fasihi
aina za fasihi hariri
- fasihi simulizi
- fasihi andishi
fasihi simulizi hariri
fasihi simulizi ni kazi ya sanaa iliyohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo(ni sanaa ya kimapokezi) kama vile hadithi, ngano, maigizo na vitendawili. Fasihi simulizi hutumia ishara ili kupitusha ujumbe kwa wanajamii. Fasihi simulizi uhusisha fanani(mtendaji), utendaji na hadhira.
maigizo au sanaa za maonyesho au michezo hariri
Aina ya neno hariri
Nomino
Umoja hariri
Igizo
Wingi hariri
Maigizo
Ngeli hariri
i-zi(kamusi teule ya kiswahili) li-ya(kamusi ya kuswahili sanifu)
Maana hariri
Tendo la kufanya afanyavyo mwengine. Kuiga maneno au matendo au yote. Maigizo hushirikisha michezo ya kuigiza na maonyesho au maonesho ambayo huigizwa kimyakimya au kwa kusimulia mambo fulani yanayomhusu binadamu. Lengo moja huwa ni kuonesha utamaduni wa jamii fulani. Huweza kutokea mahali popote , wakati wowote bila uwepo na maandalizi ya mapema.
Michezo huweza kuwasilishwa kupitia ushairi wa utendaji wa mambo ya kijamii inayohusisha utumiaji wa viungo vya mwili na maneno kuwasilisha habari.
Maigizo huwa na umbo la tamthilia.
Maneno au/na matendo ya binadamu hutokea kwa wingi katika maigizo na hupewa umuhimu mkubwa.
fasihi andishi hariri
fasihi andishi ni kazi ya sanaa katika maandishi kama vile riwaya na tamthilia.
chanzo cha neno hariri
Kiarabu
aina ya neno hariri
- kivumishi
- nomino
maana kama kivumishi hariri
-enye lugha safi;-enye kutumia lugha safi na nzuri
Nomino hariri
ngeli hariri
i-zi
maana hariri
Tafsiri hariri
- Kiingereza: literature (en)