Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-02-09

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aende
Wimbo huo ulimfanya aende katika Umoja wa Mataifa kumuaga Koffi Annan alipomaliza muda wake wa ukatibu mkuu wa umoja huo. [2]
aina
MAITI ya mwanaume mmoja imekutwa ikiwa imetelekezwa ndani ya gari aina ya Toyota Corola, katika ghorofa ya kwanza ya maegesho ya magari katika jengo la J-Mall ambalo sasa ni Harbour View. [3]
akioza
Samaki mmoja akioza, wote wameoza. [4]
akisema
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile hakutaka kuzungumzia suala hilo akisema taarifa za tukio hilo zitatolewa leo 3.00 asubuhi. [5]
akiwa
Alisema matengenezo hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika wakati Balali akiwa gavana. [6]
alifoka
Sasa huo si ujinga, picha ndio nini? Picha ndio dawa,” alifoka Kazim hali iliyomfanya waziri aendelee kufadhaika na kumueleza kuwa watakachokifanya ni kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari. [7]
alisoma
Siku moja baada ya kukutana na jamaa huyo alisoma taarifa kwenye gazeti moja kwamba kuna biashara kubwa ya kununua viungo vya albino kwa ajili ya machimbo ya madini na biashara ya uvuvi. [8]
ambako
Alisema kama kweli wachezaji hao wanavuta bangi basi wanapaswa kulaumiwa na klabu zao ambako wanakaa na hao wachezaji kwa muda mrefu na timu ya taifa wanakaa kwa muda tu. [9]
amesema
KOCHA wa timu ya Mtibwa Sugar ya Turiani, Salumu Mayanga amesema kufungwa na Prisoni si kikwako kwake kuchukua nafasi ya pili. [10]
ana
Ni mchezaji kijana menye miaka 20 na ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, chenga zake za maudhi na hata ufungaji wa mabao matamu ndicho kitu kinachowavutia mashabiki kutaka kumuangalia kila mara. [11]
anataka
Hakusikilizi, anataka umsikilize. [12]
anaweza
Huwezi kumleta Mshindo Msolla siku tatu au tano kabla ya mechi ukategemea kwamba, anaweza kuongeza makali yoyote kwenye timu. [13]
au
Nyumba hiyo, ambayo ipo eneo la Masaki, ni maalumu kwa ajili ya gavana au manaibu wake, lakini hadi sasa si gavana mpya, Profesa Benno Ndulu, wala manaibu wake, hakuna aliyehamia kwenye nyumba hiyo. [14]
baada
Gavana Ndulu alisema kuwa ni kweli kwamba nyumba hiyo ilipaswa kukaliwa baada ya kipindi cha miezi sita ya kukamilika kwa uhamishaji wa mali za Balali, lakini matengenezo yamesababisha nyumba hiyo iendelee kuwa wazi. [15]
baadaye
Endapo itashindikana, timu hiyo itaondoka Februari 14 na kurejea siku nne baadaye ikiwa ni siku moja kabla ya Stars kuondoka kwenda Ivory Coast. [16]
badala
Moja ya mambo ambayo yalisababisha ratiba ya shughuli za bunge kuvurugika tofauti na ilivyokuwa imepangwa awali, ni kujadiliwa kwa siku tatu mfululizo kwa muswada wa wanyama pori kutokana na mvutano ulioibuka bungeni, na semina ya wabunge kuhusu msukosuko wa kifedha duniani kufanyika Jumatano badala ya Jumamosi iliyopita. [17]
bado
Leo (jana) sina chochote kwani uchunguzi wa tukio hilo bado; si unajua mambo yangu sibahatishi," alisema Kamanda Kova. [18]
bahati
Wiki kama mbili tatu zilizopita kiwanja kilikuwa kinondoni Morocco, unaona bwana, mahala panaitwa Zhonghua Garden, burudani ilikuwa ikipatikana pale, na kwa kuwa ni karibu na makazi ya watu bahati mbaya ikawa yaisha kama mapema hivi, ...si unajua raha ya burudani kukesha? Malalamiko yaelekea yalifika kunako, na habari mpya kwa wasioijua, hii hapa. [19]
bali
Si kwamba Maximo alikuwa hasikii kelele hizo bali alisema kuwa wachezaji anaowataka katika timu yake ni wale wanaocheza klabu za Ligi Kuu ili iwe rahisi kuwafuatilia hivyo kuwataka wachezaji kutafuta timu za anga hizo. [20]
bangi
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limerahani vikari baadhi ya watu wanaowatuhumu wachezaji wa timu ya Taifa Taifa Stars kuwa ni wavuta bangi. [21]
bia
Tumeona jinsi kampuni ya bia ya Serengeti na Benki ya NMB yanavyoidhamini timu yetu ya taifa ya mpira wa miguu, kampuni ya bia ya TBL inavyozidhamini timu za Simba na Yanga, Benki ya Standard chartered inayodhamini timu yetu ya riadha iliyopo hivi sasa kwenye mashindano nchini Hong Kong na Vodacom kwa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara na timu yetu ya baiskeli inayoshiriki hivi sasa mashindano ya mchezo huo kwa nchi za Afrika Mashariki yaliyoanza jana Mjini Nairobi Kenya. [22]
bila
Alisema malengo ya mapinduzi ya mwaka 1964 yalikusudia kuleta umoja kwa Wazanzbari na kuimarisha usawa na kuwajengea misingi ya maisha bora wananchi wake bila ya ubaguzi wa aina yoyote. [23]
budi
Katika hatua nyingine Maximo alisema jana kuwa klabu za Simba, Mtibwa Sugar, Yanga na nyingine zenye wachezaji timu ya taifa, hazina budi kumshukuru kwa kuwatengenezea wachezaji wazuri. [24]
cha
Hivyo kiwango cha ufaulu kwa mtihani wa maarifa kimeongezeka kwa asilimia 2.58 mwaka 2008 ikilinganishwa na mwaka 2007," inaeleza taarifa ya Ndalichako. [25]
chake
Balali alifariki mwaka jana akiacha kashfa kubwa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), kwenye taasisi hiyo kubwa ya kifedha na kifo chake kimeelezewa kwa hisia tofauti. [26]
chenye
Timu hiyo itaondoka ikiwa na kikosi chenye wachezaji 20 na viongozi 6 kwa mchezo huo wa marudiano. [27]
dereva
Kwanza alipambana naye mlangoni, lakini mlevi huyo akafanikiwa kuingia kwenye gari na dereva akaanza safari kutoka Kituo cha Relini, Tabata kuelekea Gongolamboto. [28]
dhati
Kama kukiwepo na juhudi za dhati na kila mchezaji akaelewa somo na benchi la ufundi likafanya kazi yake kiumakini, hakuna kinachoshindikana. [29]
es
Mary Goreti (Kilimanjaro), Shule ya Wavulana ya Feza (Dar es Salaam), Seminari ya Don Bosco (Iringa) na Rosmini (Tanga). [30]
fainali
Awali Shirikisho la soka TFF, liliwaomba Yanga kuwaacha wachezaji wake waliopo timu ya Taifa iliwaendelee na mazoezi ya kujiandaa na michuano ya fainali za Afrika kwa ajili ya wachezaji wa ndani ( CHAN). [31]
fulani
Hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya makampuni hapa nchini yakijitokeza kudhamini michezo mbalimbali na kuwezesha michezo hiyo kubadilika kwa kiasi fulani na kuongeza ufanisi na hamasa kwa michezo husika. [32]
furaha
Lakini pamoja na yote lililo la msingi katika michezo ni kujali sheria na haki zitumike kwenye kutoa uamuzi, kwani michezo ni furaha na kujenga urafiki. [33]
gani
MIAKA mitatu mpaka minne iliyopita ungeniuliza ni timu gani ambayo ilikuwa ikinivutia kwenye Ligi Kuu ya Bara, ningekuambia Prisons ya Mbeya ambayo inamilikiwa na jeshi la Magereza. [34]
ghafla
Na wakati naangalia hivi nikasikia ghafla kama samaki wa chini wanaanza kuongea. [35]
haina
Hata hivyo, Maximo alisema hawezi kuchagua wachezaji wa Taifa Stars kutoka Zanzibar kwa kuwa ligi ya Zanzibar haina kielelezo kamili cha kumtathmini mchezaji kwa kuwa inachezwa katika kipindi kifupi. [36]
hajui
Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [37]
hana
Mwinyi kuwa ananyemelea nafasi hiyo ya urais wa Zanzibar wakati vikidai kuwa hana sifa. [38]
hao
Baadaye walinzi hao waligundua uwepo wa kitu katika gari hiyo aina ya Toyota Corola ambayo ilikuwa imeegeshwa katika ghorofa hiyo na baada ya kufanya utaratibu wa kulifungua walikuta maiti hiyo ya binadamu ikiwa ndani ya mfuko. [39]
hapa
Kampeni hizo zilizinduliwa juzi kwenye Uwanja wa Komba Wapya na naibu katibu Mkuu wa chama hicho visiwani Zanzibar, Hamada Mussa Yussuf, ambaye alisema kuwa vitendo vya ufisadi visiwani hapa ni vikubwa ukilinganisha na Tanzania Bara. [40]
hapo
Msanii huyo mzawa wa Dar es salaam alianza kusikika Octoba 2006 na hakutegemea kama ndani ya miaka miwili angefika hapo alipo, lakini kwa sasa, anajivumia mafanikio makubwa, huku akishangaa jinsi alivyopokelewa haraka na jamii na kwa mikono miwili. [41]
hasa
Lengo langu ni kuwa dereva, hivi sasa nakusanya pesa kidogo kidogo ili zinisaidia kusomea udereva hasa wa magari makubwa ya abiria," anasema. [42]
hatutaki
Sisi hatutaki, hatutaki lakini tutatupwa kama hao. [43]
hawezi
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Marcio Maximo amesema kimsingi hawezi kuwazuia wachezaji wa Yanga kwenda kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Etoile d’Or Mirontsy ya Comoro wiki ijayo kwani suala hilo ni la kiutawala zaidi. [44]
hayuko
Atataka umfanyie hiki umfanyie hiki lakini yeye hayuko tayari kwa lolote juu yako. [45]
hii
Tunalaani matukio yote ya kukutwa kwa vinasa sauti katika vyumba vya wabunge wa Chadema na CUF na pia tunasikitishwa sana na uharamia wa namna hii kwa viongozi wetu ambao wanafanyiwa kutokana na harakati zao za kupinga ufisadi," alidai Mnyika. [46]
hiki
Sehemu ya mashairi ya wimbo huo ni, 'niambie, niambie nilichotenda, niambie rafiki, labda nilipitiwa' ,katika wimbo huu nilimlenga rafiki yangu wa dhati aliyekuwa amekumbwa na kisa hiki," anasema Mwasiti. [47]
hili
Sisi Chadema tunaamini kwamba matukio haya yanahusiana moja kwa moja na baadhi ya wanausalama wa taifa na maafisa wa vyombo vya dola waliozisaliti kazi zao na kuamua kusimamia usalama wa mafisadi dhidi ya haki za wazalendo wa taifa hili," alidai Mnyika bila ya kutaja mtu maalum anayehusika. [48]
hivi
Maulid alisema Ligi Kuu ya Zanzibar inatazamiwa kuanza hivi karibuni licha ya kuibuka kwa utata kwa upande wa udhamini wa ligi hiyo ZANTEL na klabu zinazoshiriki ligi hiyo. [49]
hiyo
Idadi hiyo ni pungufu kulinganisha na ya mwaka 2007 ambapo jumla ya watahiniwa 597 walifutiwa matokeo, 526 kutoka shuleni na 71 wa kujitegemea," inaeleza taarifa ya Ndalichako. [50]
hizi
Kauli nyingine za serikali ambazo zinatarajiwa kutolewa katika siku hizi tatu za mwisho wa mkutano wa 14 wa bunge, ni juu ya uendeshaji usioridhisha wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na ya upakuaji wa mizigo bandarini ya Ticts. [51]
hospitali
Alihangahaika kwenye hospitali nyingi bila mafanikio. [52]
huko
Hata hivyo, Yanga imeiomba TFF kusaidia kupatikana kwa ndege ya kukodi kwa ajili ya wachezaji hao kwamba baada ya mchezo huo warudi mara moja kuendelea na kambi, na vinginevyo watakaa huko kwa siku zaidi ya tano. [53]
huo
Profesa Ndulu aliongeza kwamba baada ya ukarabati huo, mmoja wa manaibu Gavana atapaswa kuhamia, akimtaja kuwa ni Juma Reli, ambaye anashughulikia utawala. [54]
huu
Si kama malalamiko yatufikiapo tunayatupa na kuyadharau isipokuwa tunayashughulikia na kwa hakika hatutawavumilia wanaopiga muziki kwa sauti ya juu au maonyesho ya muziki (live band show) huu ni mwanzo na kwa watakaokaidi tutawafikisha mahakamani,"alisema. [55]
huwa
Sioni aibu kupiga debe kuita abiria kwenye daladala yangu, wapo wanawake wenzangu huwa wananidharau na kunitemea mate wakati mwingine, lakini huwa siwajali kwani hawajui kwa nini nimefikia hatua ya kufanya kazi hii,"anasema. [56]
iko
Mbali na hilo, Maximo alisema timu yake iko vizuri na anajivunia kwenda Ivory Coast na timu ambayo si ya kubeza. [57]
ila
Mama huyo anasema hapatani na wahuni, ila anachokitafuta yeye ni kuhakikisha anapata pesa kwa ajili ya kuwatunza binti yake ambaye ameanza darasa la kwanza mwaka huu, na wazazi wake walioko Iringa. [58]
ile
Siku zote tunaamini kwamba nchi yoyote ile inayoandaa mashindano hujitahidi kuweka mkakati wa kujitahidi kulibakisha kombe nyumbani. [59]
ili
TRL imekuwa ikikumbwa na matatizo mbalimbali ya kiuendeshaji na ukata, kiasi cha kukopeshwa na serikali ili iweze kulipa wafanyakazi wake mishahara huku huduma za usafiri zikidorora, wakati Ticts imeshindwa kufanya kazi kwa ufanisi na kusababisha kulundikana kwa mizigo bandarini, kiasi cha wateja wa nchi jirani kufikiria kwenda bandari nyingine. [60]
iliyopo
Alizitaja baa hizo ambazo hazikupatikana na makosa katika ukaguzi huo kuwa ni Africentre iliyopo katika kata ya Mchikichini, Furaha baa iliyopo kata ya Gerezani na Hosea Hopaja Lugano Traders ya Buguruni. [61]
ina
Alisema nyumba anayoishi naibu huyo ina matatizo. [62]
ingawa
Na ingawa wote walikuwa wananuka, kila mmoja alikuwa anamnyooshea kidole mwenzie kwa nini ananuka huku akinuka mwenyewe. [63]
iwe
Alisema kuwa miswada ya sheria kama hiyo kwa kawaida inapitia hatua nne, zikiwemo za kupelekwa kwa wananchi kisha bungeni na kwa rais ili kuisaini iwe sheria. [64]
juu
Tuelewane, bwana mwandishi, sijathibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa kuwa nataka kutoa taarifa kamili kesho (leo) juu ya upelelezi wa tukio hilo hivyo kesho (leo) nitatoa taarifa kamili. [65]
kabla
Habari zilizopatikaka jana lilieleza kuwa mabingwa hao wanataraji kuongoka nchini Jumamosi siku moja kabla ya mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo kutoa nafasi kwa wachezaji wake kucheza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Zimbambwe inakayochezwa Jumatano wiki ijayo katika Uwanja Mkuu. [66]
kali
Maiti hiyo iligundulika jana asubuhi baada ya walinzi wa eneo hilo kusikia harufu kali ya kitu kilichoharibika, hivyo kuwalazimu kufuatilia. [67]
kama
Chadema imesema matukio hayo ni mwendelezo wa njama za vigogo wa serikali dhidi ya viongozi wao na kulitaka Jeshi la Polisi kumuhakikishia usalama mbunge wao na kama haliwezi kufanya hivyo liseme. [68]
kambi
Zumo alisema mabondia wote wako katika hali nzuri na wamekuwa wakiendelea na mazoezi katika kambi zao na wanatarajia kupima uzito Februari 12 katika ukumbi wa hoteli ya Blue Room mbele ya wadhamini wa pambano hilo kampuni ya Vodacom na Pepsi. [69]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [70]
kasi
Alidai kuwa taifa lipo shakani na kwamba wanawataka Watanzania wa dini zote kuliombea taifa livuke majaribu na kuongeza kasi ya kuibana serikali kuhakikisha mafisadi wote wanafikishwa mahakamani, kufungwa na kufilisiwa iwapo watakutwa na hatia. [71]
kata
Akizungumza na wanahabari jiji Dar es Salaam Afisa Habari na elimu kwa umma wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu alisema adhabu hizo ni kwa kata nane zilizokaguliwa. [72]
kichwa
Vikaratasi hivyo visivyoonyesha mchapishaji wala eneo vilikochapishwa, vimesambazwa kisiwani Unguja vikiwa na kichwa cha habari kisemacho "Zanzibar imefikishwa wapi na mafisadi baada ya miaka 45 ya mapinduzi" na kuelezea historia ya Mwinyi, huku vikimsihi aachane na siasa za Zanzibar. [73]
kila
Nilipofanya utafiti wa kina nikabaini kwamba, benchi la ufundi linataka kuunda timu yenye damu changa kwani hata wakongwe wengi walianza kupumzishwa na kupewa kazi nyingine za kila siku za maaskari wa kawaida wa jeshi la Magereza, ikiwa ni pamoja na kuangalia usalama wa wafungwa. [74]
kilikuwa
Ali Tarab kilikuwa kimezimwa na cha Dk. [75]
kina
Hata hivyo, kulundikana kwa mambo mengi mazito katika siku tatu za mwisho, huenda kukapunguza mwanya wa wabunge kujadili kwa kina kauli hizo za serikali. [76]
kisasa
Naye mratibu wa mpambano huo, Zumo Makame kutoka kampuni ya Best Man Promotion alisema maandalizi yote yameshakamilika ikiwa pamoja na kuwasili kwa ulingo wa kisasa kwa ajili ya mabondia hao. [77]
kombe
Hiyo ni rekodi ya aina yake kwa mabingwa hao wa Afrika ‘Red Devils’ kwani imetwaa mara ya tatu kombe hilo na kuifikia rekodi ya timu nyingine ya Misri, Zamalek. [78]
kubaki
Anachoogopa yeye ni kubaki nyumbani akisubiri kuomba badala ya kufanya kazi. [79]
kufa
Wakati wanaendelea kuangalia ile picha aliingia daktari aliyekuwa akimwangalia Kazim na kumwomba waziri afupishe mazungumzo, badala yake wamsake yule mvumbuzi wa dawa kwani isingepita saa 12 kabla ya Kazim kufa ikiwa hatapata ile dawa. [80]
kuja
Nikajuta maana katika kuongea hivi, nilikuwa nimewaita wengine wenye mnuko kuja kuongea na mimi. [81]
kule
Ndio ndugu, mimi naitwa Kazim ni mwenye mgodi wa madini ya almasi kule Mwadui, tatizo ni kwamba hali kwa sasa imekuwa mbaya mno, nimechanganyikiwa hapa hata sijui la kufanya,” alisema akiomba ushauri. [82]
kumbe
Atakufundisha mambo mabaya na kukufanya uamini ni mwenzie kumbe nia yake ni kukuharibia. [83]
kuna
Pia kuna tuhuma nzito dhidi ya baba yake, rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ikimuunganisha na muasisi wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwamba wao ndio kwa pamoja walisababisha Zanzibar kufikia hali iliyo nayo sasa. [84]
kuona
Akionyesha msisitizo wa kuchukizwa na hali hiyo, alisema ni jambo la kusikitisha kuona uchumi wa Zanzibar unayumba, lakini serikali inanunua magari ya kifahari kwa matumizi ya mawaziri, manaibu wao, wakuu wa mkoa na wilaya zote za Unguja. [85]
kuoza
Lakini alipofika kwenye tenga la tatu akaanza kutupa samaki mmoja baada ya mwingine, maana kila mmoja alionekana kuoza. [86]
kupata
Somo la siasa linashika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 62.09, likifuatiwa na jiografia (58.97) na la mwisho ni hisabati (24). [87]
kurudi
Timu hiyo ipo kwenye mapumziko mafupi wanatajia kurudi kambini wiki ijayo. [88]
kusomea
Amepanga kusomea udereva wa magari makubwa. [89]
kutafakari
Nikajaribu kutafakari. [90]
kutunga
Ninaziba masikio na kujifanya sijasikia chochote na ninampa muda mwingine wa kutunga wimbo mwingine lakini sitamjibu kabisa. [91]
kuua
Ni suala la kawaida kuua albino na damu zao au viungo vyao tunavitumia kwenye shughuli hizo za uchimbaji madini na uvuvi, watu wengi wanafanya hivyo. [92]
kuungwa
Mwanaharakati huyo alibainisha kuwa kutokana na kuungwa mkono na wanasiasa hao wanakusudia kufungua mtandao wa wabunge wa wanaopambana na utoaji mimba nchini. [93]
kuwa
Ufaulu wa masomo ya lazima unaonyesha kuwa somo la Kiswahili linaongoza likiwa na asilimia 81.59 ya ufaulu, likifuatiwa na Kiingereza (63.23). [94]
kuwaza
Nikaendelea kuwaza huku nikiangalia wachuuzi wale, nikagundua kitu kingine cha ajabu. [95]
kwako
Na wanakuja kwako wakiwa wanapeperusha hii bendera ya urafiki. [96]
kwao
Hata hivyo Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alisema hawataweza kukodi ndege kwa ajili ya wachezaji wa Yanga waliopo timu ya Taifa kwa kuwa suala hilo kwao aliwaasili sana kwa kuwa timu hiyo inarudi Feb 18 na 19 timu ya Taifa inaondoka kuelekea Ivory Coast. [97]
la
Kuhusu ubora wa kufaulu, wavulana wanaongoza kwa asilimia 3.22 dhidi ya 1.49 ya wasichana daraja la kwanza, wakati daraja la pili wavulana wakiwaacha tena wasichana kwa asilimia 5.86 dhidi ya asilimia 2.71 ya wasichana. [98]
lake
Hussein Mwinyi aachane na ndoto ya kutaka kuwa rais wa visiwa hivyo, akiwa ni mtu wa pili kufanyiwa vitisho hivyo baada ya Mohammed Seif Khatib ambaye naye alianzia kupewa vitisho vya kufunguliwa jalada lake na wakongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). [99]
leo
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova hakutaka kuelezea tukio hilo na kuahidi kuzungumzia suala hilo kesho (leo) ofisini kwake. [100]
ligi
Alisema moja ya njia ya kuchaguwa wachezaji ni kuangalia katika ligi, lakini kwa muda mrefu hakuna mechi au mashindano magumu yoyote yanayoendelakatika kisiwa cha Unguja na Pemba. [101]
lugha
Anazungumziaje matumizi ya lugha za matusi? "Nimejifunza kutumia lugha za kihuni na kuwa mkali ili kwenda sambamba na abiria ambao mara nyingine huwa wakorofi," anasema. [102]
mabao
Shirikisho la Soka Tanzania, TFF liliiomba Yanga kuwaacha wachezaji wa timu hiyo walioko Taifa Stars, lakini uongozi wake ulikataa kwa maelezo kwamba pamopja na ushindi wa mabao 8-1, lolote linaweza kutokea katika soka. [103]
macho
Alidai kuwa ujasusi wa kuyaweka rehani maisha ya viongozi wa vyama umekuwa ukifanywa kwa muda mrefu na kwamba walisharipoti Jeshi la Polisi bila ya kufanyiwa kazi na kwamba sasa umefika wakati wa kutoufumbia macho tena. [104]
madini
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [105]
maeneo
Baada ya kutoka kwao Iringa alipata kazi ya utumishi wa ndani katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, lakini kutokana na manyanyaso aliyokuwa anapata kutoka kwa waajiri wake aliachana na kazi hiyo. [106]
mara
Waweke ulinzi wa kukagua mara kwa mara, labda marehemu alitelekezwa eneo hilo akiwa na hali ya kujiweza na wangekuwa wanakagua wangemuokoa, lakini kwa kuwa siku tatu zote hawakukagua ndiyo maana kifo kimemkumba," alisema mmoja wa wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo. [107]
maswali
Ukweli ni kwamba hawaridhiki wala kuvutiwa na wanachokiona uwanjani ndani ya dakika 90. Kama umekuwa ukifuatilia Ligi Kuu ya Bara unaweza ukajiuliza maswali kadhaa. [108]
matenga
Kandokando yake yalikuwepo matenga ya samaki na mchuuzi alikuwa anayakagua moja moja. [109]
mazoezi
Akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Mao-Dse-Tung wakati timu ya taifa ikifanya mazoezi alisema mfumo huo umepitwa na wakati kwa sababu hauwaweki wachezaji katika kiwango cha kuwa tayari na mashindano. [110]
mbali
Vikaratasi hivyo vimekwenda mbali zaidi vikimuonya Dk. [111]
mdogo
Hatari zaidi isianze kufungwa, ikifungwa ndio wachezaji wanaonekana kuchanganyana na uwezekano wa kurudisha bao na kushinda unakuwa mdogo sana na kama imewahi kutokea msimu huu si zaidi ya mara moja. [112]
mdomo
Hawezi kufunga mdomo wake kuzungumza mambo yako. [113]
mema
Atageuza mambo mema kuwa maovu na kuonyesha kosa katika matendo yako mema na huenda anafurahia mabaya yaliyokukuta huku akijifanya kukuhurumia, utaona vile anavyokuzungumza kwa watu. [114]
mfumo
KOCHA wa Tanzania, 'Taifa Stars' Marcio Maximo ameponda mfumo mzima wa kuendesha wa Ligi Kuu ya Zanzibar kuwa umepitwa na wakati kwa sasa. [115]
mfupi
Lakini muda mfupi baadaye usumbufu wa kilevi ulipozidi ndani ya gari, kondakta huyo, alivaa uhusika wake halisi. [116]
mimba
MTANDAO wa kutetea uhai wa viumbe(Pro-Life Tanzania) umedai umefanikiwa kuwapata wabunge wengi wakiwemo mawaziri wanaojiandaa kuupinga kwa nguvu zote muswada wa kuruhusu utoaji mimba unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni siku zijazo. [117]
mimi
Mimi ni mchezaji mwenye uwezo mdogo sana na naamini kuna wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini nafikiri kocha ana makusudi na mimi. [118]
minne
Mwanyangali alisema kutokana na mkataba huo, mwanamke atakuwa na ruksa ya kutoa mimba kuanzia ya wiki tatu mpaka wiki 18 sawa na miezi minne na nusu na baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania zilisaini makubaliano hayo lakini bado haijaridhia rasmi. [119]
miwili
Aina hiyo ya propaganda pia iliwahi kufanywa dhidi ya Waziri Khatib miezi miwili iliyopita. [120]
mkuu
Akizungumza na waandishi jijini jana, kaimu katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema wanaamini kwamba matukio hayo yanahusiana moja kwa moja na vigogo wa dola walioisaliti kazi na wajibu wao na kuwa walinzi wa mafisadi na kutaka kumuua mbunge huyo. [121]
mno
Maelezo haya yanafanana kabisa na matukio ya hivi karibuni ya Rais Jakaya Kikwete alipokuwa katika ziara mkoani Pemba kuwabeza wapinzani na kuwakatisha tamaa kwamba inawezekana ikawachukua muda mrefu mno kuongoza dola au hawataweza kabisa. [122]
mnuko
Au hata akibaki hajaoza, bado atanuka kama wenzie maana amekaa kwenye tenga la mnuko mtupu. [123]
mradi
Wilbroad Slaa na njama za kutaka kumuua, kwa madai kuwa anasimamia kidete sakata la mradi wa vitambulisho vya taifa wenye thamani ya Sh200 bilioni. [124]
msaidizi
Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [125]
msimu
Akizungumza na Mwananchi jana Mayanga alisemakupoteza mchezo wao dhidi ya Prisoni ya Mbeya haiwazuii wao kushika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu. [126]
muda
Atahamia wakati wowote katika muda wa mwezi mmoja," aliongeza. [127]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [128]
mwa
Slaa, mmoja wa wachangiaji wakubwa na wakosoaji wa serikali bungeni, alidai mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa amekuta vifaa vya kunasa sauti vikwia vimetegwa kwenye kitanda chake, jambo ambalo alisema anaamini kuwa lilifanywa na watu wasiopendezwa na tabia yake ya kufuatilia kwa makini masuala ya ufisadi. [129]
mzito
Vikiwa na maandishi ya kawaida vikaratasi hivyo vya kurasa moja vimeandikwa pande zote mbili, huku maneno yanayoonekana kuwa na nguvu yakipigiwa mstari kuonyesha msisitizo na baadhi ya maneno yakiandikwa kwa herufi kubwa na kuwekewa wino mzito. [130]
mzuri
Miongoni mwa vitu hivyo ni morali, jihadi pamoja na mchezo mzuri wa pasi za kuonana uliokuwa ukichezwa na timu hiyo inayotumia uwanja 'chakavu' wa Sokoine kama sehemu yake ya kujidai. [131]
na
Pia, katika matokeo hayo, shule zilizoshika nafasi 10 za kwanza ni watu binafsi na mashirika ya dini kutoka Tanzania Bara, huku Zanzibar ikikosa hata shule moja katika kundi hilo, wakati shule 10 za mwisho zikiwa mchanganyiko wa zile zinazomilikuwa na watu binafsi na serikali, tatu kati ya hizo zikiwa ni za Zanzibar. [132]
nami
Nilipenda sana kuwa msoni na nifanye kazi za ofisini, lakini sikubahatika kusomeshwa, kwani wazazi wangu hawakuwa na uwezo huo, ilinilazimu nijitose huku walau nami niwe na kipato changu kwa kazi halali," anasema. [133]
nani
Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuhusu vinasa sauti hivyo lakini halikueleza kwa kina, vinatoka wapi, vimewekwa na nani na kwa nini cha mbunge wa Konde, Dk. [134]
nao
Aliutaka umma wa Watanzania kuelewa kwamba kadri serikali inavyochukua muda mrefu kuwafikisha gerezani mafisadi ndivyo inavyotoa mwanya kwa mafisadi kuangamiza uhai na maisha ya wazalendo wanaojitolea kupambana nao. [135]
navigator
MSIE = navigator. [136]
nayo
Kutokana na kubaini hilo, walinzi hao walitoa taarifa polisi ambao jana mchana waliitoa maiti hiyo na kuondoka nayo. [137]
ndipo
Hapo ndipo nilimtambua mwanamke huyo, tumuite wa shoka. [138]
ndiye
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndiye atatoa taarifa hizo juu ya hatua ambazo serikali imechukua, baada ya Kamati ya Bunge kubaini ukiukwaji wa taratibu katika utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa Richmond. [139]
ngozi
Ukweli ni kwamba wapo pia katika kundi la marafiki, 'marafiki maadui' waliojivika ngozi ya urafiki. [140]
nia
Mwinyi, ambaye ni mtoto wa rais mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano, Ali Hassan Mwinyi, ni mmoja wa watu wanaotajwa katika kinyang'anyiro cha kuingia Ikulu ya Zanzibar licha ya waziri huyo kutoweka bayana nia yake. [141]
nikiwa
Ukiachilia yote hayo kubwa zaidi linalonifanya nijivunie ni wimbo ‘A New Day For Africa' ambao tuliimba wasanii wote wa Afrika kwa kuwa nilitumbukiza vionjo nikiwa na Prof. [142]
nyuma
Miaka ya nyuma ilikuwa ajabu kuona mwanamke akiwa kondakta wa daladala, wachache walikuwa kwenye mabasi ya masafa-Royal Sumayi, Scandnavia Express, Fresh ya Shamba, Dar Express, Kilimanjaro Express na mengineyo. [143]
nzito
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeibua tuhuma nzito kwa kuyahusisha moja kwa moja matukio mawili yaliyompata mbunge wa Karatu kwa tiketi ya chama hicho, Dk. [144]
of
Pitt amechaguliwa kwa kuwa muigizaji bora wa filamu ya The Curious Case of Benjamin Button ambayo aliigiza kama mtu mwenye umri mkubwa kuliko alionao. [145]
pale
Ni kweli hadi sasa hakuna mtu anaishi pale. [146]
pamoja
Pia shule 10 bora zilizokuwa na watahiniwa chini ya 35 ni pamoja na Scolastica (Kilimanjaro), Feza (Dar es Salaam), Brookebond (Iringa), Bethelsabas (Iringa) na Seminari ya Maua (Kilimanjaro). [147]
pekee
Jambo pekee litaloweza kuleta mabadiliko hapa ni kubadili mfumo wa ligi na kwenda na wakati kwa kuangalia ligi za nchi mbali mbali duniani. [148]
pia
Kwa mujibu wa ratiba hiyo mpya, ndani ya siku tatu serikali pia itatoa taarifa kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali, zoezi ambalo limekuwa likilalamikiwa na kupingwa kwa madai ya kukiuka taratibu. [149]
picha
Mapema wiki hii 50 Cent alitoa wimbo huo uitwao Officer Ricky, pia alitoa picha za Ross kupitia mtandao wake zikimwonyesha mwanamuziki huyo akiwa katika sare za polisi. [150]
rais
Hata hivyo, alisema malengo ya mapinduzi yanaonekana kutoweka ikilinganishwa na miaka nane ya rais wa kwanza, Hayati Abeid Amani Karume, ambayo ilionekana Zanzibar kunawiri katika maendeleo, ikilinganishwa na sasa. [151]
roho
Ubingwa wa Tanzania mmeshakosa, mnawania nafasi ya pili sasa, kinachotakiwa ni kuivaa roho ngumu na kutokubali kupoteza nafasi hii ya kombe la Shirikisho. [152]
rudi
Wachezaji wanapaswa kukaza misuli na kurejesha akili zao uwanjani kwa kuelewa kwamba, wana dakika 90 za kuamua kama wanataka kuendelea na michuano ya kimataifa msimu huu au la warudi wakaendelee na Ligi ya Tanzania ambayo miaka nenda rudi hata ubingwa wameshindwa kuchukua. [153]
saa
Magari hutozwa kiasi cha Sh1,000 kwa kuegesha gari kwa nusu saa kwenye eneo hilo. [154]
sare
Katika msimu uliopita wa Ligi Kuu ilianza kwa matokeo mazuri, lakini kadri siku zinavyokwenda ikaanza kuyumba kwa kufungwa na kulazimisha sare kadhaa, lakini mwisho wa siku ikabahatika kusalia kwenye nafasi ya pili na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho mwaka huu. [155]
sasa
IKIWA karibu mwaka mmoja sasa tangu kufariki kwa Gavana Daudi Balali, nyumba ya Benki Kuu (BoT) ambayo alikuwa akiishi, imekosa mkazi. [156]
sawa
Katika mtihani wa Maarifa (QT) watahiniwa 5,653- sawa na asilimia 27.02- ikiwa ni pungufu ya mwaka 2007 wakati asilimia 24.44 ya watahiniwa walifaulu. [157]
sio
Tukiongelea kiwanja sasa, sio Zhonghua tena, kitu kimesogezwa mbele mbele, kwa juu hivi, ..ili kila mdau aweze kusogea na kuona kinachofanyika. [158]
sisi
Shirika la kutetea Uhai la Pro-life Tanzania tunaona kuwa sheria hii itaangamiza uhai wa mtu, kwa sababu sisi tunaamini kuwa kutoka siku ya kwanza mimba inapotungwa tayari ni mtu," alisema mwanaharakati huyo. [159]
soka
Awali Msemaji wa chama cha soka cha Zanzibar (ZFA) Maulid Hamad Maulid alipinga wazo la Maximo na kusema si lazima kufuata mifumo ya ligi za nchi za nje kwani mfumo uliopo haujawa wa kizamani sana. [160]
suala
Akizungumzia suala hilo, Profesa Ndulu alisema kinachofanyika sasa ni ukarabati. [161]
tajiri
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [162]
tarehe
Sitaki kutaja tarehe kamili ya kuanza ligi hiyo, lakini ninachosema kwamba Ligi Kuu itaanza baada ya kukamilika kwa mambo mbali mbali muhimu," alisema Maulid bila ya kufafanuwa. [163]
tu
Shaibu alisema jumla ya wafanyabiashara 45 walikaguliwa na watatu tu ndio walikuwa wakiendesha biashara zao kwa mujibu wa taratibu za biashara ya vileo sambamba na kuwatoza faini wafanyabiashara 25 huku wafanyabiashara 12 wametozwa faini na kupewa onyo kali. [164]
tuzo
Mwanamuziki huyo alidai kuwa 50 Cent alikataa kusalimiana naye pale alipomfuata ili wazungumze wakati wa tuzo za BET zilizotolewa hivi karibuni. [165]
uko
Sasa Kazim ujue kwamba uko chini ya ulinzi, kwa sababu ni mgonjwa sana tutakufunga pindu hapa wakati tunaangalia namna ya kukufanyia, uko chini ya ulinzi,” alisema mkuu wa jeshi la polisi ambaye alionekana kusononeka sana kwa kifo cha yule mvumbuzi wa dawa. [166]
umma
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezindua kampeni ya kupambana na rushwa na vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya mali za umma, kikirusha tuhuma kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). [167]
uozo
Na hapo nikajikuta nimekaa chini huku harufu ya uozo ikiwa imeniletea kizunguzungu. [168]
ushauri
Ukisikiliza kazi za Mwasiti utabaini kuwa yeye ni tofauti kutokana na aina ya nyimbo zake zenye ushauri na nguvu kwa walengwa wake. [169]
usiku
Siku moja usiku akiwa nyumbani alitafakari sana hali ngumu ya maisha ambayo angeanza kuishi. [170]
uwanja
Mayanga amekuwa kivutio cha wachezaji na wapenzi wa soka wa Mtibwa Sugar kutokana na kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Tusker iliyomalizika mwishoni mwaka jana michuano ambayo ilifanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. [171]
vile
Nimewahi kupelekwa kituo cha polisi siku moja kutokana na mtu ambaye alikuwa anadaiwa nauli kunigeuzia kibao kuwa nimemuibia, niliteseka, lakini kwa vile sikuwa nimemuibia, polisi waliniachia," anasema na kuongeza kuwa matukio ya namna hiyo tayari ameyazoea. [172]
vileo
WAFANYABIASHARA sita wamefungiwa leseni zao za biashara kwa muda usifahamika kutokana na kuizuia mamlaka ya utoaji leseni za vileo kufanya kazi walipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa kujionea hali halisi baada ya kupata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi. [173]
vipi
Alipoulizwa atakabiliana vipi na ushindani wa namba, Kazimoto anasema: “Nitahakikisha anajitahidi na kupata namba katika kikosi cha kwanza. [174]
vita
Katika mkutano huo, ambao ulihudhuriwa na watu wachache, alisema Operesheni Sangara itakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Zanzibar baada ya wabunge na wawakilishi wa CUF kushindwa kupiga vita vitendo vya ufisadi tangu walipoanza kuingia Baraza la Wawakilishi. [175]
vitisho
Alilitaka Jeshi la Polisi kutoa taarifa ya matukio ya vitisho kwa viongozi wa Chadema yaliyotokea mwaka juzi na mwaka jana na kuandikiwa barua. [176]
vya
Tayari, bunge limepitisha miswada sita ya sheria ya afya ya jamii, viwango, wanyama pori, mamlaka ya maendeleo ya biashara, vyama vya siasa na marekebisho ya sheria mbalimbali. [177]
vyake
Machoni alionekana kama mwanamke mwingine yeyote, lakini vitendo vyake vilimfananisha na kondakta mwingine yeyote. [178]
wale
Katika matokeo hayo wavulana wanaongoza kwa asilimia 79.21 dhidi ya asilimia 72 ya wasichana kwa wanafunzi wa shuleni, huku wale wa kujitegemea wanaume wakiongoza kwa 62.65 dhidi ya asilimia 55.86 ya wanawake. [179]
walioko
Yanga itaondoka katikati ya wiki ijayo kwenda Comoro kwa mchezo wa marudiano wakiwemo wachezaji walioko kwenye ya taifa kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika. [180]
waliooza
Ilionekana wazi kwamba waliooza zaidi ni wale wa juu, kisha wale wa juu walikuwa wameambukiza wale wa chini uozo wao. [181]
wananuka
Na hata wachuuzi wenyewe walikuwa wananuka. [182]
wao
Oktoba mwaka 2008 jumla ya wanafunzi 233,848, sawa na asilimia 96.84 ya wanafunzi wa kidato cha nne nchini kote walifanya mtihani wao wa taifa. [183]
wapya
Katika kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mashindano CHAN nchini Ivory Coast, Maximo aliwaita wachezaji wawili wapya na wengine akiwarudisha wa zamani. [184]
wenu
Anakuwa mwema zaidi anapokuwa na shida, katika kipindi chako cha mafanikio urafiki wenu utanoga, ukifilisika atakugeuka. [185]
wenzao
Kikwete, Karume na Pinda wanachokiamini kinafanana na walichokiamini watumwa wa shimoni ambao waliukataa ukweli na kuendelea kuwapotosha watumwa wenzao. [186]
wiki
BAADA ratiba ya shughuli za bunge kuvurugwa wiki iliyopita, sasa kauli za serikali kuhusu azimio la bunge juu ya zabuni ya ufuaji umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond Development (LLC), imepangwa kutolewa keshokutwa. [187]
wimbo
RAPA kutoka Miami, Rick Ross amesema hataujibu wimbo wa 50 Cent ambao unamhusu yeye moja kwa moja. [188]
wote
Alisema kwa sasa wawakilishi wa CUF na CCM wanafanana kwa kuwa wote wanashindwa kusimama imara kuikosoa serikali iliyo madarakani na kupiga vita vitendo vya ufisadi, zaidi matumizi mabaya ya ardhi. [189]
yako
Nyumba anayoishi sasa imepata matatizo kidogo," alisema Ndulu na kuongeza kuwa matengenezo ya nyumba hiyo kwa sasa yako katika hatua za mwisho. [190]
yale
Akizungumza na Mwananchi jijini jana msemaji wa Chama cha kuogelea nchini Tanzania 'TSA' Alex Mwaipasu alisema kikosi hicho kitatangazwa baada ya mashindano ya Arusha wiki ijayo na yale ya Mwanza na Zanzibar mwezi Marchi. [191]
yao
Watahiniwa 347 wamefutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu, ambao 192 ni wa watahiniwa wa shuleni huku 155 wakiwa wa kujitegemea. [192]
yapo
Maajabu yapo kila mahali. [193]
yetu
Nafasi ya pili ni yetu tutacheza Kombe la Shirikisho mwakani tumeshajiwekea malengo makubwa tutakaporejea kambini baada ya mapumziko haya, alisema Mayanga. [194]
yeye
Happy ambaye ni mcheshi anasema watu wengi wanamuona mhuni kutokana na kazi yake hiyo, lakini ukweli ni kwamba yeye si mhuni wala mvuta bangi kama wanavyodhani. [195]
yuko
Hawezi kuweka kitu moyoni, tena yuko tayari kupoteza urafiki wenu kutumia mdomo wake. [196]
yule
Siamini kwani hivi sasa mimi si Mwasiti yule wa zamani, hii yote ni kutokana na kujituma kwangu sambamba na mafunzo ya nguvu na ushirikiano wa karibu kutoka kikundi cha Tanzania House of Talent (THT)," anasema Mwasiti. [197]
zangu
Naomba nichukue furasa hii kuwasabahi marafiki zangu popote mlipo. [198]
zetu
Ni dhahiri kabisa michezo inahitaji maandalizi ambayo hugharimu kiasi kikubwa cha fedha, ili kutengeneza timu iliyo imara na ambayo imekaa pamoja na kucheza kwa kuelewana , hivyo tunayasihi makampuni mbalimbali kujitokeza kukisaidia chama cha mpira wa kikapu BFT katika udhamini, ili kiweze kuandaa timu zetu za wanawake na wanaume. [199]
ziada
Ingawa kwenye soka lolote linaweza kutokea, lakini kwa uchezaji wa kikosi ninachokifahamu inabidi kufanyika kazi kubwa sana na ya ziada kuanzia kwenye benchi la ufundi mpaka wachezaji wenyewe. [200]