ukilima pantosha utavuna pankwisha
Ni methali yenye maana kuwa ukilima shamba ndogo huku ukidai kuwa panakutosha utakuja kuwa na mapato haba ambayo utayamaliza mara moja na kulalamika kuwa yamekwisha.
Hutumiwa kuonya dhidi ya tabia ya uvivu na kuhimiza tufanye kazi kwa bidii ili tupate manufaa makubwa.