viza
Viza inaweza kuwa kivumishi au nomino.
Kama kivumishi sharti iambatane na yai. Yai viza ni yai bovu; yai ambalo halijakamilisha ukuaji wa kifaranga; yai lisilokomaa.
Kama nomino iko katika ngeli ya i-/zi-. Ni hati maalumu inayomruhusu mtu aliye raia wa nchi nyingine kuingia katika katika nchi ya kigeni. Imetokana na neno la Kiingereza 'viza'.