Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-23

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


adhma
Baada ya kushindwa kutimiza adhma yao ya kumwondoa Nkunda madarakani. [1]
afanye
Huenda unadhani hafanyi vile unataka afanye na hujamuambia au hujui unataka afanye nini. [2]
aheri
Lakini aheri hata siasa. [3]
ambao
Sisi ndio wenye dhamana kwa waliotuchagua na hata wale ambao hawakutuchagua. [4]
ana
Akizungumza baada ya kufungua soko la Mvumoni na kutoa boti na nyavu za uvuvi kwa vikundi mbalimbali, Rais Kikwete amesema kuwa amefurahi kusikia kuwa vikundi vilivyopewa boti na nyavu havikuchaguliwa kwa ubaguzi wa vyama ana itikadi. [5]
angalau
Tunaona kasi hii hairidhishi huku ukiangalia nchi yetu inahitaji wataalam wa taaluma hii kwa kiasi kikubwa na jambo ambalo hata Rais Kikwete alishaliagiza kuwa angalau kila mwaka kuwe na wahitimu 1,000," alisema Profesa Sarungi. [6]
au
Lakini Rais Kikwete aliwaambia Wazanzibari jana kuwa wasijidanganye kwa kukataa kushirikiana na CCM katika kuleta maendeleo kwa kuwa itawachukua muda mrefu au pengine isitokee kabisa kwa wapinzani wa serikali kushika madaraka. [7]
bali
Kitu ambacho wananchi wa Pemba walivutiwa nacho sio tu kumwona Waziri Mkuu bali pia ni vile alivyoanza kuwashukuru wananchi waliojitokeza kumpokea na baadaye kutoa hotuba yake ya kuwataka wananchi washirikiane katika kuleta maendeleo katika kisiwa chao na mwisho alimalizia kwa kutoa fursa ya kuulizwa maswali. [8]
bar
Wakati mke wake alikuwa amlala na yeye alikuwa bar akipiga pombe. [9]
beki
Alisema hanachotaka kwa sasa ni kuhakikisha kila beki katika timu hiyo anacheza kwa kujiamini anapokuwa uwanjani na siyo kwa papara na kuchanganyana. [10]
bila
Lakini alisema SMZ na serikali ya Muungano zitaendelea kuwaletea maendeleo wananchi wa Visiwani bila upendeleo wala kumbagua yoyote kwa sababu huo ndiyo mkataba kati ya serikali na wananchi, na kwa sababu kuwapa maendeleo ni dhamana ya serikali iliyo madarakani, na wala siyo wapinzani. [11]
bodi
BUNGE limeitaka serikali kuipa meno bodi ya wahandisi katika kusimamia na kukagua majengo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki wote ambao majengo yao hayakidhi viwango wa ubora. [12]
budi
KATIKA hali ya isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliwaambia wananchi kuwa wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja vikongwe ni hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea. [13]
bukta
Eti beki alimvuta bukta. [14]
bungeni
Midahalo yao itabakia bungeni tu. [15]
bwana
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na bwana mmoja aitwaye John Gottman unasema: namna vile watu wanavyogombana unaweza kujua ni kiasi gani watu wanapendana halikadhalika utaweza kujua ni maamuzi yatokanayo. [16]
chao
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Kindamba alimshukuru Mlanzi kwa msaada huo ambao una malengo mazuri ya kuendeleza michezo katika kijiji chao na wilaya ya Rufiji. [17]
chongo
Kweli ushabiki ni chongo. [18]
dhana
Katika taarifa tunazosoma katika magazeti dhana zinazowasilishwa hazileti maana inayokusudiwa. [19]
dunia
Katibu wa kamati ya ulinzi wa chama hicho, Mazee Rajab alidai kuwa utata huo umejitokeza katika vituo mbalimbali ambako baadhi ya majina yamejirudia na mengine ya watu waliofariki dunia kuorodheshwa katika vituo hivyo. [20]
duniani
Kuhusu uwekezaji, Balozi Parham alisema mazingira ya kufanya biashara Tanzania si mazuri kwani katika viwango vya Benki ya Dunia vya kibiashara, Tanzania ni nchi ya 127 kati ya nchi 160, ni rahisi kufanya biashara katika nchi 126 duniani kuliko kufanya biashara na Tanzania. [21]
endapo
Alisema endapo itabainika kwamba baadhi ya Mashirika hayakufanya kazi vizuri , ama kuwa na mapungufu katika uongozi ,Kamati yake italishauri Bunge na kuamuru mabadiliko katika mashirika hayo. [22]
es
CHAMA cha Wahadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (Udasa) kimetoa tamko la kuutaka uongozi wa chuo hicho kuwarejesha wanafunzi wote waliosimamishwa ili waweze kuendelea na masomo yao kama kawaida. [23]
eti
Tunaona ushabiki mtupu tunapoona hawa wanaojidai waumini wakitetea yasiyoteteka eti kwa sababu aliyetenda ni ‘mwenzetu’ wa dini yetu. [24]
faulo
Wachezaji hao walianza muda mrefu kutolea maneno machafu kutokana na Nyoso kumkwatua mchezaji mmoja wa Villa hivyo mwamuzi kuamuru ipigwe faulo. [25]
fulani
Neno kusadikiwa halifai hapa kwa sababu kusadiki ni kukubali kuwa kitu fulani ni cha kweli. [26]
fyongo
Mchezaji kiungo wa timu ya taifa alipiga fyongo na mpira ukatoka nje. [27]
gani
Lakini akitoa hadharani anabeza akisema hawa CCM watu gani? Lakini maji anakunywa. [28]
hadhari
Kabla ya majina haya kuwekwa hadhari kwa mara ya kwanza. [29]
hadi
Akitangaza kuahirishwa kwa safari hiyo kwa wajumbe wa kamati, Makigi alisema, hadi juzi mchana maandalizi yalikuwa yamekamilika na taarifa zilikwishatolewa kwa wabunge, lakini usiku wa siku hiyo, alipokea simu kuhusu kuahirishwa ziara hiyo bila ya maelezo zaidi. [30]
haina
Katika sekta ya elimu, elimu inayotolewa haina ubora wa kuridhisha. [31]
hakuna
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kitawasilisha bungeni hoja binafsi inayolenga kuilazimisha serikali kuhakikisha hakuna mtoto atakayekosa fursa ya kusoma kwa sababu ya umasikini wa wazazi wake. [32]
hao
Rais Kikwete ametoa kauli hiyo wakati CCM na CUF zikizidi kulumbana kuhusu matokeo ya uchaguzi wa rais ya mwaka 2005, ambayo wapinzani hao wanayapinga wakidai kuwa CCM iliiba kura, kama ilivyokuwa mwaka 2000 wakati hali ilipochafuka kutokana na CUF kuamini kuwa ilishinda uchaguzi huo. [33]
hapo
Tutambue kuwa siasa za uchaguzi ni siasa za uchaguzi, baada ya hapo mleta maendeleo ni serikali. [34]
haramu
Kwa hiyo ni sahihi kuandika, Mwanamume mmoja anayefahamika kwa jina la Khalfani Sheriveji amefariki dunia kwa Watu 120 wanaosadikiwa kuwa ni wahamiaji haramu wamekamatwa. [35]
hasa
Unaweza kusema lolote hasa inapokuwa usemaji wenyewe ni wa kufitini, yaani kudanganya watu, ili wakuchague. [36]
hasira
Ilibidi viongozi wa CUF wamwondoe maeneo hayo kumuokoa baada ya wanachama wa chama hicho wenye hasira kutaka kumpiga. [37]
hatua
Pamoja na serikali kutangaza hatua kadhaa za kupambana na wauaji hao, bado matukio ya kuuawa kwa watu hao wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiendelea kuripotiwa, lakini Waziri Pinda ameenda mbali zaidi katika kukabiliana na tatizo hilo alipotaka wauaji hao wauawe badala ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. [38]
hawa
Anapata taabu sana kuisifia serikali ya CCM hadharani, lakini akikaa na mkewe chumbani anasema kuwa hawa CCM kiboko kwa maendeleo. [39]
hawafikiwi
Mwandosya anasema kuwa, takribani watu milioni tano wanaoishi katika jiji la Dar es Salaam, Bagamoyo na Kibaha mkoani Pwani, hawafikiwi na huduma ya maji safi na salama. [40]
hawana
Hawa wengine hawana serikali. [41]
hewa
ZIKIWA zimebaki siku mbili kabla ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Mbeya Vijijini, Chama cha Wananchi (CUF) kimedai kuhujumiwa kikisema kimegundua orodha ya majina hewa yakiwa yamejirudia na mengine ya wafu. [42]
hicho
Watu wamekikataa chama hicho zamu hii. [43]
hii
Nafurahi kusikia kuwa tabia hii haiko kwenye mradi huu. [44]
hiki
Huku wananchi wakiwa kimya wakimsikiliza Waziri Mkuu alisema: "Ili kuimarisha mafanikio hayo ya kujivunia, CCM katika kipindi hiki itatekeleza yafuatayo: kuimarisha matunda ya mwafaka kwa faida na maslahi ya Wazanzibari wote, kuendelea kupiga vita kwa nguvu zote ubaguzi wa dini, kabila, kijinsia au asili ya mtu katika utoaji wa huduma na fursa mbali mbali za kijamii pamoja na kuendeleza umoja, mshikamano, amani na utulivu miongoni mwa wananchi wote na kuimarisha jumuiya mbali mbali za maendeleo na kijamii," alisisitiza Pinda. [45]
hili
Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili juzi, Prof. [46]
hilo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, katibu mkuu na mjumbe wa Udasa, Profesa Josephat Rugemalira alisema kuwa utaratibu huo, ambao umewekwa na uongozi wa chuo, ni mbovu na ambao umesababisha usumbufu kwa wageni, majirani na wananchi wa eneo hilo kwa ujumla. [47]
hivi
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matokeo mazuri ya miradi ya maendeleo, kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na shule za msingi, ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na shule za sekondari, kupunguza vifo vya watoto wadogo na pia kuna mafanikio katika mapambano dhidi ya malaria. [48]
hizi
Akizungumzia mabezo na kejeli za wapinzani wa CCM kuwa SMZ haijaleta maendeleo yoyote kwa wananchi, Rais Kikwete aliwaambia wananchi hao wa Kengeja akisema: "Wananchi, hizi ni fitina tu. [49]
hizo
Kuhusu rada ya Tanzania iliyonunuliwa Uingereza ambayo inadaiwa kuwa manunuzi yake yalifanyika katika mazingira ya rushwa na serikali ya Tanzania kudai kuwa ikithibitika kama bei ya rada ilikuwa imeongezwa itaiomba Uingereza irudishe fedha iliyozidi, Balozi Parham alisema wanaopaswa kurudisha fedha hizo ni wale waliochukua. [50]
huenda
Inachokupasa ufahamu kuwa kuziba kauli katika suala ambalo limekuudhi hupelekea madhara makubwa mbeleni katika mahusiano yenu na huenda ikaathirika afya yako. [51]
hujui
Kwa kuwa hujui aliyekuletea ana nia gani na mumeo. [52]
huku
Tayari wanafunzi wanne wamekamatwa kwa makosa ya kuandamana kutaka wenzao waliokataliwa kurudi chuoni, waruhusiwe huku viongozi wa serikali ya Chama cha Wanafunzi (Daruso) wakifikishwa mahakamani. [53]
humo
Alisema kuwa TFF iliridhia na kutoa baraka kwa mchezaji huyo kwenda kufanya majaribio nchini humo baada ya kuwa amekubaliana na uongozi wa klabu yake. [54]
husika
Tulichelewa kuanza kwa kuwa tulikuwa tunaweka utaratibu, sasa mambo yamekamilika na kila timu inatakiwa kuwa na timu ya watoto zitakazocheza kabla ya mechi husika ya Ligi Kuu," alisema Mwakalebela. [55]
huwa
Mpaka wakati huu tupo katika harakati za kumpatia visa ya kusafiria kwani tunatambua umuhimu wa nchi kuwa na wachezaji wa kulipwa ndiyo maana hata Maximo huwa nasisitiza hili"alisema Mwakalebela. [56]
huyo
Sasa utafanyaje hata kama huyo ndiye mwenye dhamani. [57]
huyu
Mimi niliongea na mwamuzi, sasa nashangaa huyu ananijia juu," alisema Moshi ambaye ni kaka ya Haruna Moshi wa Simba na Ali Moshi wa Polisi Moro. [58]
ijayo
Prisons itashiriki michuano hiyo, na wiki moja ijayo, itapambana na Khalij Sert ya Libya ya Libya, katika mchezo wa kwanza utakaofanyika. [59]
ikiwa
Kwa mujibu wa Rugemalira, baada ya kuona mapungufu hayo Udasa iliunda kamati mbili ambazo zimepewa majukumu tofauti ikiwa moja ni jukumu la kushughulikia chanzo cha migomo kwa wanafunzi na njia mbadala ambazo zitasaidia kupunguza tatizo la gharama za elimu ya juu. [60]
ila
Mlanzi alisema kuwa mbali ya kuendeleza michezo, amegundua kuwa timu ya Kilimani ina wachezaji wengi wenye vipaji, ila wanakosa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kutokana na kukosa vifaa vya kisasa. [61]
iliamua
Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Osha, Hamisi Kitumbo, alikanusha madai ya kuwepo kwa uzembe katika maandalizi kuhusu ziara hiyo na kwamba Coca Cola, iliamua tu kuahirisha ziara hiyo. [62]
imeanza
Polisi Morogoro imeanza kujinanusua baada ya kushinda mechi moja na kufungwa moja hivyo kufikisha pointi 15 mbele ya Moro United yenye pointi 13 huku Villa Squad nayo ikijitahidi kukwepa hali hiyo ya kushuka daraja baada ya kuifunga na Tanzania Prisons na kufikisha pointi 11 kabla ya kufunga na Simba juzi. [63]
imeanzisha
Ili kuboresha huduma kwa wakulima, Mamlaka imeanzisha vituo vya hali ya hewa na kilimo Matangatuani kisiwani Pemba, wilayani Mbozi katika Mkoa wa Mbeya na katika Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma. [64]
imebainisha
Katika taarifa yake kamati hiyo imebainisha kuwa miswaada hiyo ni pamoja na Muswaada wa Sheria ya Pembejeo (Fertilizers Act,2008); Muswaada wa Sheria ya Kanuni za Vinasaba vya Binadamu (The Human DNA Regulation Act, 2008) na Supplementary Appropriation Act, 2009 na hatua zake zote. [65]
ina
Simba ndio ina kazi kubwa ya kuisaka hata nafasi ya pili ili icheze michuano ya kimataifa baada ya kukosa michuano hiyo mwaka huu huku mwenyekiti wake Hassan Dalali akikaririwa akisema kuwa hata ubingwa wanaweza wakachukua. [66]
ingawa
Hata hivyo Balozi Parham alisema jitihada zinazochukuliwa na serikali kwa sasa zinatia moyo ingawa hazitoshi, kwani bado kuna mambo mengi zaidi ya kufanya kuhakikisha kwamba kunakuwa na utawala bora na udhibiti mzuri wa matumizi ya fedha za serikali. [67]
ipo
Ni muhimu kwa watu kukubali kuwa ipo serikali iliyoko madarakani hata kama wanaikataa jinsi ilivyoingia madarakani. [68]
iwe
Alipendekeza Dawasa na Dawasco iwe kampuni moja kubwa itakayosimamia miundombinu na usambazaji wa maji safi na uondoaji wa maji taka jijini na Pwani. [69]
iweze
Pamoja na hilo Profesa Sarungi alisema kuwa kamati yake imeitaka serikali kupitia sheria hiyo kuipatia bodi ya wahandisi kiwanja ili iweze kujenga jengo lake la kujitegemea ili iweze kuendesha shughuli zake kwa uhuru na ufanisi zaidi. [70]
juu
Hadi sasa mazungumzo baina ya vyama hivyo juu ya kuunda serikali ya umoja bado hayajafikia muafaka baada ya CUF kutangaza kujitoa. [71]
juzi
Waziri Pinda alionekana kukerwa na mauaji ya albino wakati alipopata taarifa kwamba kuna mama mwingine aliuawa usiku wa kuamkia juzi. [72]
kata
Tumegundua kasoro mbalimbali, kwa mfano katika kata za Santilya, Iwiji na Ilembo kuna majina 252 ya watu ambao tayari walishafariki dunia, na katika kata ya Ilembo kuna majina 25 ya watu ambao wamejiandikisha mara mbili," alisema. [73]
kiasi
Ukichanganya misaada yote ya maendeleo inayotolewa na jumuiya ya kimataifa, bajeti ya Tanzania ya mwaka huu ni kiasi cha dola za Marekani 6 bilioni ambazo ni asilimia 3 tu ya bajeti ya mwaka ya Wizara ya Afya ya Uingereza, lakini kiasi hicho kwa Tanzania kinatarajiwa kufanya kila kitu kwa watu milioni 40 na nchi yenye ukubwa mara nne kuliko Uingereza. [74]
kidogo
KOCHA wa timu ya Simba, Patrick Phiri amesema amegundua kuwepo kwa matatizo kidogo na kukosa kujiamini kwa mabeki wa timu yake. [75]
kila
Tutamwendeleza kila mtu kwa sababu dhamana ya maendeleo ni yetu katika serikali. [76]
kile
Nimesema kuwa tutatoa huduma za kijamii kwa wananchi wote bila kubagua kati ya wale waliotupigia kura, au wale waliokipigia kile chama kingine. [77]
kilimo
KATIKA ukurasa wa kwanza wa gazeti hili jana, kulikuwa na habari iliyomkariri Rais Jakaya Kikwete akisema kuwa, serikali yake imesitisha ununuzi wa magari ya kifahari kwa viongozi wa serikali ili fedha zitakazopatikana zitumike kwa ajili ya kununulia matrekta kama mojawapo ya juhudi za kuinua kilimo nchini. [78]
kipindi
Tutofautishe kipindi cha uchaguzi na kipindi cha maendeleo. [79]
kirefu
KWA kipindi kirefu sasa nimekuwa nikiandika makala kuhusu matumizi bora ya Kiswahili katika magazeti yanayochapishwa hapa nchini. [80]
kocha
Kwa sasa, Prison iko chini ya kocha Mshindo Msolla ambaye alishawahi kuwa kocha wa timu ya Taifa katika benchi la ufundi akisaidiana na Kocha James Nestory hivyo wanaihakikishia Watanzania ushindi mnono. [81]
kuandika
UAMUZI wa juzi wa Hakimu Mkazi wa Kisutu, kuwazuia waandishi wa habari kuandika chochote ndani ya mahakama hiyo wakati kesi ya watuhumiwa wa wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ni wa kushangaza kwa sababu ulilenga kuingilia uhuru wa vyombo vya habari na jamii kupata taarifa juu ya mwenendo wa kesi hiyo. [82]
kubuni
Tunashauri zitafutwe njia nyingine ukiwepo mjadala wa kitaifa kuzungumzia tatizo hilo, kubuni mikakati ya kuondoa ujinga, kuongeza elimu, kuongeza kipato na maisha bora ya watu kwa njia halali. [83]
kucheza
Ligi hiyo inaendelea tena leo kwa kuzikutanisha Moro United itakaposhuka kwenye Uwanja wa Taifa kucheza na Polisi Dodoma. [84]
kuchokwa
Afadhali hata mpira maana hatimaye mashabiki wataanza kudai mabadiliko lakini katika siasa, watu watashabikia weeeeeeeeeeeee huku chama fulani kimeshapondwa badala ya kupendwa, kimechekwa na kuchokwa na hata kuchukiwa kutokana na kuchakaa kwake. [85]
kuifuta
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, amepingana na msimamo wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma kuhusu kuifuta Kampuni ya Usambazaji Maji katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam (Dawasco), kuinusuru Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam, (Dawasa). [86]
kulala
Kwa Pinda hii ilikuwa ziara yake ya kwanza Kisiwani Pemba tokea ateuliwe kuwa Waziri Mkuu lakini pia yeye ni waziri mkuu wa pili kulala katika kisiwa hicho ukiacha aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo Dk Salim Ahmed Salim (kwao) ambaye aliwahi kutembelea maeneo mbalimbali na kulala. [87]
kulipwa
NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Henry Joseph Shindika anarajia kuondoka nchini Jumatatu kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM) kwenda Norway kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu ya Tromso. [88]
kumbe
BALOZI wa Uingereza nchini Tanzania anayemaliza muda wake, Philip Parham amesema suala la EPA liliwaweka katika wakati mgumu kwa sababu walibaini kuwa kumbe fedha za walipa kodi wa Uingereza na wengineo zinatumiwa vibaya. [89]
kumsikiliza
Ongeza umakini katika kumsikiliza. [90]
kupimia
Kinachotia moyo zaidi ni kufungwa kwa vituo vya kupimia hali ya hewa vinavyojiendesha vyenyewe katika maeneo ya Mtwara, Bukoba, Babati, Tabora, Kigoma na Kibondo. [91]
kusema
Unajua midomo kazi yake ni kusema. [92]
kusikiliza
Epuka dhana na kusikiliza maneno ya watu. [93]
kuua
Kauli ya Pinda, ambayo inaweka maswali katika suala la utawala bora, imekuja wakati ambao wananchi wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kuua vikongwe kutokana na imani za uchawi. [94]
kuvuruga
Baadaye viatu hivi vitatolewa kwa watoto yatima ili na wao waweze kumkumbuka aliyefanikiwa sana kuvuruga amani ya dunia, uchumi wa dunia na mazingira ya dunia, baada ya kuvuruga demokrasia ya dunia ndani ya nchi yake mwenyewe wakati wa ‘kuchaguliwa’ mara ya kwanza. [95]
kuweza
Maneno yanayofaa hapa ni mchanganuo wa mradi, kwa maana kwamba hakuna nchi hata moja iliyopeleka uchambuzi wa maandishi wa mradi ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya nchi. [96]
kuzidi
Lakini mara nyingi kunyamaza ni kuzidi kuzidisha matatizo. [97]
kuzuia
Mpaka leo hakuna ufumbuzi uliopatikana kuzuia mauaji hayo. [98]
kwake
Alisema taarifa za ziara hiyo zilikuwa zinagongana hasa kufuatia kitendo cha Mengi kukataa kwa madai kuwa hatokuwepo na kwamba, asingependa kuona wabunge wanatembelea kiwandani kwake, bila ya yeye kuwepo. [99]
kwanza
Katika taarifa yake iliyoitoa jana jijini Dar es Salaam, Chadema imesema kuwa imesikitishwa na utaratibu wa kudahili upya wanafunzi wa shahada ya kwanza unaoendelea UDSM na hivyo itawasilisha hoja hiyo binafsi kupitia kwa Waziri Kivuli wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambaye pia ni mbunge kwa chama hicho, Susan Lyimo. [100]
kweli
Mwanademokrasia wa kweli, akimaliza uchaguzi hushirikiana na wenzake katika kuleta maendeleo. [101]
kwenda
Ziara hiyo ilikuwa mahususi kwa ajili ya kwenda kukagua afya na usalama wa wafanyakazi wa kiwanda hicho, kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam. [102]
kwetu
Pamoja na kupoteza mechi mbili mfululizo, hiyo si sababu kwetu ya kufanya vibaya kwa mechi inayotukabili kwani tunawategemea wachezaji wetu ambao walikuwa wagojwa lakini kwa sasa wanaendelea vizuri na watacheza katika mechi hiyo. [103]
la
Rais, ambaye anategemewa kutoa suluhisho la muafaka baina ya Chama cha Wananchi (CUF) na CCM baada ya kuvunjika kwa mazungumzo, alisema hayo wakati aliposalimia wananchi kwa nyakati tofauti jana, akiwa kwenye siku yake ya pili na ya mwisho ya ziara yake katika Kisiwa cha Pemba. [104]
lake
Mwaswale, aliyekuwa amefikishwa katika ofisi za CUF zilizo katika tarafa ya Mbalizi, alikiri kosa lake. [105]
lazima
Yakitangazwa matokeo hata kama hukuridhika nayo ni lazima ukubali kushirikiana na washindi. [106]
leo
Umoja wa vijana mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbno na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena," alisema waziri mkuu. [107]
ligi
ZIKIWA zimebakia mechi tisa ligi ya Tanzania Bara kabla ya kumalizika mabingwa watetezi Yanga wanahitaji kushinda mechi tano kujitanga ufalme, huku wapinzani wa jadi Simba wapo kwenye harakati za kutafuta nafasi ya kufuzu kwa michuano ya Afrika mwaka mwakani. [108]
lina
Waziri Pinda, ambaye ameanza ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kuhamasisha vita dhidi ya mauaji ya vikongwe na albino, aliutaka Umoja wa Vijana wa CCM kuongoza vita hiyo, akisema lina jeshi zuri. [109]
lolote
Madai kuwa serikali haijafanya lolote wala chochote ni fitina tu za kisiasa. [110]
lugha
Katika lugha ya Kiswahili neno shadadia halimo na ni makosa kubuni neno ambalo siyo la Kiswahili na kulitumia bila ya uangalifu na kwa kuzingatia taratibu za uandishi. [111]
lukuki
MALALAMIKO juu ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, yamezidi kuwa mengi huku lawama lukuki zikipelekwa kwa Kmpuni ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (Dawasco). [112]
maana
Dawasco ni kampuni ya kutoa huduma ya kusambaza maji, ukisema unaiondoa, maana yake mzigo wote wa uzalishaji na usambazaji wa maji unaibebesha Serikali ambayo ni mmiliki wa Dawasa,"alisema. [113]
mabango
Katika hatua nyingine, chama cha CUF kimemkamata mwanachama wa CCM kikidai kuwa alikuwa aking'oa mabango yenye picha za mgombea wa CUF, Daudi Stembela Mponzi. [114]
mabao
Ukiachana na msimamo wa ligi kwenye uapachikaji wa mabao bado mshambuliaji wa Yanga, Boniface Ambani anaongoza kwa ufungaji akiwa maeziona nyavu mara 13 akifuatiwa Mkenya mwenzake Beny Mwalala, huku Hussen Bunu wa JKT na Orji Obina wa Simba wote wameshafunga mabao sita kila mmoja. [115]
malengo
Alisema lengo lake ni kuhakikisha Simba inafanya vizuri na wachezaji wote wanacheza mpira wa kufundishwa na wenye malengo uwanjani. [116]
mawili
Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma, kimeendelea kuboreshwa kwa kujengewa madarasa mawili zaidi. [117]
mbaya
Taarifa hizo zinahusu utabiri wa hali ya hewa wa kila siku na wa msimu, na utoaji tahadhari ya hali mbaya ya hewa na majanga yanayohusiana na hali ya hewa. [118]
mchango
Lakini hata hao wana CCM kidogo waliopo wanapaswa kutunzwa na kuthaminiwa ili nao wajisikie wana thamani katika ujenzi wa demokrasia kwa kuchagua chama wanachokitaka badala ya kupuuzwa na kuonekana kuwa ni wachache hivyo hawana mchango katika gurudumu la kuendeleza demokrasia nchini. [119]
mchezaji
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Frederick Mwakalebela alisema kuwa tayari mchezaji huyo amekutana na Kocha Mkuu wa Taifa Stars , Marcio Maximo na kupata baraka zote. [120]
mishale
Amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana mishale ya saa 10:30 katika eneo la Sabasaba. [121]
mitaani
Aliandika neno kulingana na jinsi linavyotumika mitaani. [122]
mitambo
Akizungumza katika majumuisho ya ziara ya wabunge 21 wa Kamati ya Kilimo na Ardhi katika mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini, Mwandosya alisema tatizo la wizi wa miundombinu latakoma kwa ulinzi shirikishi. [123]
mke
Inadaiwa kuwa mume wa mama huyo alichukizwa na kitendo cha mke wake kung'ang'ania kwenda kliniki kupima, hivyo alimpiga kwa fimbo kichwani na kuzirai kisha kumkata kwa panga. [124]
mmoja
Nimeambiwa kuwa juzi wilayani Sengerema kuna mama mmoja ambaye ni mlemavu wa ngozi amekatwa mkono na wauaji wakaondoka na mkono huo na tayari mama huyo amekufa," alisema Pinda na kusisitiza kushughulikia wauaji hao. [125]
mpango
Mwakalebela alisema kuwa mchezaji huyo ambaye amefanyiwa mpango wa kwenda nchini humo na mmoja wa mawakala wanaotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ataongozana pia na mchezaji mwenzake kutoka klabu ya Simba, Emeh Izuchukwu. [126]
mtaa
Alisema ili kufanikisha suala hilo la kijamii la uchangiaji watoto wanaoishi katika mazingira magumu, ofisi ya mtendaji kata pamoja na kamati ya mazingira hatarishi mtaa wa Makangarawe zinatakiwa kushirikiana na mratibu wa mpango huo ili kuwawezesha kupata wafadhili. [127]
mumeo
Kubeba ulichoambiwa ukakitumia kama fimbo ya kumhukumu mumeo ni makosa makubwa. [128]
mwa
Kazi ya maendeleo haiko mikononi mwa mbunge ama mwakilishi. [129]
mwezi
Hali kadhalika ATCL ilikuwa 'wodini', kwa kusimamisha usafiri wa ndege karibu mwezi mmoja, lakini inatarajia kuanza kurusha ndege zake leo, wakati nayo TRL imekuwa na usafiri usioaminika na wenye usumbufu mkubwa kwa abiria. [130]
mwingi
Ugomvi mwingi wa wanawake wengi unatokana na maneno ya kuambiwa ama kudhania. [131]
na
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete jana alitonesha machungu ya siasa za visiwani wakati alipowaambia wapinzani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuwa wanaweza kuchukua muda mrefu kabla ya kupata nafasi ya kuunda serikali, ama pengine wasiipate kabisa, na hivyo ni muhimu kwao kushirikiana na serikali ya CCM katika kuwaletea wananchi maendeleo. [132]
nao
Akihutubia wakati wa kufungua mkutano wa 16 wa Shirikisho la Vyama vya Kuweka na Kukopa (SCCULT) kwenye ukumbi wa Chuo cha Utumishi Umma mkoani hapa, Waziri Pinda alisema iwapo wananchi wataendelea kuwahurumia wauaji hao ambao wanatafuta viungo vya albino wakitegemea mahakama itatenda haki huku nao wakiongeza kasi ya mauaji kwa Watanzania, watakuwa wanakosea. [133]
naye
Muhimu kushirikiana naye. [134]
nayo
Ukweli ni kwamba ipo na ni muhimu kwa watu wote kushirikiana nayo katika kuleta maendeleo. [135]
nchini
Mauaji ya albino yamekuwa ni tatizo kubwa nchini na hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. [136]
ndani
Hata hivyo Kabwe alifafanua kwamba katika kikao cha Bunge cha mwezi huu, watajadili suala la ATCL na kuangalia njia za kutatua matatizo yaliyoko ndani ya Kampuni hiyo. [137]
ndio
Sisi ndio wenye dhamana ya serikali na wala hatubagui. [138]
ndugu
Mafanikio yamepatikana mengi ndugu wananchi katika elimu, katika barabara. [139]
ngazi
Mzee Mussa alisema Pemba wapo wana CCM tena wenye kuumwa na chama chao isipokuwa uongozi uliopo ni mbovu na haufai kutokana na kuwa wadanganyifu na hawataki kuwashirikisha wananchi wa ngazi za chini katika maamuzi ya kichama. [140]
ngumu
Ligi hiyo ambayo imekuwa ni ngumu sana hivi sasa huku kila timu ikijinasua ili iwe juu na kukwepa kushuka daraja timu za Polisi Morogoro, Moro United, Polisi Dodoma na Villa Squad ambazo zilimaliza vibaya mzunguko wa kwanza zinapigana vikumbo kuhakikisha kila mmoja hashuki daraja. [141]
nia
Tumeshangazwa na baadhi ya taarifa hasa kuhusu fedha zilizopatikana kutokana na zile zilizorudishwa na watuhumiwa wa EPA, ambazo zilikusudiwa kuwasaidia wakulima kuchelewa kuwafikia wahusika na hivyo kufanya nia njema ya Rais Kikwete kukumbwa na upinzani usiotarajiwa. [142]
nini
Na inawezekana ikawa hujui nini kamwambia mumeo kuhusu wewe. [143]
nyingi
Kwa kawaida, Kamati hiyo inashughulikia mashirika 180 yenye thamani ya Sh 4.4 trilioni jambo ambalo Kabwe alisema ni fedha nyingi na ni lazima yahakikiwe mara kwa mara. [144]
nzuri
Alisema kuwa mfano nzuri ni wa Marekani. [145]
pale
Timu itakuwa kambini mpaka pale itakapocheza mchezo wa kirafiki na Zimbabwe mwezi ujao, lakini baada ya hapo tutaangalia uwezekano wa kupata mechi nyingine ya kujipima nguvu hii itategemeana na muda utakavyoruhusu,"alisema katibu huyo. [146]
pamoja
Tupambane wakati wa uchaguzi, baada ya hapo tujenge nchi yetu kwa pamoja. [147]
papo
Hivyo alisema kwamba kuanzia sasa mtu yeyote atakayemuona mtu amemkata shingo au mkono mweziwe basi naye auawe papo hapo hii itakuwa ndiyo dawa kwani vingozi wote tumechoka na mauji hayo. [148]
pia
Rais pia alisema kuwa ni fitina za kisiasa kwa wapinzani wa SMZ kuibeza na kuikejeli serikali hiyo kwa madai kuwa haijaleta maendeleo yoyote Tanzania Visiwani. [149]
picha
Mawakala hao walidai kugundua majina mengi yamerudiwapamoja na kubadilishwa picha na mengine ya waliofariki kutoondolewa katika darfari hilo. [150]
poa
Na kwa kuwa Makengeza Enterprises haitaki watu wapekue baadaye na kupata funza badala ya mafunzo, viatu maalum vitauzwa kwa bei poa hapohapo kwenye tamasha. [151]
pointi
Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 36 itapofanikiwa kushinda mechi zote hadi mwisho itafikisha pointi 63 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwani Kagera Sugar yenye pointi 23 na iliyo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hata kama ikishinda mechi zake zote itakuwa na pointi 50 ambazo zitakuwa bado hazijafikia pointi za mabingwa hao watetezi. [152]
rafiki
Ninaye rafiki yangu ambaye alikuwa mpigania uhuru wa Afrika Kusini. [153]
saa
Mwana CCM huyo anayejulikana kwa jina la Saja Daudi Mwaswale, ambaye ni ofisa mtendaji wa kijiji cha Itimba, alikamatwa na katibu wa wilaya wa chama cha Wananchi CUF akidaiwa kungo'a mabango katika kijiji hicho muda wa saa 3:00 asubuhi. [154]
safi
Wao wacha waendelee kutia fitina, kubeza maendeleo, lakini maji safi wanaendelea kunywa; barabara wanaendelea kupita wakipeperusha bendera zao kwa sababu zinateleza kama mgongo wa ngisi. [155]
salaam
Ujinga gani huo! Kwanza hawajui maana ya salaam hizi, na pili ushabiki wao unawafanya wachekwe na kuchokwa na ujinga wao. [156]
sana
Maana ukisubiri hiyo serikali yako, inaweza ikachelewa sana ama pengine isije kabisa katika uhai wako," alisema. [157]
sare
Dalali alisema michezo yao yote uiliyobakili lazima washinde yote na hawatakubali sare kwani wamepania kutwaa ubingwa na nafasi ya pili na ya tatu ni ya timu nyingine si Simba. [158]
sera
Karibu theluthi mbili ya wanafunzi wa chuo hicho wamezuiwa kurejea chuoni kwa madai kuwa wameshindwa kutimiza masharti, yakiwemo ya kulipa sehemu za gharama za elimu baada ya chuo hicho kufungwa mwishoni mwa mwaka jana kutokana na wanafunzi kugomea sera ya uchangiaji elimu, wakidai kuwa inabagua. [159]
si
Inasemekana kuwa fedha za ziada za manunuzi ya rada hiyo zililipwa kama ‘kamisheni’ na rushwa kwa hivyo waliochukuwa ikiwa ni Waingereza au Watanzania ndio watakaopaswa kuzirudisha na wala si serikali ya Uingereza. [160]
sifa
Imefafanua kuwa utaratibu huo ni batili kwa kuwa unakiuka mchakato mzima wa udahili ambao hufanywa na vitivo vinavyotakiwa kuhakiki fomu za mwombaji na kuangalia vigezo, vikiwemo ufaulu wa mwanafunzi katika matokeo ya kidato cha sita au sifa zinazofanana na hizo. [161]
sio
Alisema utaratibu uliopo sasa wa kuwarudisha wanafunzi chuoni kwa kuwafanyia udahili upya baada ya kulipa ada zote za mwaka wa masomo 2008/09 kwa kufuata masharti yaliyowekwa na kuweka ulinzi mkali, sio mzuri na unasababisha usumbufu mkubwa. [162]
sivyo
Anayewaongopea vinginevyo, mwambie hivyo sivyo. [163]
soka
SHIRIKISHO la soka Tanzania, TFF imetangaza siku mbili za mapumziko kwa wachezaji wa timu ya Yanga kabla ya kujiunga kwenye kambi Taifa Stars Februali 3 au 4 tayari kwa mandalizi ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN). [164]
tena
Wamemchagua Barack Hussein Obama, Mswahili, tena baba yake Jaluo. [165]
tu
Rais aliwaambia wananchi wa Pemba, ambako Chama cha Wananchi (CUF) kina nguvu kubwa na ambako huzoa karibu majimbo yote, kuwa wanayo haki ya kuendelea kumchagua yoyote wanayemtaka ili awe mbunge ama mwakilishi, ili mradi tu waendelee kukabidhi CCM dhamana ya kuendesha serikali. [166]
tuna
Najua watu watachukulia matokeo ya mechi za Ligi Kuu kuwa ndiyo kigezo cha sisi kutiofanya vizuri, lakini nasema hilo si tatizo, tuna uhakika wa kufanya vizuri," alisema. [167]
uamuzi
Kilichowafurahisha wananchi wa Pemba ni uamuzi wa Pinda kutenga siku angalau moja kwa kutembelea maeneo kadhaa na kuzungumza na wananchi, hasa kwa kuwa viongozi wachache ndio waliowahi kufikia uamuzi kama huo wa kuzungumza na wananchi moja kwa moja kama alivyofanya yeye. [168]
ugumu
Tusingetoa lawama kwani mwanzo wa kila kitu una ugumu wake na hasa kwa nchi zinazoendelea Tanzania ikiwa mojawapo. [169]
uhakika
Mwenyekiti wa timu hiyo, Salumu Chambuso alisema timu yao wana uhakika itafanya vizuri katika mashindano hayo kwani kwao ni muhimu kushinda. [170]
una
Phiri aliongeza timu hiyo inafanya vizuri kwa sasa kwa kuwa amebadilisha mfumo kutoka waliokuwa wanacheza awali na kucheza mfumo mpya na anaona una mafanikio na atahakikisha kuwa timu yake inashinda mechi zote zilizobaki. [171]
unyama
Enzi zile, daima alinielezea unyama wa makaburu, unyama wa kutisha. [172]
upya
Aliongeza kuwa ili uweze kutatua matatizo yaliyojitokeza, uongozi wa chuo hicho ulipaswa kuangalia upya utaratibu mzuri wa udahili kwa wanafunzi hao ambao utasaidia kupunguza usumbufu chuoni hapo na kuangalia mustakabali mzima wa hadhi ya chuo hicho na taifa kwa ujumla. [173]
uwezo
Tumeamua kuwapa uwezo huo ili kuwaongezea heshima za kuchunguza utitiri wa majengo yasiyokuwa na ubora na viwango vya ujenzi vinavyotakiwa," alisema. [174]
uzazi
Tukio pia hili linatupa picha kwamba, elimu ya afya ya uzazi bado watu wengi hawajaipata nchini hususan maeneo ya vijijini, hivyo pamoja na harakati za kupiga vita ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake, elimu ya uzazi itolewe kwa wanaume wote hasa wa vijijini. [175]
vema
Hata hivyo kwa kuwa uchunguzi juu ya suala hilo unaendelea kwa upande wa Uingereza na hata kwa upande wa Tanzania, ni vema tusubiri matokeo ya uchunguzi huo," alisema Balozi Parham. [176]
vikuu
Hatua hiyo ya Chadema imekuja huku wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakipinga mchakato wa kudahili wanafunzi upya baada ya vyuo vikuu kufunguliwa. [177]
vile
Hata hivyo alisema bado zipo changamoto kubwa zinazoikabili Tanzania katika miradi ya maendeleo kama vile vifo vya kinamama wajawazito, utapiamlo uliokithiri kwa watoto na hata vifo vya watoto wachanga. [178]
vya
Rais Kikwete alisema kuwa ni wajibu wa vyama vya siasa kujua kuwa kila mtu anatawala kwa zamu yake kama anachaguliwa na wananchi lakini muhimu ni kushirikiana. [179]
vyuo
Hata hivyo Profesa Sarungi alisema kuwa idadi hiyo ya wahandisi wazawa bado haitoshi kwani takwimu zinaonesha kuwa ni wahandisi 500 tu ndiyo wanaohitimu kwa mwaka katika vyuo mbali mbali. [180]
wafuasi
Ni kweli nimeng'oa mabango hayo," alisema Mwaswale alikiri alipoulizwa na wafuasi hao. [181]
wakazi
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wamesisitiza umuhimu wa kuunganisha kazi za Dawasco na Dawasa ili kuongeza ufanisi katika huduma ya maji. [182]
wake
Tumeamua kumpeleka kituo kikuu cha polisi mkoani Mbeya ili sheria ichukue mkondo wake," alisema Mazee. [183]
wakuu
Hali hiyo imesababisha kwa kiasi kikubwa watu kuamini kwamba Pemba hakuna wana CCM ingawa hiyo inaweza kuonekana kama ni kweli kwani inatokana na viongozi wakuu walivyokitupa kisiwa hicho kiasi cha watu kukosa imani na chama chao. [184]
wana
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Prisons ya Mbeya wamewataka mashabiki wake kutokatishwa tamaa na matokeo ya Ligi Kuu kwani wana uwezo wa kufanya vizuri katika michuano ya klabu Afrika. [185]
wanaishi
Sio mtoto huyo tu, wapo watoto wengi katika maeneo hayo ya Makangarawe ambao wanaishi katika mazingira magumu na ambao wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa jamii. [186]
wananyimwa
Wako Wakristo ndani ya nchi za Kiislamu ambao wananyimwa haki zao na wako Waislamu ndani ya nchi za Kikristo ambao wananyimwa haki zao vilevile. [187]
wao
Kazi ya wabunge wao na wawakilishi wao ni kufoka tu. [188]
wasio
Maamuzi ya zimamoto hayatawasaidia albino KUANZIA miaka ya 1970 jamii yetu imekumbwa na wimbi la mauaji ya watu wasio na hatia kutokana na kile kinachodaiwa imani za kishirikina. [189]
wawe
Na sasa si suala la Waislamu tu, wawe Waislamu wenzetu au Waislamu waleee. [190]
wewe
Hivi wewe hutaki kushiriki na serikali iliyopo ukingojea serikali yako. [191]
wiki
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, waliishutumu Osha kwa maandalizi hafifu yaliyosababisha kukwama kwa ziara hiyo kwa siku mbili mfululizo ndani ya wiki hii. [192]
yao
Rais Kikwete alisema kuwa ni muhimu kwa serikali kuendelea kutoa huduma kwa wananchi bila kubagua kwa sababu serikali ndiyo yenye dhamana ya kuleta maendeleo, akisisitiza: "Maana wao hawana serikali, kazi yao na wabunge wao na wawakilishi wao ni kufoka tu. [193]
yenu
Naamini kuwa kupitia msaada huu, timu yenu itafanya vema katika ligi na vijana wengi kujitokeza kujishughulisha katika mchezo wa soka ambao kwa sasa ni ajira," alisema Mlanzi wakati akikabidhi msaada huo. [194]
yeye
Hata kama hukuridhika na jinsi mwenzako alivyoshinda, yeye ndiye kashinda, yeye ndiye yuko madarakani. [195]
yule
Na ni vyema ukaongea naye ili upate ukweli kwa kusema wasiwasi wako, au kile ulichoambiwa kwa kumkutanisha na yule aliyesema itasaidia kuondoa migogoro yenu. [196]
zaidi
Mpaka sasa, zaidi wa wanafunzi 2,000 hawajarejea chuoni hapo kutokana na kushindwa kutekeleza masharti yaliyowekwa na uongozi huo. [197]
zake
Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia amekuwa mstari wa mbele kupiga vita mauaji hayo, alitofautiana na Waziri Pinda katika moja ya hotuba zake aliposema kuwa adhabu ya kuua haitofautishi muuaji wa albino na muuaji mwingine na kwamba watakaopatikana na hatia ya kuua albino, atakabiliana na adhabu ya kifo kama ilivyo kwa muuaji mwingine. [198]
zetu
Aliuagiza Umoja wa Vijana wa CCM kuhakikisha mauaji hayo yanatokomezwa kabisa, akisema kuwa ni jeshi zuri ambalo likiamua kutokomeza kabisa mauaji ya vikongwe na ndugu zetu maalbino inawezekana. [199]
zote
Hii ni kazi na dhamana ya serikali zote mbili ya SMZ na Muungano. [200]