hakuna mchele ukosao ndume

Ni methali yenye maana kuwa katika kundi la watu wengi wema, hapakosi kuweko na mmoja mbaya.

Hutumika kukumbusha kuwa wabaya na wazuri wamechanganyikana.