ChriKo
ChriKo, salam. Nina jambo moja ninataka kukueleza. Eti si umeona kuna baadhi ya sehemu nimeweka template "WIKIPEDIA" kwa maana ya kuelekeza ukurasa wa hapa uende kule kwenye Wikipedia? Tazama tembo utaona nimefanya hivyo. Eti ninaona afadhali na hizi makala zako za ndege nazo ziwe kama hivyo!! Kazi ndogo. Fanya hivi {{wikipedia|lang=sw|{{PAGENAME}}} basi itapeleka ukurasa huu kule kwenye Wikipedia ya Kiswahili! Kila la kheri.--Muddyb Blast Producer (majadiliano) 08:25, 6 Agosti 2009 (UTC)
- Ahsante, Muddyb, nitaifanya. ChriKo (majadiliano) 17:19, 6 Agosti 2009 (UTC)
- Kumradhi, mzee wangu. Nilikosea kuandika tahajia moja moja ya lugha. Yaani, lang=sw... Niliandika lag=sw, badala ya lang=sw!! Kazi njema.--Muddyb Blast Producer (majadiliano) 10:44, 7 Agosti 2009 (UTC)
- ChriKo, salaam! Nimeona ukiendelea kuongezea viungo kutoka hapa kwenda Wikipedia ya Kiswahili. Lakini naona kama bado hujatimiza baadhi ya uga? Tazama hii:
- {{wikipedia|lang=sw|Kukuziwa}}
Ukiweka hivyo, itataja jina la lugha ya Wikipedia yenyewe. Kwa mfano:
Inasema Wikipedia ya Kiswahili ina... Na hata ukiweka kwa it, af, en, na kadhalika, basi itasema ni Wikipedia ya lugha gani. Sehemu ya lang= ni namna ya kigezo kilivyojengwa ili kiweze kutaja aina ya wikipedia kwa kufuatana na makala! Kifupi usiweke wikipedia tupu bila lang=... Kila la kheri.--Muddyb Blast Producer (majadiliano) 14:41, 22 Septemba 2009 (UTC)