kistari kirefu
Kistari kirefu(_) hutumiwa: 1. Kutoa maelezo zaidi. Kwa mfano: nchi zote za Afrika Mashariki_Kenya, Uganda na Tanzania_zinawavutia watalii wengi kila mwaka. 2. Kuonyesha mabadiliko ya ghafla. Kwa mfano: siwataki hapa watu wasiojua wanafanya nini_samahani, sikunuia kuwatusi. 3. Kuonyesha ni nani aliyesema maneno fulani. Kwa mfano: umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu_Peter Anyanzwa.