwango cha kuridhisha. [41]
- halisi
- Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Haruna Lipumba anasema, ripoti hiyo si sahihi kulingana na hali halisi ya maisha ya Watanzania na kwamba imelenga zaidi katika kupotosha. [42]
- hana
- Semboja Hajji kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam anasema, hana hakika kuwa takwimu hizo ni sahihi, lakini anasema hata kama ni sahihi hakuna tofauti yoyote kwa kuwa hata katika bajeti zilizopita takwimu hizo za kukua kwa uchumi zilitajwa. [43]
- hao
- Alisema wakiwa katika harakati za kusafirisha mali hizo, walizingirwa na wananchi wenye hasira kali na wenzao wawili kupigwa vibaya hadi kufa na baadaye kuchomwa moto, wakati washitakiwa hao wawili waliokolewa na polisi na kufikishwa mahakamani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha. [44]
- hapo
- Kwa hiyo, ofisi inaandaa utaratibu ili wale waheshimiwa wabunge ambao hawajazipata fomu hizo, sasa wazichukue kutoka Ofisi ya Spika mara moja na kuzirejesha hapo haraka inavyowezekana," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya Ofisi ya Bunge. [45]
- haraka
- Taarifa hiyo ilisema kutokana na hali hiyo, ofisi ya Bunge inaandaa utaratibu utakaowezesha wabunge ambao hawajapata fomu hizo kuzipata na kuzirejesha haraka inavyowezekana. [46]
- hasa
- Naomba Watanzania wenzangu wote na hasa wanasiasa wenzangu tuyatambue hayo na tujiepushe nayo. [47]
- hata
- Vitendo hivyo havitavumiliwa hata kidogo. [48]
- hawana
- Semboja anafafanua kuwa, kukua kwa mauzo ya nje nchini Tanzania si jambo la kujisifu kwamba serikali imepiga hatua, kwa sababu bidhaa nyingi zinazouzwa nje ni za kampuni za nje na kwamba Watanzania hawana bidhaa wanazouza nje ya nchi. [49]
- hicho
- Mgombea wa Chadema, Sambwee Shitambala ameenguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho cha kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mbunge wa CCM, Richard Nyaulawa, aliyefariki kwa ugonjwa, lakini amekata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo inatarajiwa kutangaza uamuzi kesho. [50]
- hii
- Leo hii tukisema wangapi wanamuunga mkono Mkapa tutawapata wengi kuliko wachache wanavyofikiri. [51]
- hiki
- Nimewaeleza wachezaji wangu wawe makini kwani hiki ni kipimo kikubwa kwao kwa michuano ijayo iliyo mbele yao. [52]
- hisia
- Mwaka 2008 tumeshuhudia wananchi wakionyesha hisia zao wazi wazi kwa nia mbalimbali, lakini pia tunmeona jinsi serikali ikiwajibika kwa njia moja au nyingine. [53]
- hofu
- Kitendo cha wamiliki wa vituo vya mafuta kinapaswa kukemewa kwani wanawasababishia wananchi hofu ya maisha. [54]
- hoja
- Wilbroad Slaa ameahidi kuwasilisha hoja ya kutaka Mkapa, aliyeongoza nchi kwa vipindi viwili (1995-2005), apandishwe kizimbani kujibu tuhuma za kufanya makosa wakati akiwa Ikulu, huku kiongozi wa upinzani Bungeni, Hamad Rashid, akiahidi kuwasilisha hoja ya kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili aweze kupandishwe kizimbani. [55]
- huo
- Naomba makundi ya kijamii yatambue ukweli huo na waache kuwaendekeza wanasiasa hasidi. [56]
- idadi
- Alifafanua kuwa endapo watakuwa wakisaidiana katika maeneo ambayo chama Fulani kinaonekana kuwa na nguvu na chama hicho kikashinda, idadi ya vitu bungeni itahesabiwa kwa chama kimoja kilichoshinda kiti hicho hata kama nyuma yake kulikuwa na mchango mkubwa wa vyama vingine. [57]
- ikiwa
- Tunaumaliza mwaka nchi ikiwa tulivu. [58]
- ile
- Alisema wamiliki hao wako chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) na ndiyo waliowapa leseni ya kufanya biashara kama ambavyo mamlaka hiyo ilivyotoa leseni kwa waagizaji hao hivyo bado wana mamlaka ya kuwadhibiti kwa namna yoyote ile ili tatizo la aina hiyo isije ikajitokeza tena. [59]
- ili
- Ni matumaini yangu kuwa tutajiepusha na mambo hayo katika mwaka 2009. Nawasihi viongozi wenzangu wa kisiasa na wa kijamii tubadilike, tuweke mbele maslahi ya taifa ili tuiepushe nchi yetu na mabalaa ambayo baadhi ya wenzetu yaliwakuta. [60]
- ilianza
- Awali, Zambia 'Chipolopolo' ilianza vizuri baada ya kuitandika Djibouti mabao 3-0 katika machezo wa ufunguzi uliofanyika katika Uwanja wa Bugembe uliopo, Jinja, kilometa 80 kutoka Kampala. [61]
- imara
- Bwalya, nahodha wa zamani wa Zambia aliyecheza soka ya kulipwa nchini Ubelgiji , Amerika Kusini, alisema kuwa huo utakuwa mtihani mzuri kwa vijana wake ambao watacheza na timu imara kama Tanzania, Uganda, Sudan, Rwanda na Kenya. [62]
- imeanza
- Kwa upande wao baadhi ya majirani walisema wameshitushwa na tukio hilo la kishirikina na kwamba wamesikitishwa kwani kutokana na ukaribu wao na mfanyabiashara huyo imani yao imeanza kuondoka kwa kutoaminiana tena katika shughuli zao za kila siku. [63]
- inadai
- Ripoti hiyo, ambayo imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuchapishwa katika Magazeti ya serikali, inadai kuwa uchumi wa Tanzania ndani ya kipindi cha miaka miatatu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete unapeta kulingana na viashiria kadhaa ambavyo inavitaja. [64]
- iwe
- Hakimu Issa Magori alitoa hukumu hiyo kwa mhasibu huyo msaidizi wa zamani wa Jeshi la Polisi, ili iwe fundisho kwa watu wengine wote wanaofikiria kufanya makosa kama hayo. [65]
- jijini
- WATANI wa jadi, Simba na Yanga wamepangiwa kuchezwa Aprili 19 au 23 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu. [66]
- jipya
- Kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri Baada ya Waziri Mkuu kujiuzulu, Rais Jakaya Kikwete alilazimika kulivunja baraza lake la mawaziri na baada ya kutafakari kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja, hatimaye Rais aliunda Baraza jipya la mawaziri na kumteua Mizengo Peter Pinda kuwa Waziri Mkuu. [67]
- juzi
- Hakimu magori alitoa hukumu hiyo juzi baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani na upande wa mashitaka. [68]
- kadhalika
- Hali kadhalika kwa rais wetu atakapomaliza muda wake, kama alitenda kosa naye atashitakiwa," alisema Mohammed Omari. [69]
- kashfa
- Lowassa hakujiuzulu peke yake, bali aliambatana na mawaziri Nazir Karamagi aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini na Dk Ibrahim Msabaha aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufuatia kuhusishwa kwao katika kashfa ya Richmond. [70]
- kata
- Katika tukio jingine, jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa tukio moja la kuuawa mtu mmoja kwa tuhuma za kuiba gunia mbili za mpunga, katika kijiji cha Ihalo kata ya Kwesela wilaya ya Shinyanga. [71]
- kawaida
- Ni kipindi ambacho kilikuwa na shinikizo, wasiwasi mkubwa nchini, lakini sasa taifa limerudia hali yake kawaida," alisema Rais Kikwete na kuongeza: "Uamuzi ule ulileta mashaka makubwa sana, ulileta mtikisiko nchini. [72]
- kazi
- Akizungumzia mauaji ya albino Rais Kikwete alisema serikali inaendelea na mapambano kuhakikisha inatokomeza mauaji hayo na kwamba imeunda kikosi kazi kuendesha mapambano hayo. [73]
- kiasi
- KOCHA wa Taifa Stars, Marcio Maximo amesema kuwa majina ya nchi na historia zao za nyuma hazimpi taAbu kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya vizuri wakati wa michuano ya Afrika ya wachezaji wa ligi za ndani(CHAN) iliyopangwa kufanyika Februari mwakani nchini Ivory Coast. [74]
- kila
- Tutafanya kila tuwezavyo kurekebisha mambo ili huduma hizo ziboreshwe na kuwafanya watumiaji kufurahi. [75]
- kile
- Tuache vitendo vya kuchochea ghasia kwa kisingizio chochote kile. [76]
- kina
- Hivi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kina nchi nzima kuwatambua wahalifu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria. [77]
- kinga
- Wakati shinikizao la kutaka Mkapa aondolewe kinga na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za makosa anayodaiwa kufanya akiwa Ikulu, wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara na wananchi kuibuka na kumtetea. [78]
- kisha
- Kutokana na matusi hayo ukichanganya na kuwa alikuwa amekolea kinywaji Mrema ambaye alikuwa amepandisha hasira alichomoa kisu alichokuwa nacho kisha akamchoma mkono wa kushoto na damu kuanza kuvuja kwa wingi,"kilisema chanzo kimoja. [79]
- kiti
- Alisema kuwa katika kikao hicho cha halmashauri kilichofanyika jana, wamejipanga kuhakikisha kila mbunge anapangiwa majukumu yake katika kuhakikisha CCM inatetea vizuri kiti hicho kilichoachwa wazi na mbunge wake, Richard Nyaulawa. [80]
- kiwe
- Zaidi ya wananchi 10,000 wa Kisiwa cha Pemba, wameuomba Umoja wa Mataifa (UN) uilazimishe Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibadili muundo wa sasa wa serikali utakaoruhusu visiwa vya Unguja na Pemba, kila kimoja kiwe na serikali yake. [81]
- klabu
- Awali, timu zilipangwa kukutana Aprili 12, imesogezwa mbele kwa ajili ya michuano ya timu ya taifa na klabu bingwa Afrika. [82]
- kocha
- Baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Zambia, Herne Renald alilalamika uwanja wa Bugembe kuwa ni mbovu na mkavu akiulinganisha na ule wa Chuo Kikuu cha Zambia. [83]
- kodi
- Mara baada ya Uchaguzi mkuu wa 1995 waliokuwa mawaziri wa fedha Simon Mbilinyi na Naibu wake Kilontsi Mporogomyi walilazimika kung'oka kwa kilichodaiwa kutoa misamaha ya kodi. [84]
- kombe
- Kaijage alizitaja mechi nyingine ambazo huenda zikabadilishwa kuwa ya Moro United na Kagera Sugar ambayo zinatakiwa kucheza Aprili 20, lakini mabadiliko zaidi itategemea kama Yanga itafanikiwa kuingia raundi ya pili na Prisons kushindwa kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Shirikisho. [85]
- koo
- Na kama desturi ilivyo, mwenye pendekezo lazima alainishe koo za waishiwa, pamoja na kutoa posho la tako (si tuzo la tako). [86]
- kosa
- Hakimu huyo, baada ya kuridhika na ushahidi, alitoa adhabu hiyo ya miaka mitatu jela kwa kila kosa ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya makosa kama hayo. [87]
- kuagiza
- Aliongeza kuwa moja ya sababu zinazoongeza hofu ya kukosekana kwa mafuta ni hatua ya waagizaji na wamiliki wa vituo vya mafuta nchini kuagiza mafuta kidogo kutokana na bei ya bidhaa hiyo kuyumba. [88]
- kucheza
- Alisema kuwa kutokana na wachezaji wengi wa Simba na Yanga kuwa katika timu ya Kilimanjaro Stars ambayo inashiriki michuano ya Chalenji inayoendelea Uganda na kuisha Januari 13,mechi za klabu hizo, zilizotakiwa kucheza Januari 10, sasa zitachezwa Januari 21 kwa Simba kucheza na Villa Squad na Yanga itacheza na Prisons mjini Mbeya. [89]
- kufikishwa
- Tayari watu 91 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani. [90]
- kufoka
- Bila hata kutoa tuzo ya tume kwa ajili yetu, alianza kufoka moja kwa moja. [91]
- kuiunga
- KOCHA Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Marcio Maximo amewataka Watanzania kuiunga mkono timu hiyo ambayo imeondoka jana kwenda Uganda kushiriki michuano ya Chalenji ambayo imeanza kutimua vumbi jana. [92]
- kujiuzulu
- Tukio kubwa kabisa mwaka huu ni lile la kujiuzulu Waziri Mkuu Edward Lowassa. [93]
- kukusanya
- Serikali ilisema imefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh 50 bilioni zilizorejeshwa na watuhumiwa wa ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). [94]
- kuleta
- Alisema kutoka na utendaji aliouita kuwa mahiri wa Mkapa wakati wa uongozi wake, umewafanya Watanzania wengi kumuunga mkono hadi sasa na kwamba kitendo cha kumshitaki ni udhalilishaji ambao unaweza kuleta mgawanyiko katika umoja wa kitaifa uliopo. [95]
- kulipa
- Anakubali kuwa, kiwango cha mauzo ya nje kimeongezeka, lakini anasema, kinatokana na madini hasa dhahabu na bei yake katika soko la dunia jambo ambalo halimfaidishi hata kidogo raia wa kawaida kwa kuwa makampuni yanayozalisha na kuuza madini nchini yanakwepa kulipa kodi. [96]
- kuna
- Mulla alisema kuwa, endapo kuna vyama vya upinzani vitatimiza lengo lao la kumkashifu kiongozi huyo, CCM haitakubali kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa. [97]
- kununua
- Pesa za kununua shangingi moja zinatosha kununua kompyuta kwa watu zaidi ya thelathini pamoja na kulipa gharama zote za mtandao. [98]
- kuomba
- Kabla ya kuomba hela ya soda, Rama aliulalamikia upande wa mashitaka kwa kuchelewa kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo. [99]
- kuuza
- WAAGIZAJI wakubwa wa mafuta nchini wamewakana na wamiliki wa vituo vya kuuza nishati hiyo na kushangazwa na kitendo cha kupandisha bei kiholela wakati wa sikukuu ya Krismas kwa kisingizio cha uadimu wa mafuta baada ya meli kuzuiwa na maharamia wa Kisomali. [100]
- kuwa
- Hii inathibitisha kuwa nchi inaweza kuwa tulivu isipokuwa pale ambapo baadhi yetu tutakapokuwa tumeamua kuwa isiwe hivyo. [101]
- kuzungumza
- Kocha wa Kenya, Francis Kimanzi aligoma kuzungumza mchezo huo, lakini Owino na wenzake walionekana wakimzonga mwamuzi Ally Kalyango wa Uganda. [102]
- kwao
- Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kila timu ikitaka ama kuongeza bao au kusawazisha, lakini milango ilikuwa ni migumu na mabekiwa timu zote walikuwa makini kuondoa hatari zilizoekekezwa kwao. [103]
- kwenu
- Na kwa maana hiyo naomba nichukue fursa hii tena kuwashukuru wasomaji wote wa makala zangu na zaidi niseme ni fahari iliyoje kupata kusikia kutoka kwenu. [104]
- la
- Katika mwaka 2008 uliomalizika jana taifa lilishuhudia matukio mbalimbali- maandamano na migomo ya wafanyakazi, wanafunzi wa vyuo vikuu, wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mapigano ya kikabilila mkoani na fujo katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime mkoani Mara. [105]
- lake
- Hakuna taasisi iliyoonesha ushirikiano katika mambo yake ikashindwa kufikia lengo lake, liwe la kisiasa, kiuchumi, kibiashara na kadhalika. [106]
- leo
- Aidha habari ambazo gazeti hili imezipata kutoka ndani ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinasema rufaa ya Shitambala itatolewa leo saa 4:00 asubuhi. [107]
- licha
- Sisi hatuwezi kuchukua polisi na kwenda kuwakamata licha ya ukweli kuwa ongezeko hilo linawaumiza wananchi. [108]
- ligi
- Alisema ratiba ya raundi ya pili imezingatia mashindano mbalimbali kama klabu bingwa Afrika na shirikisho, michuanio ya fainali ya wachezaji wanaocheza ligi ya ndani ( CHAN). [109]
- madai
- Askari hao walijitambulisha kwa mama huyo na kumtaka awaruhusu kufanya upekuzi ndani ya nyumba kitendo ambacho mama huyo alikipinga vikali kwa madai kuwa mumewe hayupo, lakini Polisi walimuhakikishia usalama wa mali zake hata hivyo mke huyo aligoma kabisa kuwaruhusu kuingia ndani kwa upekuzi. [110]
- madeni
- Ni mwezi huo huo wa Februari, baada ya sakata la Richmond, lilizuka kwa kasi kubwa suala la wale waliochota fedha kutoka akaunti ya madeni ya nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA). [111]
- maendeleo
- Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema jana kuwa katika kikao hicho walijadili mambo muhimu ya maendeleo ya soka la Afrika Mashariki na Kati. [112]
- mafanikio
- Matumani hayo kwa kiasi kikubwa yalichochewa na mafanikio ya kuwa na nguvu ya pamoja iliyochangia kukiondoa madarakani chama cha KANU nchini Kenya na kukiingiza chama kilichokuwa na muunganiko wa vyama mbalimbali vya upinzani nchini humo cha NARC Kenya. [113]
- makini
- Alipowasilisha rufani yake juzi Shitambala alisema kuwa, msimamizi wa uchaguzi hakusoma kwa makini maelezo yake na kuyazingatia kikamilifu kabla ya kufanya maamuzi ya kumuengua. [114]
- makubwa
- Hata hivyo, kocha huyo alisema pamoja na matumaini makubwa aliyonayo kwa kikosi chake, bado Watanzania watatakiwa kuiunga mkono hata pale michuano hiyo itakapoanza akiwataka wale wenye uwezo wa kusafiri kufanya hivyo ili kwenda kuishangilia timu hiyo. [115]
- mama
- Ramadhan na mama yake Hadija Ally wanadaiwa kuwa Aprili 24 mwaka huu walimuua mtoto Salome Yohana (3) ambapo Rama alikamatwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa na kichwa cha mtoto huyo. [116]
- manaibu
- Alipotangaza Baraza jipya iligundulika kuwa Mawaziri tisa na manaibu mawaziri nane, walipoteza nyadhifa zao. [117]
- mara
- Alisema kuwa, mara nyingi kumekuwepo kambi za vijana wa CCM kwa ajili ya kujifunza itikadi za chama hicho na kwamba kambi hiyo ni kwa ajili ya shughuli za vijana. [118]
- masikini
- Lipumba anafafanua kuwa, ripoti hiyo inatofautiana na ripoti ya serikali ya Novemba/Desemba mwaka huu, ambayo yenyewe inaonyesha kuwa watu masikini wameongezeka kutoka 11.7 milioni 2005 hadi 12.7 milioni 2007, na kuongeza kuwa kuna ongezeko la watu milioni moja ambao ni masikini. [119]
- matatizo
- Yapo matatizo ya uendeshaji ambayo yamesababisha huduma zitolewazo ATCL kuwa za kiwango kisichoridhisha, alisema Rais Kikwete. [120]
- mfumuko
- Profesa Lipumba anasema kwamba hali ya mfumuko wa bei inayotangazwa katika ripoti mbalimbali za serikali ni mara mbili zaidi ya hali halisi ya mfumuko wa bei za bidhaa muhimu nchini. [121]
- mgomo
- Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, latangaza kuwasimamisha masomo kwa muda usiojulikana, wanafunzi wa shahada ya kwanza kufuatia mgomo waliouitisha kuishinikiza serikali iwaongezee fedha za mikopo. [122]
- mistari
- Rais Kikwete kupitia hotuba yake hiyo alisema kuwa amedhamiria kumaliza kabisa mpasuko wa kisiasa katika visiwa vya Unguja na Pemba ambapo alisema kuwa unatokana na sababu za kihistoria za wananchi wa kisiwa hicho kusimama kwenye mistari yao ya kihistoria wakati wa mapambano ya kujitawala. [123]
- mke
- POLISI wilayani hapa wanamshikilia mkazi wa kitongoji cha Kobhetimo kijiji cha Nyansurumuti kata ya Kisaka tarafa ya Ngoreme maarufu kwa majina ya Mrema Mantago Nkoba (28) kwa tuhuma za kumchoma kisu na kusababisha kifo cha mdogo wake baada ya kumtuhumu kuwa na uhusiano wa mapenzi na mke wake. [124]
- moja
- Katika tukio jingine, mahakama hiyo imewahukumu watu wawili, Richard Mhoja, 29, mkazi wa Mshikamano na Bundala Mahona, 28, mkazi wa Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga, kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja kwa kosa la kuvunja na kuiba duka vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 607,000 kwenye duka moja. [125]
- mpango
- WAKATI Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) likikamilisha mpango maalum wa kuinua kiwango cha mchezo huo, utekelezaji wake unatarajia kukamilika baada ya miaka nane, imeelezwa. [126]
- mpya
- Kuhusu utekelezaji wa kazi za Bunge kwa mwaka huu mpya wa 2009, Spika Sitta alisema atahakikisha unafuata katiba na sheria. [127]
- mwa
- Miongoni mwa tuhuma za Mkapa, ambaye anasifika kwa kuinua uchumi baada ya kuukuta kwenye hali mbaya, ni kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kwa bei nafuu akitumia kampuni ya Tan Power Resources anayoimulika pamoja na waziri wa zamani wa nishati na madini, Daniel Yona wakati akiwa rais. [128]
- mwisho
- Spika Sitta alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu urejeshwaji wa fomu hizo ambao tarehe yake ya mwisho ilikuwa jana. [129]
- na
- Rais alitoa onyo hilo katika hotuba yake ya salaam za Mwaka Mpya wa 2009 kwa wananchi, aliyoitoa jana kupitia vyombo vya habari, akizungumzia changamoto kadhaa za mwaka 2009 na mikakati ya serikali yake kukabiliana nazo baada ya mikakati ya mwaka 2008 kuathiriwa na kuporomoka kwa uchumi wa nchi tajiri kutokana na kuyumba kwa taasisi za kifedha. [130]
- nani
- Katika soka ya sasa hutakiwi kuangalia unacheza na nani, jambo la msingi ni kuwa tayari wakati wote kukabiliana na yeyote, hivyo kitendo cha kukutana na mwenyeji na hata hizo timu nyingine si tatizo au unaweza kuangalia ni vipi tuliweza kuikabili na kuimudu Cameroon. [131]
- nao
- Kamanda huyo alisema baada ya mzozo wa muda mrefu kama wa dakika 10 hivi mama huyo aliamua kuwaruhusu kufanya upekuzi huku akishirikiana nao kwa kuwafungulia chumba kimoja baada ya kingine na ndipo walipokuta fuvu hilo likiwa limehifadhiwa kwenye ndoo kidogo ikiwa imefunikwa na mafuta mengi ya samli ili isionekana kama kuna kitu kingine zaidi ya samli hiyo. [132]
- naye
- Morumbe Mantago(22) ambaye ni mdogo wake naye mkazi wa kijijini hapo. [133]
- ndio
- Tunaangalia jinsi ya kuiandaa Taifa Stars kwa vile ndio inawakilisha ukanda wetu na kikao kimeshauri kwamba timu hiyo ipatiwe maandalizi ya kutosha ili ituwakilishe sawasawa,îalisema Musonye. [134]
- ndipo
- Alisema mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 1992 hadi 1999 wakati wizi huo ulipogunduliwa na ndipo alipokamatwa na kufikishwa mahakamani. [135]
- ndivyo
- Lakini ndivyo tulivyo. [136]
- ndiyo
- Sitta aliongeza kuwa, wamewasiliana na Ofisi ya Kamishna wa Maadili na kueleza hali hiyo na ndiyo sababu ofisi yake imetoa tamko kuwataka wabunge wasiopata fomu hizo kuzifuata ofisini kwake. [137]
- ngono
- Habari hizo zinadai kuwa hali hiyo iliendelea huku wakiwa wanakunywa ambapo marehemu anadaiwa kumtukana kaka yake akimujumuisha na mke wake Nyabuke Mrema (24) ambaye anahusishwa naye katika masuala ya ngono. [138]
- nia
- Kilichofatia baada ya hapo ndio kinachotia hofu kuwa kama kweli vyama vya upinzani vilikuwa na nia ya dhati ya kuungana na kuwa na nguvu ya pamoja dhidi ya chama tawala, kwani mambo yalianza kwenda mrama wakati wa hekaheka za uchaguzi mdogo katika jimbo la Tarime kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Chacha Wangwe. [139]
- njaa
- Katika tukio jingine, timu ya Kenya, Harambee Stars ikiwa na wachezaji wa Yanga, Joseph Shikokoti, John Baraza juzi ililala njaa Jumatatu ilipokwenda Jinja kwenye hoteli ya Triangle kwa kuwa hakukuwa na taarifa kwa uongozi wa hoteli. [140]
- nje
- Alisema baada ya kukuta fuvu hilo polisi walikitoa kindoo hicho nje ambako muda huo tayari majirani na watu wengine waliosikia uwepo wa tukio hilo waliwa wameshafika kushuhudia upekuzi huo na askari waliwaruhusu kuangalia ndani ya sadolini hiyo ili waweze kuona kilichokuwa kikifanyika ndani ya nyumba hiyo. [141]
- nne
- Hatari yake ni kwamba wanafunzi watakaopitia mazingira hayo watamaliza kidato cha nne bila ya kuwa na elimu inayolingana na kiwango hicho. [142]
- nyeti
- Hali hiyo ilisababisha Rais Kikwete kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali kutokana na kushindwa kudhibiti upotevu wa fedha hizo akiwa kama kiongozi mkuu wa taasisi hiyo nyeti ya umma. [143]
- nzuri
- Jamani Mkapa amelitumikia taifa hili na kuliacha katika hali nzuri. [144]
- ona
- Lakini ona Wakorea sasa na hakuna ambaye atatambia saa za Kikorea. [145]
- ovyo
- Uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 aliyekuwa Waziri wa Biashara na Viwanda Iddi Simba aliondolewa madarakani baada ya kubainika alitoa ovyo vibali vya uagizaji sukari nje ya nchi. [146]
- papo
- Waziri Mkuu aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya papo kwa papo. [147]
- pato
- Baadhi ya viashiria vilivyoainishwa katika ripoti hiyo kuwa vimefanikiwa sana ni pamoja pato la taifa, pato la serikali, mauzo ya nje, pato la mtu mmoja mmoja na miradi mipya iliyofunguliwa na kusajiliwa. [148]
- pia
- Rais pia alisema serikali imekusudia kulifanyia marekebisho shirika hilo katika mwaka 2009, ili liweze kutoa huduma ipasavyo. [149]
- pili
- CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mbeya,kimevionya vyama vya upinzani vyenye lengo la kumchafua rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijijini. [150]
- rasilimali
- Matumizi makubwa ya fedha yanayofanywa na vyama vya siasa wakati wa kampeni za uchaguzi ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma. [151]
- rasmi
- Mgeni rasmi katika mchezo wa Uganda na Zanzibar atakuwa Janet Museveni, mbunge na mke wa Rais Yoweri Museveni. [152]
- ripoti
- Kwa mujibu wa ripoti hiyo serikali inajigamba na kujinasibu kuwa uchumi wa Tanzania unapeta ndani ya kipindi hicho cha miaka mitatu. [153]
- sera
- Sisi Wabunge tupo kwa ajili ya kuifanyia marekebisho katiba, kutunga sera na sheria," alisema Sinani na akaongeza kusema: "(Suala la hoja binafsi) Likiletwa tutalijadili, lakini pamoja na majukumu hayo sidhani kama ni busara kuifanyia marekebisho katiba kila kukicha, hasa pale unapomlenga mtu fulani. [154]
- shida
- Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam juzi, Maximo alisema kuwa umaarufu wa nchi alizopangiwa nazo haumpi shida kwani soka ni mchezo unaochezwa kwa vitendo na si maneno. [155]
- si
- Akizungumzia matokeo ya darasa la saba Kikwete alisema matokeo hayo si ya kuridhisha katika miaka miwili iliyopita na kuwa ameiagiza wizara husika kufanya uchunguzi wa sababu za kushuka kwake, pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, kazi ambayo itasimamiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. [156]
- sisi
- Siku chache kabla ya sikukuu ya Krismasi baadhi ya wafanyabiashara walihofia kutokea kwa uhaba wa mafuta baada ya kuwepo taarifa kwamba nchi jirani hazina mafuta, hivyo wakalazimika kupandisha bei ya bidhaa hiyo kiholela ingawa sisi kwa ujumla wetu kila mmoja ana akiba itakayoweza kutumika kwa siku 25 na kabla hayajamalizika meli za mafuta zitakuwa zimeshawasili nchini," alisema Hirani. [157]
- soko
- Alisema serikali itatumia nguvu nyingi katika kuhami na kukuza uchumi na kwamba,serikali itaendelea kushirikiana na Benki Kuu kuzuia athari za soko la fedha duniani zisilifikie taifa na iwapo zitalifikia, makali yake yawe nafuu. [158]
- tako
- HE jamani, mambo ya nishani ya viatu na tuzo la tako yameleta ubishi mkubwa sana. [159]
- tamaa
- Msemo huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua maendeleo ya watu mbalimbali hasa pale kunapoonekana kuna vikwazo ambavyo vinakatisha tamaa, na hivyo kufanya baadhi ya watu au kikundi cha watu kuanza kujitenga kwa ama kukatishwa tamaa, ama kuona mambo hayatakuwa kama wanavyofikiria. [160]
- tangu
- Hapa nchini tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kumekuwa na ushindani dhaifu dhidi ya chama tawala CCM katika chaguzi zote zilizofanyika tangu mwaka 1995 ulipofanyika uchaguzi mkuu chini ya mfumo wa vyama vingi. [161]
- tathmini
- Wenzetu Rwanda, Kenya, Uganda wanakimbia wakati sisi ndio kwanza tunajikongoja na tunajisifu uchumi unakua, lakini ukifanya tathmini ya kina utagundua kuwa badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma," anasema Dk. [162]
- tatu
- Ndivyo unavyoweza kufupisha kitendo cha baadhi ya wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara kujitokeza hadharani na kumtetea rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa. [163]
- teke
- Hili teke linalotujia wazee limepindua ulimwengu maana sasa ni watoto na vijana wanaojua si sisi wazee. [164]
- tena
- Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 14 mwakani itakapotajwa tena. [165]
- timu
- Mwakyoma alisema taarifa hizo timu ya askari ilitembelea eneo la nyumba hiyo ambapo hata hivyo hawakufanikiwa kumkuta mfanyabiashara huyo na badala yake walimkuta mke wake aitwaye Mwanaidi Ramadhani (25). [166]
- tu
- Si hilo tu amefanya mengi ambayo anastahili kuheshimiwa na kuachwa apumzike. [167]
- tukiwa
- Nahodha Henry Joseph alieleza:"Uungwaji mkono ambao mmetupa tukiwa Taifa Stars, unahitaji ili tuweze kulileta kombe ambalo Tanzania imelikosa kwa muda mrefu. [168]
- tume
- Hata hivyo sisi waishiwa tulifaidi sana maana tulikuwa tumeshajiteua kuwa tume ya tuzo. [169]
- tuna
- Hakuna mgawanyiko ndani ya chama chetu cha CCM na hakuna wabunge waliogawanyika wote ni kitu kimoja na tumejipanga vizuri na tunamwomba Mwenyezi Mungu atusaidie ili tuweze kupata ushindi kwa asilimia kubwa na tuna imani kuwa tutashinda," alisema. [170]
- ufisadi
- Meghji na Mramba, wamepoteza nyadhifa zao wiki chache baada ya kuibuka kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ni taasisi ya umma iliyo chini ya wizara waliyokuwa wakiiongoza kwa nyakati tofauti. [171]
- ukanda
- Musonye alisema katika kikao hicho walizungumzia maendeleo ya soka la vijana kwenye ukanda wao pamoja na maandalizi ya Taifa Stars inayoshiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN). [172]
- ule
- Katika maelezo yake, Spika Sitta alisema kuwa mfumo uliotumika mwaka jana kuwafikishia wabunge fomu hizo kwa kuzituma majimboni mwao umesababisha usumbufu, tofauti na ule wa miaka iliyopita wakati wabunge walipokuwa wakigawiwa fomu hizo kwenye kikao chao cha mwezi Novemba. [173]
- umma
- Rais alitaja taasisi nyingine za umma ambazo utendaji wake ulikuwa mbaya ni Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). [174]
- vifaa
- Haitoshi kuwa na vyumba vya madarasa kama vifaa vya kufundishia havipo au havitoshi, na hakuna walimu wa kutosha. [175]
- vumbi
- Yanga itafanikiwa kuingia raundi ya pili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika inayotarajiwa kutimua vumbi Februari Mwishoni kwa kuanza na timu kutoka Comoro. [176]
- vyao
- Baraza, George Owno , wote wa Yanga hawakuonyesha viwango vyao, Joseph Shikokoti alikuwa benchi. [177]
- wadau
- Ripoti hiyo imewashitua wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa, kidiplomasia na kiuchumi nchini ambao wanasema kuwa ripoti hiyo inapotosha umma wa Watanzania kwa kuwa haijazungumzia uhalisia wa uchumi wa nchi. [178]
- waheshimiwa
- Imebainika sasa kwamba baadhi ya waheshimiwa wabunge hawakuzipata fomu hizo. [179]
- wakisema
- Watu waliotoa maoni yao kuhusu hilo walionyesha kuridhishwa kwao na kitendo cha serikali kuwapandisha kizimbani mawaziri wawili wa zamani wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi, huku baadhi wakisema kuwa bado wengi zaidi wanatakiwa kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. [180]
- wala
- Suala la mafuta kupanda ni suala la wamiliki wa vituo vya mafuta wala halihusiani na sikukuu za Krismas ama sisi kufunga ofisi wakati wa sikukuu na wala lisihusishwe na suala la maharamia wa Kisomali, bali ni maamuzi ya wamiliki wa vituo vya mafuta ya kupandisha bei kwa sababu wanazozifahamu. [181]
- walio
- Baada ya kuwapelekea walimu katika vituo hivi, Armstrong anakiri kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya kimtazamo kuhusu elimu kwa Wahadzabe walio wengi. [182]
- wangu
- Wakati naanza kuifundisha Stars wachezaji wangu walikuwa na hofu pale watakapokutana na Cameroon au timu yoyote, lakini niliwaambaia waondoe kitu hicho na kusikiliza maelekezo yangu, nafikiri walifanya nini kwenye michezo iliyiopita,"alisema. [183]
- wao
- Alizungumza masuala mengi yakiwemo ya sheria zilizotumika kumuondoa na akazikosoa na hatimaye aliwataka wananchi wawe wavumilivu, hata kama rufaa yao haitakubaliwa kwa kuwa atawaachia wananchi wenyewe waamue hatima ya mustakabali wao ingawa pia aliwahakikishia kuwa haki yao lazima wataipata. [184]
- wasiwe
- Tunakiri kwamba akiba yetu inatosha hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi. [185]
- wengi
- PAMOJA na kuwekewa pingamizi na hatimaye kuenguliwa kwa mgombea wake wa ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kiliendelea kupiga kampeni katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na watu wengi. [186]
- wenyeji
- Katika michuano hiyo, Stars imepangwa Kundi A ikiwa na wenyeji wa michuano hiyo, Ivory Coast pamoja na Senegal na Zambia. [187]
- wetu
- Navionya vyama vya upinzani vinavyosema kuwa vitamkashifu rais wetu mstaafu wa awamu ya pili wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi katika jimbo la Mbeya Vijijini, kuwa hatutakubaliana na vitendo hivyo. [188]
- wewe
- Hiyo itakupa nafasi ya kuona wewe ni mtu muhimu kiasi gani na huenda ikawa nafasi nyingine kwako kumshukuru tena Muumba. [189]
- wiki
- Katika makubaliano yetu ya kupanga bei tumeafikiana mambo mawili moja ni kukutana na Ewura kwa ajili ya kubadili takwimu za bei ya mafuta nchini na suala la pili ni kukutana kila wiki mara mbili - Alhamisi na Jumatatu- kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali, likiwemo suala la hali ya bidhaa hiyo," alifafanua Bisarara. [190]
- yeye
- Katika mahojino ya tukio hilo mke wa mfanyabiashara huyo alikiri fuvu hilo kukutwa ndani ya kisadolini lakini alisema hajui kichwa hicho kilifikaje kwani hata yeye ameshitushwa na tukio la askari kukuta fuvu hilo. [191]
- yote
- Ingawaje Rais mwenyewe amekuwa akipita na kujigamba kuwa wananchi wasiwe na hofu itakapofika 2010 yote aliyoyaahidi yatatekelezwa lakini muda umeshakuwa kikwazo kwake. [192]
- zake
- CCM inatarajia kuzindua kampeni zake za ubunge Januari 4 kwenye kijiji cha Ilembo kilicho tarafa ya Isangati, ikiongozwa na rais huyo wa serikali ya awamu ya pili. [193]
- zao
- WABUNGE wametakiwa kurejesha fomu za tamko la mali zao walizopatiwa na Ofisi ya Kamishna wa Maadili ndani ya siku 14 kuanzia leo, Spika wa Bunge Samuel Sitta amesema. [194]
- zenu
- Meseji zenu, email zenu zilinipa nguvu ya kuendelea na kila siku nilikuwa nasema hilo. [195]
- zetu
- Kwa mwaka mpya wa 2009, tutafanya kazi zetu tukiweka umuhimu katika kufuata sheria na katiba ya nchi. [196]
- zichukuliwe
- Hatua zichukuliwe dhidi ya warsha zisizo na maana. [197]
- zile
- Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Muhammed Seif Khatib alisema harakati hizo hazina tofauti na zile zilizoongozwa na Kanal Bacar wa visiwa vya Anjourn nchini Comoro. [198]
- zisizo
- Anasema kuwa, serikali inapoangalia kipengele cha ajira huangalia zaidi katika ajira zisizo rasmi, jambo ambalo ni kinyume na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwapatia Watanzania ajira milioni mbili. [199]
- zoezi
- Hata hivyo, jana Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa inayobainisha kuwa baadhi ya wabunge hawakuzipata fomu hizo kama ilivyokusudiwa na Ofisi ya Kamishna wa Maadili mwenye dhamana na zoezi hilo. [200]