mabano
Mabano/parandesi/braketi/vifungo.
Mabano ni nomino.
Mabano yako katika ngeli ya ya-.
Mabano ni alama za nusu mviringo zinazotumika kuzingira maandishi. Kwa mfano: (nukta). Kisawe cha mabano ni braketi.
Parandesi ni ( ), / /, { } au [ ].
Matumizi ya mabano. 1. Kufungia maneno yatoayo maelezo zaidi kuhusu maneno yanayotangulia. Mfano: aliootelea jijini (Nairobi). 2. Kubainisha nambari katika orodha. Mfano: (1.)...(2.)... 3. Kubainisha herufi katika orodha. Mfano:(a)...(b)...