Kiswahili

hariri

Nomino

hariri

ramli

  1. utabiri unaofanywa na wataalamu wanaotumia nyota au vifaa vingine

Tafsiri

hariri

Ramli Ni neno lenye asili ya kiarabu likiwa na maana mchanga(kwa kiingereza sand).

Jamii nyingi hutumia neno hili kumaanisha utabiri au ubashiri wa Mambo mbalimbali ikiwa pamoja na magonjwa, shida, Mambo ya mapenzi, biashara n.k
Kulihusisha neno hili na utabiri Ni kutokana na hadithi inayovuma kwa watu wanaofanya utabiri wa nyota kuwa, Kuna nabii mmoja wa Zama za unabii alifundishwa elimu ya utabiri na malaika jibril kwa kuandika katika mchanga, hapa ndipo ilipopatikana asili ya kuita vitendo vyote vya utabiri RAMLI.

Kuna njia mbalimbali zinatumika katika kubashiri shida au matatizo ya mtu, aliyonayo au ya wakati ujao. Moja ya njia hizo Ni Kama ifuatavyo;- 1. Kusoma saa. Kuna wanaobashiri shida, matatizo au maradhi kwa kuangalia saa aliyoulizwa swali na mtu mwenye shida.

Kwa mujibu wa watabiri kila saa Ina nyota yake maalum ambayo inaisimamia na hiyo ndio hutoa tafsiri ya shida, matatizo au magonjwa ya mtu.

2. Kusoma shikeli. Hizi zinapatikana baada ya kuchora vistari Bila ya kuhesabu huku mtabiri akijiuliza tatizo la mtu. Kisha hukata vistari viwiliviwili na mwisho vitakavyobaki huandikwa pembeni na kutafsiri kutokana na hivyo vilivyobaki.

3. Kuita jini(shetani). Wapo pia baadhi ya watu hutumia majini kwa kuwaita na kupanda ndani ya vichwa vyao Kisha Juni huyo hutumia kinywa Cha mtabiri kutoa maelezo ya utabiri. Wapo wengine waliozama kwenye elimu ya kiza huwaita majini na kuweza kuonana uso kwa uso na wakatabiri shida au Mambo mbalimbali ya mtu.

Zipo njia kadha wa kadha zinazotumiwa na watu wa jamii mbalimbali duniani kutabiri. Hizo tatu Ni baadhi tu ambazo hutumika zaidi na watu wengi.